Posts

EDWARD LOWASSA AMBANA BERNAD MEMBE KWENYE KIKAO CHA KAMATI YA BUNGE

Image
 Mhe. Edward Lowassa (Mb.)Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa  na Mbunge wa Monduli akizungumza wakati wa kikao na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika kupitia Taarifa ya Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi ya Wizara. Kikao hicho kilifanyika katika  Ofisi Ndogo za Bunge tarehe 19 Agosti, 2013.   Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akiwasilisha  Taarifa ya Wizara ya Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge (hawapo pichani).   Baadhi ya Waheshimiwa wa Wabunge ambao pia  ni Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani).  Kikao kikiendelea. Baadhi ya Wakurugenzi na Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifuatilia kwa karibu taarifa iliyokuwa ikiwasilishwa na Mhe

IVANOVIC AEPUKA RUNGU LA FA BAADA YA KUMCHEZEA RAFU BENTEKE

Image
BEKI wa Chelsea, Branislav Ivanovic hatakutana na adhabu zaidi kwa rafu aliyomchezea Christian Benteke jana usiku katika mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Astin Villa. (HM) Kocha wa Aston Villa, Paul Lambert 'alimuwakia' refa Kevin Friend kwa kutomtoa beki huyo baada ya rafu hiyo mbaya, kiasi cha sekunde tu kabla hajaifungia wenyeji bao la ushindi Uwanja wa Stamford Bridge. Lakini kwa sababu, Friend alimuonyesha kadi ya njano beki huyo Mserbia baada ya kuona tukio alilomfanyia Benteke, Chama cha Soka (FA ) hakitachukua hatua zaidi. Lambert, ambaye baada ya mechi alilalamika timu yake kuonewa katika mechi hiyo, alisema: "Nafikiri Ivanovic alicheza rafu. Nafahamu ni mchezo wa maguvu. Lakini hicho ndicho nachofikiria,". Mourinho, pamoja na hayo, alipuuza madai hayo akisema: "Hii soka soka ya England. Kwa sababu fulani, dunia inaipenda hii kuliko ligi yoyote,". Sheria za FA zimebadilika majira ya

as cannes yamwagia sifa kapombe

Image
Shomari Kapombe akitambulishwa rasmi AS Cannes RASMI, klabu ya Daraja la Nne Ufaransa, AS Cannes imetangaza katika tovuti yake kwamba katika kujiimarisha ili kutoka katika kipindi kigumu, imeboresha kikosi chake kwa kumsajili kiungo Mtanzania, Shomari Salum Kapombe. (HM) Klabu hiyo imesema hiyo pia itakuwa fursa kwa mchezaji huyo kutoka Simba SC ya Tanzania kujipatia uzoefu wa kimataifa akiwa na Weupe hao Ufaransa. Imemuelezea Kapombe, kama kinda mwenye umri wa miaka 21, ambaye hadi sasa amekwishachezea mechi 14 timu yake ya taifa, Taifa Stars pamoja na kumkabidhi jezi kuanza rasmi mazoezi na wenzake. Na imevutiwa naye zaidi baada ya wasifu wake kusema anaweza kucheza nafasi nyingine pia, zikiwemo za ulinzi, hivyo atakuwa msaada mkubwa kwa kocha Jean-Marc Pilorget msimu huu. Imesema viongozi wanafanya jitihada kubwa kuhakikisha wanainua kiwa

NITATUMA OFA NYINGINE KWA UNITED KUMSAJILI ROONEY"MOURINHO"

Image
Jose Mourinho amethibitisha kwamba Chelsea kwa sasa watasitisha mbio zao za kumuwania mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney mpaka klabu hiyo itakapocheza na United kwenye dimba la Old Trafford siku ya jumatatu. (HM) The Blues wameshuhudia ofa zao mbili zikikataliwa na mabingwa wa premier league, huku kocha David Moyes akisisitiza kwamba mshambuliaji huyo wa England hauzwi. Jana jumatano zilitoka taarifa kwamba United wapo tayari kuzungumza na Chelsea katika dili la uhamisho wa Rooney lakini ikiwa tu litamhusisha Juan Mata - lakini Mourinho amesema hakuna mazungumzo yatakayofanyika mpaka baada ya mechi ya jumatatu. "Tulituma ofa kwa ajili [Rooney] huko nyuma na tutfanya hivyo tena baadae," kocha huyo wa kireno aliwaambia waandishi wa habari baada ya ushindi wa 2-1 dhidi Aston Villa. "Lakini sitaki Chelsea ifanye kitu chochote kabla ya mechi ya Jumatatu tutakapoenda Old Trafford."  Chanzo: Shaffihdaud

WATU MILIONI 2.9 KUCHUKULIWA ALAMA ZA VIDOLE, PICHA.

Image
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeanza zoezi la uchukuaji alama za vidole, picha na saini za kielekroniki kwa waombaji wa Vitambulisho vya Taifa katika mkoa wa Dar es Salaam ambapo watu wapatao milioni 2,900,000 wanatarajiwa kupatiwa huduma hiyo. Zoezi hili lilianza Julai 15 katika wilaya ya Temeke ambayo imegawanywa katika kanda tano, itafuatiwa na Wilaya ya Ilala na kuhitimishwa na Kinondoni. Kila Wilaya imegawanywa katika kanda, ili kuhakikisha wananchi wanahudumiwa vizuri na kurahisisha zoezi kwa kuwapunguzia wananchi usumbufu wa kukaa muda mrefu kusubiri katika foleni. Zoezi la uchukuaji alama za vidole linakwenda sambamba na ujazaji fomu kwa waombaji wapya ambao hawakupa fursa ya kujaza fomu wakati wa zoezi la ujazaji fomu za maombi ya vitambulisho vya Taifa. Waombaji wanatakiwa kufika kwenye vituo vya usajili na nyaraka halisi za kuthibitisha uraia na umri mathalan, cheti cha kuzaliwa, pasipoti, v

WENGER AMGEUKIA FLAMINI, AMREJESHA EMIRATES

Image
Mathieu Flamini KOCHA Arsene Wenger yuko katika siku 12 ngumu za kukimbizana kukamilisha usajili kabla ya dirisha kufungwa na sasa amehamishia ndoana zake kwa Mathieu Flamini, kiasi cha miaka mitano tangu aondoke Arsenal kuhamia AC Milan. (HM) Klabu hiyo ya Italia imemtema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 mwishoni mwa msimu na sasa kiungo huyo kiasi cha wiki mbili amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha Wenger. Kocha wa Arsenal amevutiwa kiasi cha kutosha na hali ya mchezaji huyo na yuko tayari kumpa ya Mkataba Flamini baada ya kukubali kurejea nyumbani licha ya kutakiwa na klabu nyingine. Atakuwa mchezaji wa pili kusainiwa na Wenger majira haya ya joto— wote wachezaji huru — na mchezaji wa nne wa zamani wa timu hiyo kusainiwa tena na kocha huyo, baada ya awali kuwarejesha Sol Campbell, Jens Lehmann na Thierry Henry Emirates.

HUYU NDO MKENYA ANAYEDAIWA KUWA DEMU WA DIAMOND PLATINUMZ ATUPIA PICHA ZA UTATA.

Image
 Angel Maggie ni Mkenya ambaye wiki hii amepamba mitandao kadhaa ya nchini kenya akisemekana kuwa mpenzi wa mwanamuziki Diamond Platinumz ingawa Diamond mwenyewe bado hajaweka wazi kama ni kweli au lah! licha ya kwamba wanajuana muda sasa. Hata katika shows alizofanya Diamond hivi karibuni Nairobi na Mombasa alikuwa na Angel muda mwingi. Angalia picha zake mpya.......................

SHILOLE AAMBULIA MATUSI BAADA YA KUANIKA TUMBO LAKE MBELE ZA WATU......!!

Image
  Msanii wa filamu za Kibongo,na mwanamuziki wa Bongo Fleva Zuwena Mohamed‘Shilole’amenangwa kwenye mtandao wa instagram baada ya kupost picha akiwa na madansa wake huku wakiacha matumbo yao wazi.

BUNGE KUANZA VIKAO VYAKE JUMANNE DODOMA

Image
Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa tanzania linataraji kuanza vikao vyake kwa wiki mbili mjini Dodoma.Wabunge wamehitimisha vikao vya kamati za bunge leo ikiwa ni utekezaji wa shuguli mbalimbali za Bunge ikishiria kuanza kwa vikao vyake jumanne ijayo mjini Dodoma, Ambapo miswada mbalimbali itawasilishwa katika vikao hivyo  

WASTARA HATAOLEWA BONGO TENA

Image
Na Imelda Mtema KAKA wa staa wa Filamu za Kibongo, Wastara Juma aitwaye Juma Juma ameliambia Risasi Mchanganyiko kwamba dada yake hatafunga  tena ndoa nyingine hapa nchini. “Iwapo dada yangu akitaka kuolewa atafanya hivyo Uarabuni siyo hapa kabisa,” alisema kaka huyo na kudai kuwa ameshuhudia mateso mengi ya dada yake kwa wanaume wa Kitanzania. Kaka huyo amesisitiza kwamba wanaume wasipate tabu ya kumuuliza dada yake kuhusu suala la ndoa kwani watajisumbua bure. Juma alizungumza kwa niaba ya dada yake ambaye awali alipigiwa simu ili kuulizwa kama alikuwa na mpango wa kufunga ndoa nyingine hapa nchini. Hata hivyo, Wastara alimwachia kaka yake huyo kujibu badala yake, ingawaje kaka huyo hakufafanua kama dada yake ameshapata mtu wa kufunga naye ndoa huko Uarabuni. Wastara alifunga ndoa tatu na wanaume tofauti na mume wake wa mwisho alikuwa msanii wa filamu, Juma Juma Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki dunia mapema mwaka huu.

MKENYA AKIRI KUUA MTU NA KULA MOYO NA UBONGO MAREKANI

Image
Alexander Kinyua (kushoto) na mwanamume aliyekuwa akiishi naye nyumba moja Kujoe Bonsafo Agyei-Kodie. Picha/MAKTABA Mwanafunzi kutoka Kenya aliyekuwa akiishi Marekani amekiri kwamba alimuua mwanamume waliyekuwa wakiishi nyumba moja na kula moyo wake na ubongo wake. MWANAFUNZI kutoka Kenya aliyekuwa akiishi Marekani amekiri kwamba alimuua mwanamume waliyekuwa wakiishi nyumba moja na kula moyo wake na ubongo wake. Alexander Kinyua, 22, alikiri mashtaka ya mauaji ya Kujoe Bonsafo Agyei-Kodie, 37, katika jimbo la Maryland mwaka jana lakini Jaji akasema hafai kulaumiwa aliposhtakiwa Jumatatu wiki hii. Jaji Stephen Waldron alisema Kinyua hawezi kulaumiwa kwani alikuwa anaugua akili na akaagiza awekwe kwenye hospitali ya watu wenye akili punguani. Kinyua, aliyekuwa mwanafunzi wa uhadhisi katika chuo cha Morgan State, aliambia maafisa kwamba alitumia kisu kuua mwenzake kabla ya kula viungo vyake. Agye

Tuhuma nzito : Magufuli, Mwakyembe, Lukuvi kufikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge

Image
Dar es Salaam.  Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imesema itawafikisha kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akiwatuhumu kwa kulidanganya Bunge. Hatua hiyo ilitangazwa jana na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe baada ya kumhoji Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango kuhusu hati ya mashaka waliyoipata kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mwaka wa fedha 2011/2012. Kamati hiyo ilieleza kuwa kwenye Bajeti ya mwaka huo kiasi cha Sh348,075,000,000 fedha za ndani zilizokuwa zimetengwa chini ya fungu lililotajwa kuwa ni la mradi maalumu (Special Road Construction Project) hazikutumiwa kwa malengo yaliyoelezwa bungeni. “Ni vizuri leo uiambie kamati fedha hizi ziliombwa kwa kitu gani na zilitumika kwa jambo gani. Tunajua kwamba fedha

Mungu aliniamuru nijiuzulu, asema Papa Benedict XVI

Image
Rome, Italia. Miezi sita baada ya kujiuzulu, Papa Benedict XVI, amefungua mdomo na kueleza sababu za kufikia uamuzi huo wa kushangaza. Jana, vyombo vya habari vilimkariri Papa Mstaafu Benedict akimweleza mgeni wake kuwa aliitwa na Mungu kwa miujiza. P.T Kiongozi huyo ambaye alishangaza watu kwa uamuzi huo wa Februari 8, mwaka huu, hata hivyo alisema sauti ya Mungu imejibu kupitia kwa mfuasi wake, Papa Francis. Papa Benedict alitangaza uamuzi wa kujiuzulu Februari 11, maelezo yake yalielekeza katika afya yake. Alisema nguvu zake zilikuwa zimepungua kiasi cha kutokuweza kumudu majukumu yake ipasavyo. Alisema, "Mungu aliniambia 'niondoke,' nami nikatimiza wajibu huo bila kusita," alisema Papa Benedict ambaye amekuwa kiongozi wa kwanza kufikia uamuzi huo baada ya miaka 600 ya Kanisa Katoliki. Alisema tangu wakati huo ameishi maisha ya sala. Mkongwe huyo mwenye umri wa mi

HURUMAA...MZEE GURUMO ASTAAFU MUZIKI..AMWAGA CHOZI ASEMA HANA HATA BAISKELI

Image
Mzee Muhidin Gurumo (katikati) akizungumza na wanahabari wakati akitangaza kustaafu rasmi kazi ya muziki katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni mdau wa muziki Juma Mbizo na Meneja wa Msondo Ngoma, Said Kibiriti (kushoto). (Picha na Magreth Kinabo). Mwanamuziki mkongwe wa bendi ya Msondo Ngoma Mzee Muhidin Gurumo leo amestaafu rasmi kazi ya muzika alioifanya kwa muda wa miaka 53. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mzee  Gurumo mwenye umri wa miaka 73 amesema ameamua kustaafu kazi hiyo kwa hiari yake mwenyewe kutokana na umri wake kuwa mkubwa. Mzee Gurumo amesema “Muziki kwangu umekuwa kama asili yangu na kazi yangu lakini nimeamua kustaafu kutokana na umri wangu na nitabaki kuwa mshauri tu kwa mwanamuziki yeyote atakayetaka ushauri wangu”. Pamoja na kufanya kazi ya muziki Gurumo amesema kuwa hakupata mafanikio makubwa zaidi ya kujenga nyumba anayoishi na familia yake. Amesema ameimba kwa muda mrefu

WAZIRI MKUU PINDA AFUNGUA KONGAMANO LA UWEKEZAJI MANYARA

Image
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama asali wakti alipotembela Banda la Halmashauri ya Wilaya Mbulu  kabla ya kufungua kongomano la  Kwanza la  Uwekezaji katika mkoa wa Manyara  mjini Babati  Agosti 22, 2013.  Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dr, Mary Nagu na Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, Erasto Mbwilo.(Picha na Ofisi  ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama asali wakti alipotembela Banda la Halmashauri ya Wilaya Mbulu  kabla ya kufungua kongomano la  Kwanza la  Uwekezaji katika mkoa wa Manyara  mjini Babati  Agosti 22, 2013. (Picha na Ofisi  ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akitazama  mbolea  wakati alipotembelea  banda la kiwanda cha Mbolea cha Minjingu  kabla ya kufungua Kongamano  la Kwanza  la Uwekezaji  katika  Mkoa wa  Manyara mjini Babati Agosti 22, 2013. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Manyara, Erasto Mbwilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wanachama wa    k

Rais Museveni afunguka asema masomo ya ‘Arts’ yanachangia ongezeko la wahitimu wasio na ajira.

Image
  Rais Museveni wa Uganda amewakosoa wataalam wa elimu nchini humo kwa kuhamasisha masomo ya ‘Arts’ ambaye amedai yanachangia kuwepo kwa kiwango kikubwa cha wahitimu wa Vyuo Vikuu wasio na ajira. Akizungumza katika Sherehe za Shule ya Msingi ya Mchanganyiko ya Ibanda katika mji wa Ibanda, rais Museveni amesema katika miaka iliyopita aliwaambia wataalam wa elimu na wasomi kutoa muongozo wa fani na pia kuhamasisha masomo ambayo yanauzika, lakini hawakumsikiliza. Badala ya kuhamasisha masomo ya sayansi, rais Museveni amesema mameneja wa vyuo na taasisi za elimu waliwaacha wanafunzi kuendelea kusoma kozi zisizo na soko kama ‘Jinsi ya Kutatua Migogoro’ na ‘Saikolojia’. Aidha amewaasa wanafunza kuwa na nidhamu na kuepuka ngono katika umri mdogo, na kuongeza kuwa wanahitaji kuchanganya euelewa wa elimu ya asili nay a kisasa ili waweze kufanikiwa kimaisha. PATA MATUKIO YOTE HAPA:NAKUOMBA LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK

LIYUMBA MAJI SHINGONI TENA,MKE WAKE AMPANDISHA KIZIMBANI

Image
Amatus Liyumba. Mke wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu (BoT), Amatus Liyumba, Aurelia Ngowi amefungua kesi ya madai akipinga mumewe kuuza mali za familia na kumfukuza kwenye nyumba wanayoishi. Aidha,  anaiomba Mahakama iamuru yeye na watoto wake waendelee kuishi kwenye nyumba hiyo, hadi shauri hilo litakapokwisha. Mama huyo anadai Liyumba aliwafukuza na kuweka walinzi ili wasiingie kwenye nyumba hiyo. Kesi hiyo imefunguliwa mbele ya Hakimu Mkazi Jackline Rugemalila katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam. Katika hati ya madai, Aurelia anaiomba Mahakama iweke zuio la muda ili Liyumba asiuze mali za familia, pia asiuze nyumba iliyopo Africana Mbezi Beach, katika kiwanja namba 2232/2233 ambayo walikuwa wanaitumia kama makazi ya familia. Aurelia ameiomba Mahakama iamuru waendelee kuishi katika nyumba hiyo wakati shauri hilo likiendelea pia mshitakiwa alipe gharama za uendeshaji wa kesi. K

WATU SABA WANUSURIKA KWA AJALI YA NDEGE ILIYOTUA ZIWA MANYARA

Image
Ndege ndogo ya shirika la Tanzanair iliyokuwa ikitokea mjini Bukoba mkoani Kagera kwenda Dar ss Salaam imelazimika kutua kwa dharura katika ziwa Manyara baada ya injini yake moja kuzimika ghafla ikiwa angani.  Ndege hiyo ilikuwa na abiria sita na rubani mmoja ambapo wote wamejeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Seliani mjini Arusha kwa matibabu. Chanzo: ITV

MKUU WA FFU - ARUSHA NA POLISI WENGINE WATATU WAFUKUZWA KAZI

Image
Imeandikwa na Lydia Churi — Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewavua madaraka Maafisa wanne wa Jeshi la Polisi nchini na kumsimamisha kazi mmoja ambaye atafunguliwa mashtaka ya kijeshi kutokana na kukiuka maadili na taratibu za jeshi hilo. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Waziri Nchimbi amesema hatua hiyo ni katika kuendeleza vita ya kuhakikisha kuwa jeshi la polisi linakuwa na nidhamu, linatekeleza wajibu wake wa kutenda haki na kuwalinda raia na mali zao. Alisema amewachukulia hatua Maafisa hao baada ya kuridhia maoni ya kamati aliyoiunda kufanya uchunguzi wa matukio yaliyolalamikiwa dhidi ya askari polisi katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro na Kigoma kati ya Desemba 2012 na Mei, 2013. Waziri Nchimbi aliwataja waliovuliwa madaraka kuwa ni Mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoani Arusha Mrakibu wa Polisi Ramadhan Giro, Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro Inspekta Jamal Ramadhan, Mku

MANAIKI SANGA ATIWA MBARONI.....PICHA ZA UCHI ZIMEMPONZA....HIZI NI PICHA ZINGINE 400 AKIWA MTUPU

Image
    Jeshi la polisi kanda ya Dar es Salaam linadaiwa kumtia mbaroni msanii anaetuhumiwa kupiga picha chafu na wanawake mchanganyiko wakiwema mamiss maarufu na baadae kusambaza kwenye mitandao yote ya kijamii pamoja na kuripotiwa kwenye magazeti mbalimbali   Mwandishi wetu amefanikwa  kuzinasa  picha  za  Manaiki  akiwa chini ya ulinzi wa  polisi huku akiwa amevishwa pingu na kurukishwa kichurachura.   Habari za uhakika zilizonaswa  zinasema kuwa msanii huyo alikamatwa siku chache baada kuvuja kwa picha zake za aibu zikimuonesha akiwa na wanawake tofauti tofauti.   HIZI  NI  PICHA  ZAKE  NYINGINE  400  AKIWA  MTUPU  NA  MADEMU  ZAKE..... << PICHA, BOFYA  HAPA>>