WENGER AMGEUKIA FLAMINI, AMREJESHA EMIRATES

flamini d9c37
Mathieu Flamini
KOCHA Arsene Wenger yuko katika siku 12 ngumu za kukimbizana kukamilisha usajili kabla ya dirisha kufungwa na sasa amehamishia ndoana zake kwa Mathieu Flamini, kiasi cha miaka mitano tangu aondoke Arsenal kuhamia AC Milan. (HM)

Klabu hiyo ya Italia imemtema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 mwishoni mwa msimu na sasa kiungo huyo kiasi cha wiki mbili amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha Wenger.

Kocha wa Arsenal amevutiwa kiasi cha kutosha na hali ya mchezaji huyo na yuko tayari kumpa ya Mkataba Flamini baada ya kukubali kurejea nyumbani licha ya kutakiwa na klabu nyingine.
Atakuwa mchezaji wa pili kusainiwa na Wenger majira haya ya joto— wote wachezaji huru — na mchezaji wa nne wa zamani wa timu hiyo kusainiwa tena na kocha huyo, baada ya awali kuwarejesha Sol Campbell, Jens Lehmann na Thierry Henry Emirates.

Wenger anatumai dili hilo litafuatiwa na usajili wa mchezaji mqwenye jina kubwa katika klabu hiyo.
Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema ni mchezaji anayetakiwa zaidi kwa sasa na Wenger baada ya kushindwa kuwapata Luis Suarez au Wayne Rooney.

Na Mfaransa huyo pia ametenga dau kubwa zaidi kwa ajili ya mchezaji mwenzake Benzema, Angel Di Maria, na pia atarajea na ofa nzuri zaidi kwa ajili ya kiungo wa Newcastle Yohan Cabaye na kipa wa Valencia, Vicente Guaita.

Mchezajhi mmoja tu ambaye anaweza kuondoka kwa sasa ni Lukas Podolski, ambaye anatakiwa na Schalke. Chanzo: Binzubeiry

Comments

Popular posts from this blog