Maafisa Ugavi Waaswa Kuzingatia Sheria na Kanuni Katika Manunuzi
Maafisa Ugavi Wametakiwa
Kuzingatia Sheria Kanuni na Taratibu za Manunuzi ili kuleta thamani
halisi ya fedha zinazotumika katika sekta hiyo ili halmashauri zote
zitekeleze dhana ya kutoa huduma bora kwa wananchi.
Akizungumza wakati akifungua
mafunzo kwa maafisa hao leo Jijini Mbeya, Mkurugenzi msaidizi
anayeshughulikia shughuli za Serikali, Idara ya Tawala za Mikoa Bw.
Johnson Nyingi amewata kuzingatia weledi na taratibu zote zinazosimamia
sekta ya manunuzi kwa kuzingatia mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor
10.2 yanayoendelea kwa mikoa ya Mbeya, Rukwa, Njombe na Songwe.
Mkurugenzi msaidizi
anayeshughulikia shughuli za Serikali, Idara ya Tawala za Mikoa Bw.
Johnson Nyingi akifungua mafunzo kwa maafisa ugavi wa mikoa ya Mbeya,
Njombe, Rukwa na Songwe leo Jijini Mbeya.
Mafunzo hayo yanaendeshwa na Ofisi
ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa ufadhili
wa Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la
Marekani (USAID) na kutekelezwa kupitia mradi wa uimarishaji wa mifumo
ya sekta za umma (PS3). Mradi huu ni wa miaka mitano na unatekelezwa
katika mikoa 13 ya Tanzania bara.
“ Mafunzo haya yanalenga
kuwajengea uwezo maafisa ugavi ili kuongeza tija katika huduma mnazotoa
kwa wananchi, mifumo ipo ili kuwezesha utendaji wenu uwe na tija kwa
wale mnaowahudumia” Alisisitiza Bw. Nyingi
Akifafanua amesema kuwa washiriki
wanalo jukumu la kushauri viongozi wao katika maeneo yao juu ya namna
bora yakutumia rasilimali fedha wakati wa kufanya manunuzi yanayolenga
kuwasaidia wananchi kupata maendeleo endelevu .
Aliongeza kuwa mafunzo kwa maafisa
ugavi hao yamekuja wakati muafaka ambapo Serikali ya Awamu ya Tano
imeweka kipaumbele katika usimamizi wa rasilimali fedha katika
halmashuri zote ili ziweze kuwanufaisha wananchi wote.
“ Zaidi ya asilimia 70 ya fedha za
Serikali zinatumika katika manunuzi hivyo jukumu la maafisa ugavi ni
kuhakikisha kuwa sheria na taratibu zote za manunuzi zinazingatiwa
kikamilifu” Alisisitiza Bw. Nyingi.
Afisa Ugavi Kutoka Halmashauri ya
Manispaa ya Sumbawanga Bw. Martin Sanane ambaye alikuwa Mwenyekiti wa
mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 yanayowashirikisha Maafisa
Ugavi wa mikoa ya Mbeya, Njombe, Rukwa na Songwe yanayofanyika kwa siku
mbili kuanzia leo Jijini Mbeya .
Kwa upande wake mmoja wa
wawezeshaji wa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 kutoka Ofisi
ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) Bw. Allan
Bendera amesema kuwa jambo la muhimu kwa maafisa ugavi pamoja na mafunzo
ya matumizi ya mfumo huo ni kuwa wazalendo katika kutekeleza majukumu
yao kwa maslahi ya Taifa.
Aliongeza kuwa jukumu la maafisa ugavi ni chachu katika kuchochea maendeleo katika halmashauri zote hapa nchini.
Pia aliwaasa washiriki wa mafunzo
hayo kuzingatia yale watakayojifunza ili yaweze kuwanufaisha wale ambao
hawakushiriki katika mafunzo hayo.
Mkurugenzi msaidizi
anayeshughulikia shughuli za Serikali, Idara ya Tawala za Mikoa Bw.
Johnson Nyingi akisisitiza umuhimu wa maafisa manunuzi katika kuleta
tija kwa huduma zinazotolewa kwa wananchi.
Kiongozi wa Timu ya Habari na
Mawasiliano PS3 Bi. Leah Mwainyekule akifurahia jambo na Mshauri wa
mifumo ya fedha wa PS3 Bw. Ramadhani Mseya (katikati) na Meneja Mradi wa
PS3 mkoa wa Rukwa Bi. Rose Mangilima (kushoto) .
Mkurugenzi msaidizi
anayeshughulikia shughuli za Serikali, Idara ya Tawala za Mikoa Bw.
Johnson Nyingi (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya
washiriki wa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 ambao ni
maafisa ugavi wa mikoa ya Mbeya, Njombe, Rukwa na Songwe leo Jijini
Mbeya.
Mkurugenzi msaidizi
anayeshughulikia shughuli za Serikali, Idara ya Tawala za Mikoa Bw.
Johnson Nyingi akifurahia jambo na wawezeshaji wa mafunzo ya matumizi
ya mfumo wa Epicor 10.2 kutoka Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambao ni mchumi kutoka Idara ya Sera na
Mipango Bw. Allan Bendera (kulia) na Afisa Usimamizi Fedha Bw. Mmaka
Mwinjaka (katikati) leo Jijini Mbeya mara baada ya kufungua mafunzo hayo
yaliyowashirikisha maafisa ugavi wa mikoa ya Njombe, Rukwa, Mbeya na
Songwe.
Sehemu ya Washiriki wa mafunzo
hayo wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati wa mafunzo ya matumizi ya
mfumo wa Epicor 10.2 yaliyowashirikisha maafisa ugavi wa mikoa ya
Njombe, Rukwa, Mbeya na Songwe leo Jijini Mbeya.
Mwezeshaji wa mafunzo ya matumizi
ya mfumo wa Epicor 10.2 kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) Bw. Allan Bendera akisisitiza umuhimu wa
maafisa ugavi kuzingatia uzalendo katika kutekeleza majukumu yao wakati
akiwasilisha mada kwa maafisa ugavi wa mikoa ya Njombe, Rukwa, Mbeya na
Songwe leo Jijini Mbeya kuhusu mfumo wa Epicor 10.2 leo Jijini Mbeya.
(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO, Mbeya
Comments
Post a Comment