Posts

SUPER STAR DIMONDO na DAVIDO ..NDANI YA CLUB ZA LAGOS AKIPONDA RAHA

Image

RAIS DK.SHEIN AZUNGUMZA NA BALOZI WA THAILAND

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Thailand Nchini Tanzania Ittiporn Boonpracong,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya kusalimiana.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Thailand Nchini Tanzania Ittiporn Boonpracong,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Balozi wa Thailand Nchini Tanzania Ittiporn Boonpracong,baada ya mazungumzo yao,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

MASTAA WAENDELEA KUSHIKANA UCHAWI

Image
Uchunguzi wa gazeti hili ndani ya ulimwengu wa mastaa hao ulibaini kwamba, ukiwaacha wale wa Bongo Fleva ambao wamekuwa wakishikana uchawi kila kukicha, kwenye filamu ndiko hakufai. Ilibumburuka kwamba masuala ya kurogana ndiyo yamesababisha filamu za baadhi yao kudoda na kukosa soko. Inaelezwa kwamba mbali na sinema  zao kubuma sokoni pia wamekuwa wakizibiana riziki za tenda kama ilivyokuwa zamani. Elizabeth Michael 'Lulu'. KIVIPI? Kwa mujibu wa ‘mtaalam’ wao mwenye kituo cha kazi huko Yombo-Buza, Dar, wanachokifanya ni kufifisha na kuzimana nyota hivyo kumpotezea mhusika mvuto kwenye jamii. “Unajua kuna mastaa ambao walikuwa na majina makubwa sana lakini siku hizi siyo kama zamani. “Baadhi wanawaroga wenzao kwa kuwasababishia matatizo ya magonjwa au kwenye familia,” alisema mmoja wa wasanii waliokuwa waking’ara zamani lakini siku hizi kafifia huku akimtolea mfano mwigizaji mmoja wa kiume ambaye mkewe aliwahi kumkuta na hirizi. Katika uchunguzi huo, baa

AUNT, WOLPER, SNURA WAFUNGA MTAA

Image
                                                     Stori: Hamida Hassan Mastaa wa filamu za Kibongo wenye jina kubwa mjini, Aunt Ezekiel, Jacgueline Wolper na Snura Mushi hivi karibuni walitisha kwa kufunga mtaa kutokana na mauno waliyokuwa wakikata mbele za wapiga ngoma wa Kundi la Baikoko, tukio lililojiri Mwananyamala, Dar nyumbani kwa msanii mwenzao Vanitha Omary. Snura Mushi. Wasanii hao waliwashangaza watu jinsi walivyokuwa wakijituma kukata mauno huku Wolper akimtunza mpiga ngoma na kumkatikia kwa staili mbalimbali zikiwemo za chumbani.… Stori: Hamida Hassan Mastaa wa filamu za Kibongo wenye jina kubwa mjini, Aunt Ezekiel, Jacgueline Wolper na Snura Mushi hivi karibuni walitisha kwa kufunga mtaa kutokana na mauno waliyokuwa wakikata mbele za wapiga ngoma wa Kundi l

MWILI WA DKT. SENGONDO MVUNGI KUWASILI LEO

Image
Tume ya Mabadiliko ya Katiba inawafahamisha wananchi kuwa taratibu za kuusafirisha mwili wa Mjumbe wake, Dkt. Sengondo Mvungi aliyefariki nchini Afrika Kusini zimekamilika na mwili wake unatarajia kuwasili nchini siku ya Leo. Baada ya kuwasili, mwili huo utahifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo iliyopo jijini Dar es Salaam. Aidha, siku ya Kesho, Novemba 16, 2013 kutafanyika Ibada ya mazishi katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi. Baada ya misa, marehemu ataagwa katika Viwanja vya Karimjee kuanzia saa 6:30 mchana siku hiyohiyo ya Jumamosi, Novemba 16, 2013. Aidha, Marehemu Dkt. Mvungi anatarajiwa kusafirishwa siku ya Jumapili, Novemba 17, 2013 kwenda Kisangara Juu, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu, Novemba 18, 2013. Dkt. Mvungi alifariki jana (Jumanne, Novemba 12,

WOLPER AANIKA A - Z YA KULICHOMNASISHA KWA DALLAS

Image
STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa suala la yeye kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Abdallah Mtoro ‘Dallas’ halikusababishwa na ukata kwani yeye hakufuata fedha kwa mwanaume huyo. Jacqueline Wolper. Akijibu swali la paparazi wetu lililomtaka afunguke kama alifuata mkwanja kwa Dallas, Wolper alisema moyo wake huwa hauna tamaa ya fedha na aliingia katika penzi la Dallas kwa mapenzi aliyokuwa nayo wakati huo na kwa kuwa yaliisha, maisha yanaendelea. Abdallah Mtoro ‘Dallas’. “Sikufuata pesa kwa Dallas, pesa ni pesa na mapenzi ni mapenzi. Kama ni pesa nilikuwa nazo na hata kabla sijawa naye na sasa pia ninazo, waniache,” alisema Wolper.

WOLPER AANIKA A - Z YA KULICHOMNASISHA KWA DALLAS

Image
STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa suala la yeye kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Abdallah Mtoro ‘Dallas’ halikusababishwa na ukata kwani yeye hakufuata fedha kwa mwanaume huyo. Jacqueline Wolper. Akijibu swali la paparazi wetu lililomtaka afunguke kama alifuata mkwanja kwa Dallas, Wolper alisema moyo wake huwa hauna tamaa ya fedha na aliingia katika penzi la Dallas kwa mapenzi aliyokuwa nayo wakati huo na kwa kuwa yaliisha, maisha yanaendelea. Abdallah Mtoro ‘Dallas’. “Sikufuata pesa kwa Dallas, pesa ni pesa na mapenzi ni mapenzi. Kama ni pesa nilikuwa nazo na hata kabla sijawa naye na sasa pia ninazo, waniache,” alisema Wolper.

RAIS DKT KIKWETE NCHINI SRI LANKA LEO

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa alipomtembelea kwa mazungumzo kwenye jengo la Temple Trees jijijini Colombo leo Novemba 14, 2013 kabla ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya ya madola mwaka huu (CHOGM 2013)  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini  kitabu  cha  wageni nchini  sri Lanka   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa pamoja na  viongozi  mbali  mbali  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa katika mazungumzo yao  leo (picha  zote na Ikulu) Im

UCHEKI MJENGO MPYAAA WA DIAMOND ANAOUPOROMOSHA .. NI KUFURU TUPU

Image
Diamond hivi sasa yupo nchini Nigeria kwa ajili ya video zake mbili akiwa na Iyanya na Davido lakini bado yupo karibu na mashabiki wake kupitia mitandao ya kijamii. Kutana na post hii kutoka kwa Diamond kwenye ukurasa wake wa facebook inayohusisha nyumba yake.

HIVI NDIVYO MSANII WA TAARAB FUNDIKIRA ALIVYOAGWA ... WENGI WAZIMIA MSIBANI

Image
                Mume wa marehemu, Kaisi Musa Kaisi akiwa na uso wa majonzi. Marehemu Nyawana Fundikira enzi za uhai wake. Baba… Mume wa marehemu, Kaisi Musa Kaisi akiwa na uso wa majonzi. Marehemu Nyawana Fundikira enzi za uhai wake. Baba wa marehemu (kulia) akifuta machozi, kushoto ni mtangazaji wa ITV, Hawa akilia kwa uchungu. Waombolezaji waliohudhuria kwenye msiba huo. Ndugu wa marehemu akilia kwa uchungu baada ya mwili kuondolewa na kupelekwa msikitini kuswaliwa. Mwili wa marehemu ukishushwa kwenye gari baada ya kutolewa katika hospitali ya Mwananyamala ulikokuwa umehifadhiwa. Waombolezaji wakililia kwa uchungu. Mwili wa marehemu ukipelekwa msikitini. LEO vilio vimetawala nyumbani kwa mzee Fundikira maeneo ya kwa Bibinyau, Magomeni, Dar wakati waombolezaji wakiaga mwili wa aliyekuwa mwimbaji na mtangazaji wa kipindi cha taarab ‘Ambaa na Mwambao’ kinachorushwa na Passion Fm, Nyawana Fundikira. Nyawana alifariki jana  baada

WAPIGA DEBE WAGOMBEA ...

Image
Na Dustan Shekidele, Morogoro NI jambo la kusikitisha kweli. Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Komba Faustine Aloyce ambaye ni mpiga debe, amefariki dunia baada ya kugongwa na gari wakati akipigana na mwenzake katikati ya barabara wakigombea shilingi elfu moja waliyopewa kama ujira katika kituo cha daladala kilichopo Kasanga nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro. Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Jumamosi iliyopita kwenye kituo hicho cha daladala zitokazo Mzumbe, Mlali, Mgeta Melela, Doman na Morogoro mjini kilichopo kando kando ya Barabara Kuu ya Morogoro-lringa. Mashuhuda wa tukio hilo walililiambia gazeti hili kwamba Komba na mwenzake huyo aliyefahamika kwa jina moja la Alunaki, waligombea fedha hiyo waliyopewa baada ya kufanya kupiga debe ambapo kila mmoja alidai ilikuwa yake. Wakati wakiendelea kupigana, gari moja lilitokea kwa kasi, Alunaki aliwahi kukimbia lakini bahati mbaya Komba akakanyagwa na kufariki papo hapo. Kabla ya kupigana, inadaiwa wawili hao

WANANCHI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA ELIMU

Image
Na Aron Msigwa – MAELEZO,  Dar es salaam. Serikali imewataka wananchi kuzitumia ipasavyo fursa za elimu zinazotolewa kupitia programu mbalimbali za ikiwemo Elimu ya Watu Wazima (EWW) na ile ya Elimu Nje ya Mfumo Rasmi (ENMRA) ili kupunguza tatizo la umasikini, maradhi na ujinga. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Bw. Said Meck Sadiki wakati akitoa taarifa kwa wananchi wa mkoa wa Dar es salaam kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi yatakayofanyika jijini Dar es salaam kuanzia Novemba 13, 2013 yakiongozwa na kauli mbiu “Kisomo kwa ajili ya Karne ya 21” Amesema  serikali imeanzisha programu mbalimbali za elimu kuanzia msingi mpaka sekondari kwa lengo la kuwawezesha wananchi kupata fursa hiyo na kuondokana na tatizo Umaskini, maradhi na ujinga na kuwawezesha kujikwamua  kiuchumi, Kijamii, Kisiasa na Kiutamaduni. Ameeleza kuwa mkoa wa Dar es salaam kwa sasa unaratibu program m

CHAZ BABA APATA AJALI MBAYA

Image
Na Shakoor Jongo SAD news kutoka Bongo Dansi ni ajali ya pikipiki aliyopata Kiongozi wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ na kumsababishia majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake. C haz Baba akiuguza majeraha aliyoyapata. Risasi Vibes lilifunga safari hadi nyumbani kwake Mwananyamala, Dar kumjulia hali ambapo alisema tukio hilo lilitokea katikati ya wiki iliyopita, Ubungo baada ya kugongwa na gari kwa nyuma. “Nilikuwa natokea Kimara, nikiendesha pikipiki yangu. Si unajua tena ile barabara ipo kwenye matengenezo kwa hiyo vizuizi ni vingi njiani. Ghafla nilishangaa pikipiki ikigongwa kwa nyuma, nikaanguka. “Namshukuru Mungu maana mazingira niliyopata ajali ni mabaya sana isitoshe unajua pindi upatapo ajali kuna wengine wanakuja kukusaidia na wengine ni wezi lakini sikuibiwa kitu. “Nimeumia mkono, kiuno, mguu mmoja wa kushoto na maumivu kwa ndani lakini hakuna sehemu niliyovunjika,” alisema Chaz Baba.

HAYA MAJANGAAZZZ ... MAINDA AANIKA ALIVYOICHOMOA MIMBA YA RAY

Image
HILI ndiyo Risasi bwana! Sikia, kama ulikuwa hujui ni kwamba msanii mkongwe katika filamu za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ ameibuka na kueleza mengi ikiwemo kutoa mimba ya mpenzi wake wa siku nyingi, Vincent Kigosi, tulia hapohapo.   Ruth Suka ‘Mainda’. Mbali na uhusiano wao huo uliokuwa ukifanywa siri, Mainda ameeleza… Stori:  Jelard Lucas HILI ndiyo Risasi bwana! Sikia, kama ulikuwa hujui ni kwamba msanii mkongwe katika filamu za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ ameibuka na kueleza mengi ikiwemo kutoa mimba ya mpenzi wake wa siku nyingi, Vincent Kigosi, tulia hapohapo.   Ruth Suka ‘Mainda’. Mbali na uhusiano wao huo uliokuwa ukifanywa siri, Mainda ameeleza kwa machungu jinsi Ray alivyomtesa kwa kumchanganya na wasanii wenzake, Blandina Chagula ‘Johari’ na Chuchu Hans ambaye ni mke wa mtu. Risasi Mchanganyiko lilipata wasaa wa kufanya naye mahojiano ‘exculusive’ kwa saa moja na dakika tano, wikiendi iliyopita, makao