HOUSIGELI (Mfanyakazi wa ndani ) amnyonga mtoto na kumtupa kwenye dimbwi la maji machafu
Hausigeli aliyejulikana kwa jina moja la Ester (14) yupo matatani kwa madai ya kumuua mtoto Arafat Allan (3) kwa kumnyonga shingo na kumpiga na kitu kizito kichwani kisha kuutumbukiza mwili wake kwenye dimbwi la maji machafu. Tukio hilo lilijiri Jumapili iliyopita Mailimoja, Kibaha mkoani Pwani ambako marehemu alikuwa akiishi na wazazi wake. Akizungumza kwa uchungu, mama mzazi wa mtoto huyo, Zakia Peter ambaye amelazwa katika Zahanati ya Kellen kutokana na mshtuko wa kifo cha mwanaye, alisema siku ya tukio, hausigeli huyo aliyekuwa na siku mbili tangu aanze kazi aling’ang’ania kutumwa sokoni saa mbili asubuhi ambapo alimkubalia na kumuagiza mboga. AONDOKA NA MTOTO Bila mwanamke huyo kujua, msichana huyo alimpitia Arafat kwa jirani alikokuwa akicheza na wenzake na kuondoka naye kwa madai anamsindikiza. “Nilipoona muda unasonga mbele bila hausigeli kurudi na mtoto nilianza kuwatafuta,” alisema mama wa marehemu. Akasema aliwatafuta kwa muda mrefu bila mafanikio mwisho...