ANGALIA PICHA ZA MSAFARA WA MBIO ZA MWENGE ULIVYOPATA AJALI MKOANI DODOMA:



MBIO za Mwenge wa Uhuru uliokuwa ukikimbizwa katika Wilaya ya Dodoma mjini zimeingia Dosari baada ya kupata ajali kilometa 3 kabla ya kukabidhiwa wiliya ya Mpwapwa.
Ajali hiyo iliyotokea jana majira ya 2;24 asubuhi katika mtelemko wa mlima fufu wilayani Chamwino na kusababisha watu 5 kujeruhiwa na kukimbizwa katika hospital ya mkoa wa dodoma.
Watu hao ambao majina yao Bado hayajatambulika walipata majeraha katika maeneo mbali mbali ya miili yao ikiwemo kichwani, kifuani, mguuni na mikononi.




Kaimu Kamanda wa polisi Suzan Kaganda aliyefika na kujione hali ilivyokuwa katika eneo hilo alisema chanzo cha ajali hiyo ni Matuta yaliwekwa kwenye Barabara hiyo inayojengwa kwa kiwango cha lami toka fufu hadi Dodoma bila kuwa na alama yoyote.

 majeruhi akisaidiwa kupekwa kwenye gari tayari kukimbizwa hospital


 gari iliyokuwa imembeba kiongozi wa mbio za mwenge ikiwa imeumia vibaya







 majeruhi wakipatiwa huduma ya kwanza kabla ya kukimbizwa katika hospitali ya mkoa wa dodoma kwa matibabu








 huduma ya kwanza

Comments

Popular posts from this blog