Posts

NEC YAKABIDHI POLISI MAJINA YA WATU 52,078 WALIOJIANDIKISHA ZAIDI YA MARA MBILI KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Image
 Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Kailima Ramadhan (kushoto), akimkabidhi Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Benedict Wakulyamba orodha ya majina 52,078 ya watu waliojiandika katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR zaidi ya mara mbili Dar es Salaam leo, kwa ajili ya uchunguzi na baadae hatua za kisheria zichukuliwe kwa wahusika.  Masanduku ya BVR yakiwa yamehifadhiwa Bohari ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.  Mkurugenzi wa Idara ya Daftari la mpiga kura, Dk. Sisti Cariah (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu hatua waliyoifikia kuhusu daftari hilo na shughuli mbalimbali zinazoendelea kufanywa na NEC kuelekea uchaguzi mkuu.  Mtaalami wa Tehama wa NEC, Fatuma Mkanguzi akiwaelezea wanahabari jinsi mfumo wa Tehama unavyofanyakazi.  Fundi, Francis Skale akiwa kazini.  Mafundi wa NEC wakiendelea na kazi.  Mtaalamu wa mfumo wa ulinzi wa NEC, Adolf Kinyelo akitoa maelekezo ya jinsi ya mfumo huo una

LIGI YA MABINGWA ULAYA MANCHESTER UNITED YAUWA

Image
Klabu ya Manchester United August 26 imeshuka dimbani kucheza mechi yake ya marudiano na Club Brugge ya Ubelgiji, mchezo huo ambao Club Brugge imecheza nyumbani lakini imepokea kichapo cha goli 4-0. Magoli ya Man United yamefungwa na nahodha wa timu hiyo Wayne Rooney dakika ya 20, 49 na 57 huku goli la nne lilifungwa na Ander Herrera dakika ya 63. Picha za mechi Nakusogezea video ya magoli mtu wangu

Siri 4 MATUSI ya DIAMOND Kwa DIVA wa CLOUDS FM Hizi Hapa...

Image
  Loveness Malinzi ‘Diva’ NI mtifuano! Agosti 24, mwaka huu ilikuwa siku mbaya kwa nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ au baba Tiffah na mtangazaji anayekimbiza kwa sauti tamu hewani, Loveness Malinzi ‘Diva’ kufuatia kupishana lugha ndani ya studio za redio na hivyo, Diamond kumvurumishia matusi mwenzake. Kupishana kauli huko kuliashiria kuwepo kwa uhasama wa siku nyingi kwa wawili hao huku kila mmoja akiwa anaamini mwenzake ana makosa na ndipo siri tano za Diamond kumtusi Diva zikajulikana. MCHEZO ULIVYOANZA Siku hiyo majira ya saa 9:00 alasiri, Diamond alitia timu kwenye studio za redio hiyo zilizopo Mikocheni, Dar kwa lengo la kumtambulisha msanii wake mpya kutoka studio yake ya Wasafi Records iliyopo Sinza-Mapambano, Dar.Mwanyeji wa Diamond alikuwa mtangazaji Hamis Mandi ‘B12’. Lakini ndani ya studio hiyo alikuwepo Diva. Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ au baba Tiffah. ALIANZA DIAMOND Kabla Diamond hajaanza kumtambulisha msanii wake, alianza

LULU Amhenyesha Vibaya MBOTO Ukumbini!

Image
Haji Salum ‘Mboto akisaidia kulibeba gauni la Lulu. DIVA wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ hivi karibuni amemhenyesha staa mwenzake wa filamu, Haji Salum ‘Mboto’ baada ya kumpa kibarua cha kulishika gauni lake lisiguse chini. Tukio hilo lilitokea kwenye fainali ya shindano la kusaka vipaji vya kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT 2015) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar ambapo Lulu na Mboto walikuwa washehereshaji. Katika hali iliyoonesha Lulu alikuwa ‘siriaz’ stejini alimsisitizia Mboto kila mara ahakikishe amelishika gauni lake vizuri na asiliachie. “Mboto hapa kazi yako ni kulishika gauni langu kwa nyuma kila nitakapokuwa nawe na ole wako uliachie,” alisikika Lulu ambapo Mboto alitekeleza ombi la Lulu.

WEMA SEPETU Amtafuta Shetani Tena!

Image
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu. Anadaiwa kutafuta shetani mwingine wa ugomvi baada ya ‘kumalizana’ na Aunt Ezekiel Grayson na kuanzisha ushosti na mwigizaji, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’, jambo ambalo linawapa wasiwasi mashabiki wao kutokana na dhana iliyojengeka kuwa mrembo huyo (Wema), hawezi kudumu na rafiki kwa kipindi kirefu. URAFIKI WAANZIA KWENYE KAMPENI ZA CCM Mastaa hao walianza kuwa na ukaribu mkubwa kwenye mambo ya Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizozinduliwa Jumapili iliyopita katika Viwanja vya Jangwani, Dar. Habari zilieleza kwamba, kabla ya hapo, wawili hao hawakuwahi kuwa na urafiki hata zaidi ya salamu. WEMA AMPOZA BATULI Chanzo ambacho ni mtu wa karibu na wawili hao kilieleza kwamba, baada ya Batuli kupata mkasa wa kuunguliwa nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya …Mbezi Beach, Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita, mastaa hao walikuwa wote saluni na walipopata taarifa ya mkasa huo, Wema ndiye aliyempooza machungu Batuli kwa kumsaidia katika kipindi

Mbowe Akata Rufaa Mahakama kuu Dhidi ya Hukumu yake

Image
Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe amekata rufaa Mahakama Kuu kupinga hukumu iliyotolewa dhidi yake Julai, mwaka huu, na kumtoza faini ya Sh1 milioni baada ya kupatikana na hatia katika kosa la jinai. Mbowe alitozwa faini ya Sh1 milioni au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kumshambulia mwangalizi wa ndani wa Uchaguzi Mkuu wa 2010 katika Wilaya ya Hai, Nassir Yamin. Hata hivyo, Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na Mbunge wa Hai, alilipa faini hiyo na kuachiwa huru na Mahakama ya Wilaya ya Hai. Katika rufaa hiyo namba 33/2015, iliyofunguliwa na wakili Peter Kibatala, Mbowe anailalamikia mahakama iliyomtia hatiani kuwa ilishindwa kushughulikia hoja muhimu katika kufikia uamuzi huo. Pia, Mbowe analalamika kuwa mahakama ilishindwa kupima ushahidi kwa usahihi na pia, ilishindwa kutilia maanani ushahidi wa mashahidi wa upande wa utetezi akiwamo yeye. Mbowe analalamika kuwa mahakama ilishindwa kutumia msi

Sheddy Clever: Nimelipwa pesa nyingi sana kutayarisha wimbo wa Diamond na Ne-Yo

Image
Producer Sheddy Clever wa Burn Records amesema kuwa amepata pesa nyingi alizolipwa na Diamond kutengeneza collabo yake na Ne-Yo, kiasi ambacho ingemchukua miezi mitatu kuipata kwa kazi zake za kawaida za production. Sheddy ambaye ndiye producer anayepika collabo ya Diamond na Ne-Yo inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa muziki wa Afrika, ameiambia phars kuwa hajawahi kulipwa kiasi hicho cha pesa toka ameanza kufanya production. “Hii kazi tuliyoenda kufanya juzi nimelipwa, na nimelipwa vizuri tu...sijawahi kulipwa hivyo kwakweli yaani nafurahi sana,” alisema kwa furaha. “Diamond ni msanii tofauti sana na haogopi kuwekeza katika kazi zake kwasababu anajua nini anachokifanya...Nimelipwa vizuri japokuwa kazi bado sijamaliza lakini nimelipwa pesa nyingi tu nzuri nimefikia hoteli nzuri.” alisema Sheddy. Sasabu wengi huwa hawapendi kusema kiwango wanacholipwa, nilipomuuliza kama amelipwa zaidi ya shilingi milioni 1 alijibu; Sheddy:[kicheko] Inazidi milioni 1 hata mi

LIGI YA MABINGWA ULAYA MANCHESTER UNITED YAUWA

Image
Klabu ya Manchester United August 26 imeshuka dimbani kucheza mechi yake ya marudiano na Club Brugge ya Ubelgiji, mchezo huo ambao Club Brugge imecheza nyumbani lakini imepokea kichapo cha goli 4-0. Magoli ya Man United yamefungwa na nahodha wa timu hiyo Wayne Rooney dakika ya 20, 49 na 57 huku goli la nne lilifungwa na Ander Herrera dakika ya 63. Picha za mechi Nakusogezea video ya magoli mtu wangu

MOTO WATEKETEZA MAROLI MAWILI YA MAFUTA MWANZA

Image
Malori mawili ya mafuta yameteketea kwa moto uliosababishwa na hitilafu ya Jenereta iliyokuwa inatumika kushusha mafuta kutoka ndani ya malori hayo kwa ajili ya kuyahifadhi kwenye kisima cha mafuta cha sasa kazi kilichopo eneo la Butimba kona jijini Mwanza na kusababisha hasara ya mamilioni ya shilingi,sambamba na kuteketea kwa pikipiki moja mali ya Ayoub Ismail. Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea majira ya saa 4.30 asubuhi wanasema malori hayo aina ya SCANIA – moja lenye namba za usajili T 509 AFD na Tela lake namba T 592 ACL lililokuwa limebeba lita 35 za mafuta ya Dizeli pamoja na lori jingine lenye namba za usajili T 674 AHH ambalo lilikuwa limeegeshwa kando kidogo ya kituo hicho cha mafuta cha sasa ni kazi yameteketea na kusababisha wingu kubwa la moshi mweusi,huku juhudi za wananchi kuzima moto huo uliokuwa ukiwaka kwa kasi ya ajabu zikigonga mwamba. Muda mfupi magari ya jeshi la zimamoto na uokoaji jijini Mwanza yakawasili katika eneo la tuki

MASHA AACHIWA KWA DHAMANA

Image
Lawrence Masha akiwa na wanachama wa Ukawa baada ya kuachiwa. Baada ya jana kulala mahabusu ya segerea, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha leo ameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana. Masha, ambaye anashitakiwa kwa kosa la kuwazuia Polisi wasifanye kazi ikiwa ni pamoja na kuwatolea lugha ya matusi. Jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo alisomewa mashtaka ambayo aliyakana lakini ikalazimu apelekwe mahabusu ya Segerea baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

BREAKING NEWS UKAWA WAZUIWA KUZINDUA KAMPENI JANGWANI

Image
Cloudsfm Radio ‪#‎News‬ UKAWA Wazuiwa kuzindua kampeni Jangwani Jiji la Dar es Salaam wamemzuia Mgombea waUKAWA, Edward Lowassa kuzindua kampeni yake kwenye viwanja vya Jangwani Jumamosi ya 29 Agosti , 2015 .Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA , James Mbatia amesema jiji umewagomea kufanya uzinduzihuo Jangwani kwa madai kuwa tayari kuna mtu mwingine ambaye ameshalipia uwanja huo.Mbatia anasema pamoja na kufanya juhudi zakuomba kutajiwa aliyelipia uwanja huo iliwazungumze naye , Jiji walikataa.Mbatia anasema viongozi wengine wa UKAWA wanashughulikia suala hilo ikiwa pamoja nakumtaka Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Damian Lubuva kuingilia kati.

BREAKING NEWS : FEDHA ZA KAMPENI YA LOWASSA ,UKAWA NA CHADEMA MAKUBWA YAIBUKA

Image
Kwa mujibu wa habari nyeti nilizotonywa sasa hivi kuna kizazaa cha fedha za kampeni zinazowafanya Lowassa, Chadema na UKAWA kwa ujumla kuwa katika mtafuruku mkubwa na mpaka sasa uliopelekea kuchelewa kuanza uzinduzi wa kampeni ya Urais wa ukawa. Vyama vinayounda UKAWA vinasema Lowassa aliahidi kuwa atatowa fedha zote za kampeni kwa hiyo wao wasiulizwe. Lowassa anasema alizotowa zinatosha (hasemi katowa kampa nani na za nini), Chadema nao wanavunga kuwa mpaka sasa akaunti ya kutowa kiasi kikubwa cha fedha ni lazima saini ya Katibu Mkuu iwepo na Katibu Mkuu wa chadema alipofatwa kusaini yeye kagoma ( huu ni ungo wa chadomo) wanasema eti Katibu Mkuu wao anataka kwanza taratibu za kubadili saini yake zikamilike kama watatowa fedha watowe wenyewe akikamilisha zoezi la kubadili kuwa ndiyo anawakwamisha. Kizungumkuti kinaendelea wakati marafiki matajiri waliokuwa wanampa fedha azitakazo Lowassa wameona mambo yanakuwa magumu na badala ya fedha wameanza kumpa ahadi za ke

RAIS KIKWETE ASHIRIKI MAZISHI YA MTOTO WA JAJI MKUU MJINI TANGA

Image
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Jaji Mkuu Mhe.Mohamed Chande Othman kufuatia kifo cha mwanaye Said Mohamed Chande wakati Rais alipokwenda Chumbageni Tanga kuhudhuria mazishi ya marehemu. Jaji Mkuu Mhe.Mohamed Chande Othman akiweka udongo katika kaburi la mwanaye Said Mohamed Chande wakati wa mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Chumbageni Tanga leo jioni. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Said Mohamed Chande wakati ya mazishi yaliyofanyika katika eneo la Chumbageni Tanga leo.Marehemu Said ni Mtoto wa Jaji Mkuu Mhe.Mohamed Chande Othman. Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal akiweka udongo katika kaburi la mrehemu Said Mohamed Chande wakati wa mazishi yaliyofanyika huko Chumbageni Tanga. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal,Jaji Mkuu Mhe.Mohamed Chande Othman wakiomba dua wakati wa mazishi ya marehemu Said Mohamed Chande ambaye ni mtoto wa jaji mkuu yaliyofa

LOWASSA AFUNGUKA KUHUSU MAISHA YAKE KISISASA

Image
Edward Ngoyai Lowassa 1 hr   ·   Facebook Mentions   ·   Leo ninasherehekea siku yangu ya kuzaliwa na kwa namna ya pekee ninamshukuru Mungu kwa kuendelea kunibariki, kunishika mkono na kuniongoza. Maisha yangu ni mfano wa baraka za Mungu. Kuna nyakati nilianguka lakini  kwa upendo wake akaninyanyua na mpaka sasa ameendelea kunionyesha baraka zake. Kwa namna ya pekee ninapenda kuishukuru familia yangu na watanzania wenzangu kiujumla kwa upendo na imani yao juu yangu hata pale nilipopitia vipindi vigumu katika maisha yangu. Nina furaha zaidi leo kwa kuwa ninasherehekea siku yangu ya kuzaliwa nikiwa katika kilele cha mapambano ya kusaidia wananchi wenzangu

Rais Kikwete afungua Mkutano wa Chama Cha Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashariki

Image
Rais Kikwete akifungua Mkutano wa siku tatu wa Chama Cha Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashariki unaofanyika katika Hoteli ya Malaika Beach Resort Mwanza. .Baadhi ya washiriki wa Mkuano huo. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano wa Chama Cha Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashariki (picha na Freddy Maro)

CHADEMA WAMJIBU KAMANDA KOVA

Image
Baada ya Kamishna wa Polisi kanda maalum ya Dsm kupiga marufuku Wagombea wa vyama vya siasa kufanya vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa wananchi katika maeneo mbalimbali ya jiji kama alivyofanya mgombea wa uraisi wa Chadema kwa kutembelea Gongo la mboto na kupanda daladala jambo ambalo limeleta taharuki pamoja na kusababisha shughuli za watu kusimama. Afisa habari wa Chadema, Tumaini Makene amesema Jeshi la polisi haliwezi kuwapangia nini cha kufanya. Wataendelea kufanya mikakati yao watakayoipanga ili mradi hawavunji sheria za nchi na sheria za uchaguzi

LOWASSA AZIDI KUWATEMBELEA WANANCHI DAR, NI MTAA KWA MTAA, NYUMBA KWA NYUMBA

Image
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Wazee wa Tandale, wakati alipotembelea Soko la Tandale, jijini Dar es salaam leo, akiambatana na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni (kushoto). PICHA ZOTE NA MTAA KWA MTAA BLOG Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakipata maelezo kutoka kwa Bw.Omari Juma (kulia) ambaye ni mfanyabiashara ya kuuza Maharage katika Soko la Tandale, Manzese Jijini Dar es salaam leo Agosti 25, 2015, wakati walipotembelea Soko hilo kujionea hali ya biashara masokoni. Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakiwapungia wananchi wa Tandale, Manzese Jijini Dar es salaam leo Agosti 25, 2015. Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demo