WOLPER AANIKA A - Z YA KULICHOMNASISHA KWA DALLAS

STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa suala la yeye kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Abdallah Mtoro ‘Dallas’ halikusababishwa na ukata kwani yeye hakufuata fedha kwa mwanaume huyo.

Jacqueline Wolper.
Akijibu swali la paparazi wetu lililomtaka afunguke kama alifuata mkwanja kwa Dallas, Wolper alisema moyo wake huwa hauna tamaa ya fedha na aliingia katika penzi la Dallas kwa mapenzi aliyokuwa nayo wakati huo na kwa kuwa yaliisha, maisha yanaendelea.

Abdallah Mtoro ‘Dallas’.
“Sikufuata pesa kwa Dallas, pesa ni pesa na mapenzi ni mapenzi. Kama ni pesa nilikuwa nazo na hata kabla sijawa naye na sasa pia ninazo, waniache,” alisema Wolper.

Comments

Popular posts from this blog