MERKEL APENDEKEZA MARUFUKU YA SILAHA MISRI

Ujerumani imependekeza kupiga marufuku upelekaji wa silaha nchini Misri kama hatua itakayoratibiwa kwa pamoja na Umoja wa Ulaya kupinga hatua ya serikali ya Misri ya kuvunja maandamano kwa kutumia nguvu na kusababisha umwagaji damu. Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ametowa wazo hilo katika mahojiano na televisheni la taifa hapo jana. Kansela Merkel amesema hatua zote zinaweza kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku kupeleka silaha nchini Misri zikiwemo zile ambazo tayari zimeidhinishwa kwa serikali ya Misri.

Amesema suala hilo litajadiliwa kati ya Ujerumani na washirika wenzake wa Umoja wa Ulaya katika mkutano utakaofanyika siku chache zijazo. Umoja wa Ulaya utakuwa na kikao chake cha kwanza cha mazungumzo ya dharura kutokana na umwagaji damu nchini Misri uliozusha wasiwasi mkubwa huku ukionya kwamba utaangalia upya uhusiano wake na nchi hiyo iliokumbwa na ghasia.

Comments

Popular posts from this blog