LULU Amhenyesha Vibaya MBOTO Ukumbini!



Haji Salum ‘Mboto akisaidia kulibeba gauni la Lulu. DIVA wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ hivi karibuni amemhenyesha staa mwenzake wa filamu, Haji Salum ‘Mboto’ baada ya kumpa kibarua cha kulishika gauni lake lisiguse chini.
Tukio hilo lilitokea kwenye fainali ya shindano la kusaka vipaji vya kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT 2015) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar ambapo Lulu na Mboto walikuwa washehereshaji.
Katika hali iliyoonesha Lulu alikuwa ‘siriaz’ stejini alimsisitizia Mboto kila mara ahakikishe amelishika gauni lake vizuri na asiliachie.
“Mboto hapa kazi yako ni kulishika gauni langu kwa nyuma kila nitakapokuwa nawe na ole wako uliachie,” alisikika Lulu ambapo Mboto alitekeleza ombi la Lulu.

Comments

Popular posts from this blog