Posts

Breaking News: Waziri Mwigulu Amsimamisha Kazi Merlin Komba

Image
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema Waraka wa barua unaodaiwa kuandikwa na Serikali dhidi ya Makanisa unaosambaa mitandaoni si wa kweli na kwamba ni uhalifu umefanywa na watu wasioitakia nchi mema. Waziri Nchemba amesema Serikali haipingani na dhehebu lolote na pale ambapo kuna uhitaji wa kufanyia kazi jambo kuhusu taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo taratibu huwa zinatumika kuzungumza na sio kama ilivyofanywa taarifa hiyo inayosambaa. Serikali inalinda uhuru wa kuabudu na waumini hivyo taarifa hiyo inayosambaa ni batili na tayari uchunguzi umeanza kufanyika. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Usajili wa Jumuiya za Kidini na Vyama vya Kijamii, Merlin Komba, kupisha uchunguzi wa barua iliyoandikwa kwa maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. Tunawaomba viongozi wa dini waendelee na kazi zao, nasema jam...

Kutembea haraka kunarefusha Maisha

Image
Leo June 8, 2018 nakusogezea Utafiti uliochapishwa katika jarida la “Mazoezi ya matibabu” huko Uingereza limefafanua uhusiano kati ya maisha marefu na kasi ya kutembea. Wanasayansi wa Uingereza na Australia wameelezea kwamba watu wanaotembea haraka si rahisi kupatwa na ugonjwa wa moyo. Imeonekana kwamba wale walio na umri wa miaka 60 au chini ya hapo ambao wanatembea haraka wamepunguza hatari ya kufariki kutokana na magonjwa ya moyo kwa asilimia 53. Watafiti wanasema kwamba kasi ya Kilomita 5 hadi 7 kwa saa ni ya kutosha. Madaktari wanaamini lengo kamili ni kuharakisha mapigo ya moyo na kutokwa na jasho wakati wa kutembea. Waendesha magari nchini Uingereza ambao hutumia angalau nusu saa kufanya mazoezi na kula vyakula vya afya basi hurefusha maisha kwa miaka kumi.

Mfumo Mpya wa Malipo Mamlaka za Serikali za Mitaa Kuboresha Huduma kwa Wananchi

Image
Mfumo mpya wa malipo epicor toleo Na. 10.2 unaotarajiwa kuanza kutumika Julai 1 mwaka huu na Mamlaka zote za Serikali za Mitaa nchini umeelezwa kuboresha huduma kwa wananchi kutokana na kuwa wa uwazi na kurahisisha kazi kwa watumiaji wa mfumo huo. Akieleza lengo la uboreshaji wa mfumo huo leo, Jijini Dodoma wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa Manunuzi kutoka Halmashauri za Mikoa ya Kigoma, Shinyanga, Dodoma, Arusha, Manyara na Singida, mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Agustino Manda amesema mfumo huo utapunguza kazi na kuongeza ufanisi wa kazi kwa watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa hapa nchini. “Mfumo huu utaweka mambo wazi, watu watawajibika na mtumiaji wa mwisho ambaye ni mteja atapata huduma nzuri na kuridhika na huduma atakayopewa,” amesema Manda. Ameendelea kusema, lengo la kuboresha mfumo huo ni kutoa huduma nzuri kwa Wananchi, Wananchi kutochele...

Maafisa Ugavi Waaswa Kuzingatia Sheria na Kanuni Katika Manunuzi

Image
Maafisa Ugavi Wametakiwa Kuzingatia Sheria Kanuni na Taratibu za Manunuzi ili kuleta thamani halisi ya fedha zinazotumika katika sekta hiyo ili halmashauri zote zitekeleze dhana ya kutoa huduma bora kwa wananchi. Akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa maafisa hao leo Jijini Mbeya, Mkurugenzi msaidizi anayeshughulikia shughuli za Serikali, Idara ya Tawala za Mikoa Bw. Johnson Nyingi amewata  kuzingatia weledi na taratibu zote zinazosimamia sekta ya manunuzi kwa kuzingatia mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 yanayoendelea kwa mikoa ya Mbeya, Rukwa, Njombe na Songwe. Mkurugenzi msaidizi anayeshughulikia shughuli za Serikali, Idara ya Tawala za Mikoa Bw. Johnson Nyingi akifungua mafunzo kwa maafisa ugavi wa mikoa ya Mbeya, Njombe, Rukwa na Songwe leo Jijini Mbeya. Mafunzo hayo yanaendeshwa na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)  kwa ufadhili wa Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Mareka...

Dk Shika amtambulisha rasmi Msanii wake

Image
Dkt. Louis Shika ambaye amejipatia umaarufu baada ya kutangaza dau la kununua nyumba za mfanyabiashara Said Lugumi, amefunguka na kutangaza nia ya kujihusisha na masuala ya muziki nchini Tanzania hasa upande wa kuwasimamia wasanii wachanga na wakubwa. Dkt. Shika ametoa kauli hiyo leo Juni 08, 2018 wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam na kusema siku si nyingi atatangaza jina rasmi ya label yake ambayo itakuwa inajuhusisha na kusimamia kazi za wasanii wa BongoFleva huku akidai lengo lake kubwa ni kutaka kutimiza ndoto za kila mmoja kupitia sanaa. "Sasa tutaelewana tu na kabla hatujaanza na masuala ya viwanda 30 nilivyo vitaja na 'different services', kwa sasa ninaanza na 'music industry' na tunaanzia kwa msanii mmoja ambaye anaitwa Godson anayetokea Songea na hili nina uhakika watanzania watafurahi na kufuta 'stress' mbalimbali zilizokuwa zinawasumbua", amesema Dkt. Shika. Pamoja na hayo, Dkt. Sh...

United Wamsajili Beki wa Porto

Image
Beki Diogo Dalot KLABU ya Man United imekamilisha usajili wa beki Diogo Dalot kutoka kwenye kikosi cha Porto cha Ureno. Huu ni usajili mwingine wa kocha wa Man United, Jose Mourinho, ambaye anataka kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu ujao. Beki huyo mwenye umri wa miaka 21, amejiunga na timu hiyo ya United kwa usajili wa pauni milioni 17.4 zaidi ya shilingi bilioni 37. Akiwa na kikosi cha Porto, beki huyo alianza kucheza kwenye kikosi cha kwanza mwanzoni mwa mwaka huu na kuonyesha kiwango cha hali ya juu. Dalot amesaini mkataba mrefu wa miaka mitano na timu hiyo ya England akiwa anaaminika kuwa atacheza kikosi cha kwanza chini ya kocha huyo Mreno. United wanaamini kuwa beki huyo atamsaidia Antonio Valencia, ambaye ana umri wa miaka 33 na anaonekana kuwa anaweza akashindwa kuwika msimu ujao kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya goti mara kwa mara. Kinda huyo mwenye umri wa miaka 19, anaweza pia kucheza kama beki wa kushoto na aliitumikia Porto...

Huwezi Kufanikiwa Penzini Bila ‘Mishale’, Ipokee Kadiri Uwezavyo!

Image
U NAPO-MUONA mtu amefanikiwa kwenye uhusiano wake, amefunga ndoa na mwenza wake na kufanya sherehe, akili ya harakaharaka inaweza kukutuma uamini tu kwamba mambo ni rahisi tu. Kwamba walikutana tu mahali fulani, wakakubaliana na kuanza safari ya urafiki, uchumba na mwisho wa siku wakaingia kwenye ndoa. Bahati mbaya sana ni kwamba, unawakuta kwenye mafanikio. Unahisi pengine hawatumii nguvu nyingi kuendesha maisha yao na wanaelewana, hawagombani na kila uchwao wanafurahia maisha yao ya uhusiano. Ndugu zangu, licha ya kwamba kila mtu ana historia yake na wapo ambao huingia kwenye ndoa bila kupitia changamoto nyingi, lakini kikubwa ninachoweza kukuhakikishia mimi ni kwamba, changamoto ni lazima uzipitie ili uweze kufikia malengo yako. Tunafahamu kwamba kila mmoja anatamani aishi maisha mazuri yasiyokuwa na kelele, yasiyokuwa na misukosuko, lakini dunia ya wapendanao haipo hivyo. Mnakutana watu ambao hamjakua pamoja, mna tamaduni tofauti hivyo lazima mkumbane na chang...

Yanga yamwandikia barua Manji

Image
MAANDALIZI ya Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Yanga yamekamilika kwa asilimia kubwa huku ikipanga kutoa mwaliko maalum kwa aliyekuwa mwenyekiti na mfadhili wao Yusuf Manji. Yanga imepanga kufanya mkutano huo Jumapili hii kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi, Masaki jijini Dar es Salaam. Akizungumza na Championi Ijumaa, Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa alisema tofauti na Manji wamepanga kuwaandikia barua ya mwaliko viongozi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. “Baadhi ya ajenda zitakazowasilishwa kwenye mkutano huo ni pamoja na ushiriki wa Yanga katika michuano ya kimataifa ikiwemo hatua tuliyofikia kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho, Mapato na Matumizi, bila ya kusahau mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji. “Pia, suala la uchaguzi wa kujaza nafasi zilizokuwa wazi huenda likawasilishwa kupitia mengineyo ingawa kuna uwezekano mkubwa kwa ajenda hiyo kuondolewa ili kuwapa...

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA HOSPITALI YA CCBRT JIJINI DAR

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia  hali mtoto Luke Maulid mwenye umri wa miaka 4 kutoka Mtwara ambaye anapata matibabu ya  mguu katika hospitali ya CCBRT.  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza  na Bibi Helena Mjinja mwenye umri wa miaka 64 kutoka Musoma anayepata matibabu ya Fistula  katika hospitali ya CCBRT jijini    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanawake ambao wamepata matibabu ya Fistula na kupona na kisha kufundishwa kazi za mikono katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata  maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Hospitali ya CCBRT Bw.Erwin Telemans juu  ya utengenezaji wa viungo bandia vinavyotengenezwa kwa utaalamu wa hali ya juu. Baad...

MATUKIO KATIKA PICHA ZOEZI LA KUAGA MIILI YA MAPACHA MARIA NA CONSOLATA IRINGA

Image
HUKU zoezi la  kuaga   na mazishi ya  mapacha  Maria na  Consolata  Mwakikuti yanafanyika  leo  katika  makaburi ya  viongozi wa  dini ya  Romani Katoliki  (RC)  Tosamaganga   kata ya Kalenga wilaya ya  Iringa  mkoani Iringa  wanawake  walioshiriki kuchimba  kaburi la mapacha hao lenye upana wa sentimita 180 na urefu  sentimita 200 wameomba  sanduku la mapacha hao  kubebwa na  wanawake   kabla ya  kuingizwa kaburini.               Akizungumza  jana  makaburini  hapo kwa niaba ya  wanawake wa kata ya  Kalenga  Geogena   Sekitindi (57) alisem...