Posts

Oscar Pistorious asomewa hukumu kwa kosa la kumuua mpenzi wake

Image
Mwanariadha wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius aliyekuwa nakabiliwa na shtaka la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp leo amesomewa hukumu ya kesi hiyo nchini Afrika Kusini. Pistorius amehukumiwa kifungo cha miaka 6 gerezani kwa kukutwa nahatia ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kwa kumpiga risasi. Pistorius alitenda kosa hilo Februari 13, 2013 ikiwa ni usiku wa kuamkia siku ya Valentine Day na inaelezwa alimpiga mpenzi wake risasi kwa madai alidhani ni mwizi aliyekuwa amejificha bafuni.

Aishi na risasi miaka nane

Image
Hassani Athumani akiugulia. Na Gregory Nyankaira, UWAZI MARA: Ama kweli kabla hujafa hujaumbwa! Kijana Hassani Athumani (30) mkazi wa Kiabakari, Kata ya Kukirango, Wilaya ya Butiama, mkoani Mara anaishi na risasi mwilini kwa miaka nane sasa huku akiwa anasikia maumuvi makali na mwili wake ukiwa umejaa vidonda kutokana na kulala muda wote. Kijana huyo amepata masaibu hayo baada ya kujeruhiwa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi Machi 6, 2008. Hassani Athumani akiwa na mama yake mzazi na mwanaye. Akisimulia juu ya tukio hilo Ijumaa ya wiki iliyopita nyumbani kwao akiwa amelala huku akitokwa na machozi kutokana na kudhoofika mwili wake kuanzia sehemu ya mgongo aliyopigwa risasi hadi miguuni, Hassani alikuwa na haya ya kusema: “Hiyo Machi sita mwaka 2008 tulikuwa tunacheza disko na wenzangu katika ukumbi mmoja uliopo Kiabakari, ghafla saa 4.30 usiku, majambazi yakiwa yamevalia makoti meusi na kufunika nyuso zao, yalivamia katika ukumbi huo n

NORWAY YATOA MSAADA KUSAIDIA WAHITIMU WAHANDISI WANAWAKE KUJIENDELEZA

Image
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Mhandisi Profesa. Ninatubu Lema na Balozi wa Norway hapa nchini Mhe. Hanne – Marie Kaarstad wakitia saini makubaliano ya msaada wa Dola za Kimarekani milioni 2 kwa ajili ya kuwawezesha wahitimu wa Kike wa masomo ya Uhandisi nchini kujiendeleza kwa kupata uzoefu na kusajiliwa kuwa Wahandisi kamili. Programu inayoanza 2016 – 2021. Wanaoshuhudia utiwaji wa saini ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani (nyuma kushoto). Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani akizungumza wakati wa hafla fupi ya Kutiliana saini baina ya Bodi ya Usajili wa Waandisi (ERB) na Serikali ya Norway kuhusu msaada wa kuwawezesha wahitimu wa Kike wa masomo ya Uhandisi nchini ili waweze kujiendeleza kwa kupata uzoefu na kusajiliwa kuwa Wahandisi kamili leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Balozi wa Norway hapa nchini Mhe. Hanne – Marie Kaarstad na Mwenyekiti wa Bodi

MABADILIKO RATIBA YA MAZISHI YA MHE. BEATRICE SHELUKINDO - SASA KUFANYIKA KESHO NA SIO LEO HUKO OLOIRIEN JIJINI ARUSHA

Image
  Familia ya William H. Shelukindo inapenda kuwataarifu kuwa mazishi huko Arusha ya Mpendwa wao Beatrice Matumbo Shelukindo Mbunge wa zamani wa Kilindi sasa yatafanyika kesho siku ya Alhamisi tarehe 7/7/2016 na sio leo Jumatano tarehe 6/7/2016 kama ilivyotangazwa awali. Mazishi yatafanyika kesho saa tisa alasiri pale pale eneo la Oloirien jijini Arusha. Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa. Jina la Bwana Lihimidiwe. AMEN

Kisa kukataliwa kujiunga na ISIS, mapacha wamuua mama yao, wamjeruhi baba!

Image
MAPACHA wawili wamemuua mama yao mzazi na kuwajeruhi baba mzazi na kaka yao kwenye makazi yao yaliyopo Riyadh, Saudi Arabia baada ya kuzuiwa kujiunga na kundi lenye itikadi kali la wapiganaji wa ISIS. Mapacha Khaled na Saleh al-Oraini wenye umri wa miaka 20, wamemwua mama yao Haila aliyekuwa na umri wa miaka 67, walikamatwa na kushikiliwa na vikosi vya usalama vya nchi hiyo wakati wakijaribu kutoroka kwenye mpaka wa Yemen. “Mbali na kumuua mama yao mzazi, pia walijaribu kumuua baba yao mzazi na kaka yao mkubwa ambao wamelazwa hospitalini kwa matibabu. Vilevile  wanahusishwa na mauaji yaliyofanyika June 24 mwaka huu ambapo nchini humo watu kadhaa walijeruhiwa na kuuwawa”. Alisema Msemaji wa Jeshi la Saudi Arabia, Mansour al-Turki.  

Waziri Mkuu aongoza Swala ya Eid El Fitr jijini Dar

Image
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa akitoa mawaidha  mbele ya waumini wa kiislamu katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu Majaliwa akiendelea kutoa mawaidha yake kwa waumini hao ambao hawapo pichani.            Mufti Mkuu wa Tanzania, Shekh Abubakar Zubery akitoa mawaidha yake mbele ya waumini wa kiislamu. Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa akiongea na waumini wa dini hiyo na kuwatakia sikukuu njema waislamu wote nchini. Kutoka kushoto mbele ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, Rais Mstaafu, Ally Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa. Waumini wakiomba dua. Alhadi Mussa akihutubia waumini wa dini ya kiislamu katika Viwanja vya Mnazi Mmoja. Taswira ya  baadhi ya waumini waliojitokeza katika Viwanja vya Mnazi Mmoja inavyoonekana. Sehemu ya waumini akinamama walijitokeza katika swala hiyo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja. WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa mapema leo Jumatano, ameongoza

MREMBO ANASWA LIVE AKIFANYA BIASHARA YA NGONO NJE YA OFISI YA SERIKALI.

Image
Mrembo aliyekuwa akijihusisha na biashara haramu ya ngono nje ya ofisi za serikali akikurupuka mara baada ya kunaswa mtegoni. Njaa mbaya! Kama ulikuwa unadhani ile Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers imenywea, basi umenoa! Safari hii imenasa tukio la mrembo akijihusisha na biashara haramu ya ngono nje ya ofisi za serikali, Ijumaa Wikienda lina kitu laivu. Tukio hilo lisilo la kimaadili lilijiri usiku wa manane wikiendi iliyopita kwenye ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kijitonyama, Dar. Baada ya kupokea kero kwa wakazi wazalendo wa eneo hilo kuwa ofisi yao inanajisiwa, OFM ilifanya uchunguzi wake wa kina na ilipojiridhisha ndipo ikaweka mtego. Kabla ya tukio ilisemekana kuwa pamoja na ngono kufanyika waziwazi na machangudoa waliopo maeneo mbalimbali ya Sinza na Kijitonyama, Dar, siku hizi wadada hao wafikia hatua mbaya zaidi kwa kufanyia maeneo yenye hadhi na sifa maalum kama viwanja vya shule za msingi, nje ya ofisi za watu, karibu na misikiti na makanisani. Timu ya OFM k

Kitwanga Arejea Jimboni Kwake, Akutana na Wanahabari

Image
Mbunge wa Jimbo la Misungwi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Charles Kitwanga. Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Charles Kitwanga leo amekutana na wanahabari nyumbani kwake Misungwi mkoani Mwanza ambapo amesema amerejea jimboni kuwatumikia wananchi. Kitwanga (kulia) wakati akimkabidhi ofisi Mhe. Mwigulu Nchemba. Uteuzi wa Kitwanga ulitenguliwa na  Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli Mei 20 mwaka huu baada ya kuingia bungeni na kujibu swali linalohusu wizara yake akiwa amelewa na nafasi yake kuchukuliwa na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.

Kayumba Amuumbua Mkubwa Fela

Image
Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Afrika Radio, Kayumba amesema pesa bado ipo ingawa imeshapungua, tofauti na alivyosema Mkubwa Fela, na kwamba hata ujenzi wa nyumba bado unaendelea. Kayumba “Hela ipo, ingawa sio tena milioni 50 , itakuwa uwongo nikisema bado ipo milioni 50, lakini zipo siwezi kusema imebakia ngapi, si unaona napendeza nini, nyumba ipo kama nyumba zingine, kawaida siwezi kuzungumzia labda vyumba vingapi, ili mradi nitaweka ubavu wangu nitashukuru Mungu”, alisema Kayumba. Hivi Karibuni kulikuwa na tetesi ambazo zilipigiwa mstari na bosi wa msanii huyo Mkubwa Fela, kwamba pesa alizoshinda msanii huyo zilishaisha kitambo, na nyumba yake ya kuishi ikiwa bado haijakamilika. eatv.tv

Zifahamu Faida/Hasara za kurudiana na Mpenzi wako wa zamani

Image
Kuna faida ya wapenzi kuachana na kurudiana? Vipi kuhusu hasara zake? Hiyo ndiyo mada yetu ya leo kama inavyojieleza. Bila shaka unawajua watu ambao walikuwa wakiishi pamoja kimapenzi, iwe ni ndoa, uchumba au uhusiano wa kawaida ambao wamewahi kutengana na baadaye wakarudiana, iwe ni mara moja au zaidi. Yawezekana hata wewe ukawa miongoni mwa watu wa aina hiyo, kwamba uliwahi kutengana na mtu umpendaye lakini baadaye ukajikuta unarudiana naye na kuanzisha upya uhusiano. Je, kuna faida na madhara gani kwa wapenzi kuachana kisha kuja kurudiana tena na kuanzisha upya uhusiano wa kimapenzi? Ukiwaona watu wanaoishi kwenye aina hii ya uhusiano wa kimapenzi unawachukuliaje? NI JAMBO LA KAWAIDA KATIKA MAPENZI Yawezekana aina hii ya uhusiano wa kuachana na kila mmoja akaendelea na maisha yake kisha baada ya muda mkarudiana tena, likaonekana jambo la ajabu au geni katika mila na desturi za Kiafrika lakini kwa taarifa yako, hili ni jambo la kawaida kabisa katika uhusiano wa kimapenz

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA ZIARA YA RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME

Image
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wakati wa dhifa ya Kitaifa aliyomwandalia Rais wa Rwanda Paul Kagame Ikulu jijini Dar es Salaam.  Rais wa Rwanda Paul Kagame akizungumza na wageni mbalimbali katika dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu mstaafu Salim Ahmed Salim Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Rais wa Rwanda Paul Kagame.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Rais wa Rwanda Paul Kagame.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Ma

Msanii wa Diamond Atuhumiwa Kumbaka Mrembo Jack Wolper....Jack Wolper Afunguka Makubwa

Image
Habari iliyoandikwa kwenye gazeti la Sani la leo jumamosi limemsononesha mrembo Jack Wolper kwa tuhuma za uongo kuwa amebakwa na Msanii wa Diamond... Mwenye Kayaandika haya kwenye ukurasa wake wa Instagram: @wolperstylish - I am so sad kwakweli Hii sio kuniabisha mimi tu, ni kuaibisha na wanawake wenzangu, sijui kwanini magazeti ya kibongo yanatumia Nguvu nyingi kushusha hadhi ya wasanii wa kike haswa.. Nyie SANI no wonder mmepotea katika soko.. Hivi mlivyokua mnachapa mmefkiria kuna wadogo zangu wanasoma?? Au mama angu na baba angu! Naandika kwa uchungu kwakua najua ni limtu limekosa kazi ya kutumia kipaji chake na karama yake vyema linaishia kutumia kwa kuniharibia maisha yangu... Tena front page? Tunafany mangapi mazuri hatuingii page ya kwanza hata siku moja,?! Kesho kutwa nafungua biashara mtaona kama wataandika kitu Ila kwenye ujinga wa kutunga ndo wakwaza Mnaniuzi na nawahakikishia kama Mungu aishivyo mtaona kwa wanenu pia Si mmeamua kuniandika mimi hivi!??

Tamko la RC Makonda kuhusu mashoga waliopo jijini Dar es Salaam

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametangaza vita na makaka poa (mashoga) na madada poa (makahaba) walioko jijini Dar es Salaam kuwa utaendeshwa msako mkali wa kuwaondoa. Mkuu wa Mkoa huyo aliyasema hayo kufuatia hali ya vitendo hivyo visiyokubalika na jamii kuzidi kushamiri na kuwa kuna hatari kubwa ya watoto wadogo kuiga vitendo hivyo vinavyoleta picha mbaya kwani ni kinyume na maadili ya mtanzania. Aidha alisema hawezi kuifumbia macho hali hii kwani inamomonyoa maadali ya jamii na kuwa yuko tayari kulivalia njuga suala hili ili kuhakikisha anawamaliza wote mkoani Sakati hili la ushoga na ukahaba limeibuka siku za hivi karibuni baada ya kituo cha televisheni cha Clouds Tv kumhoji shoga mmoja ambapo jamii ilipinga kitendo hicho na kuona kama walikuwa wakiuhalalisha ushoga na kuaminisha jamii kuwa ni kitu kizuri.

Nilivyofanya Bonge la Sherehe Baada ya Mke Wangu Kufukuzwa Kazi

Image
Huyu mke nilimuoa akiwa hana kitu, kwa bahati alitafutiwa kazi na ndugu yake kwenye kampuni moja ya simu akawa analipwa kama milioni 3 kwa mwezi fasheni na yeye yeye na fasheni vipodozi kila aina,handbag na nywele za laki mbili ndio mshahara wake ukawa unaishia huko mimi mshahara wangu hauzidi laki sita,nilifanyishwa vituko vyote ndani ya nyumba ,manyanyaso yote ,hapiki hafui,hafanyi chochote ndoa ikawa inaelekea kuvunjika. Nikaenda mahakamani kuprocess talaka wakasema mpaka nianzie baraza la usuluhishi la kata au kanisani,nikaamua kwenda kanisa tulilofungia ndoa tukaitwa kwa Baba Paroko for hearing sijui mediation sijui arbitration sijui mie nikatinga kwa bajaj ya kukodi nimepaukaaa yeye akaja na RAV4 . Baba Paroko alivyotusikiliza akaaniita pembeni akasema kijana hapa nadhani hata tukiomba na kukariri mistari yote ya biblia plus mapambio yote ndoa yako haitarudi kama mwanzo pambana utafute hela ,huyu ni mchaga katumwa pesa mjini Nilisali sana nikasugua goti n