Skip to main content

Rais Museveni afunguka asema masomo ya ‘Arts’ yanachangia ongezeko la wahitimu wasio na ajira.


 

Yoweri-Museveni
Rais Museveni wa Uganda amewakosoa wataalam wa elimu nchini humo kwa kuhamasisha masomo ya ‘Arts’ ambaye amedai yanachangia kuwepo kwa kiwango kikubwa cha wahitimu wa Vyuo Vikuu wasio na ajira.
Akizungumza katika Sherehe za Shule ya Msingi ya Mchanganyiko ya Ibanda katika mji wa Ibanda, rais Museveni amesema katika miaka iliyopita aliwaambia wataalam wa elimu na wasomi kutoa muongozo wa fani na pia kuhamasisha masomo ambayo yanauzika, lakini hawakumsikiliza.
Badala ya kuhamasisha masomo ya sayansi, rais Museveni amesema mameneja wa vyuo na taasisi za elimu waliwaacha wanafunzi kuendelea kusoma kozi zisizo na soko kama ‘Jinsi ya Kutatua Migogoro’ na ‘Saikolojia’.

Aidha amewaasa wanafunza kuwa na nidhamu na kuepuka ngono katika umri mdogo, na kuongeza kuwa wanahitaji kuchanganya euelewa wa elimu ya asili nay a kisasa ili waweze kufanikiwa kimaisha.

Comments

Popular posts from this blog