MATUKIO KATIKA PICHA ZOEZI LA KUAGA MIILI YA MAPACHA MARIA NA CONSOLATA IRINGA
HUKU zoezi la kuaga na
mazishi ya mapacha Maria na Consolata Mwakikuti yanafanyika leo
katika makaburi ya viongozi wa dini ya Romani Katoliki (RC)
Tosamaganga kata ya Kalenga wilaya ya Iringa mkoani Iringa
wanawake walioshiriki kuchimba kaburi la mapacha hao lenye upana wa
sentimita 180 na urefu sentimita 200 wameomba sanduku la mapacha hao
kubebwa na wanawake kabla ya kuingizwa kaburini.
Akizungumza
jana makaburini hapo kwa niaba ya wanawake wa kata ya Kalenga
Geogena Sekitindi (57) alisema kuwa mbali ya uchungu waliokuwa
nao juu ya vifo vya mapacha hao ila wangefurahi zaidi iwapo
wangepewa jukumu la kubeba jeneza lao mara baada ya kufika eneo
la mazishi.
“
Pamoja na kuwa jukumu la kuchimba kaburi la watoto hao wamepewa
vijana wa waliopo katika mashirika ya kitume ya RC hapa
Tosamaganga ila mimi kama mwanamke na binti huyo ambae alipata
kushiriki semina na mapacha hao enzi za uhai wao tumeona ni
vema tushiriki hata zoezi la uchimbaji wa kaburi lao ila
ingependeza leo wakati wa mazishi tupewe nafasi wanawake kubeba
jeneza lao” alisema Sekitindi
Kuwa
heshima kubwa ambayo Kalenga imepewa ya mapacha hao kuzikwa
Tosamanganga ni heshima kubwa iliyoambatana na huzuni kubwa ila
njia pekee ya kuenzi heshima hiyo juu ya watoto hao ni ushiriki
mkubwa wa wanawake katika mazishi hayo .
Kwani
alisema ushiriki wao wanawake ni sehemu ya kuifuta machozi familia
ya Mapacha hao pamoja na walezi wa shirika la Maria Consolata
ambao waliwalea mapacha hao toka utoto wao.
Aisha
Kibindo (16) ni mkazi wa kata ya Kalenga ambae amepata kushiriki
mafunzo na marehemu hao enzi za uhai wao alisema kuwa kwa mara ya
kwanza alipata kushiriki mafunzo ya kiroho ya mapacha hao mafunzo
yaliyokuwa yameandaliwa na kanisa na ndipo alipokutana nao .
Kuwa
imani yake kuja kuonana nao katika mafunzo mengine kwani
waliahidi kuwa wataendelea kushiriki mafunzo mbali mbali na jamii ya
Iringa ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri kwa washiriki juu ya namna
gani wanaweza kuishi kama mabinti kwa kujitunza na kuzingatia
masomo .
“
Tukiwa katika mafunzo Maria na Consolata walikuwa wakitutia moyo
wa kusonga mbele kimasomo ya kuwataka wale ambao
hawakubahatika kufaulu kutokata tamaa kwani kuna maisha mengine
mazuri nje ya kufaulu ila iwapo watakuwa watii na wenye
heshima kwa wale wanaoishi nao”
Alisema
mafundisho na ushauri wao kwa washiriki wa warsha hiyo ya
kiroho yaliwagusa mabinti wengi na baadhi ya wale ambao
hawakubahatika kuendelea na elimu akiwemo yeye wanaishi kwa
kuzingatia mafundisho hayo na hadi sasa hajutii kutofaulu ila
anajipanga kuona anatafuta njia ya kuendelea kupambana na maisha
kwa kujiendeleza zaidi kielimu.
Wilbert
Kihwele ni kiongozi wa vijana wachimbaji na wajenzi wa kaburi la
Maria na Consolata anasema kuwa uchimbaji wa kaburi hilo umeanza
majira ya saa 2 asubuhi hadi saa 7.20 mchana na kuwa ni moja kati
ya kaburi ambalo wamechimba kwa muda mrefu ukilinganisha na
makaburi mengine ambayo wamepata kuchimba katika eneo hilo .
Kihwele
alisema kwa kawaida kaburi kawaida huwa linachukua kati ya saa
1.30 hadi saa 2 kutokana na aina ya udongo wanakutana nao na upana wa
kaburi na kuwa udongo wa eneo hilo ni wa kawaida na makaburi
ambayo huwa wanachimba ni urefu huwa sentimita kati ya 95 hadi
100 na upana kati ya sentimita 40 hadi 45 ila kaburi hilo
limeweza kuchukua muda mwingi kutokana na urefu kuwa sentimita 200
na upana sentimita 180.
Alisema
ukubwa huo unatokana na vipimo vya Sanduku ambavyo walipewa na
kuwa Sanduku la Maria na Consolata lina upana wa Sentimita 90 na
urefu sentimita 160 na kuwa kwa upande wa kaburi baadhi ya
sentimita zimeongezwa kwa ajili ya ujengaji wa kaburi .
Kiongozi
huyo alisema zoezi hilo la kuchimba kaburi na kujenga wanalifanya
kwa kujitolea na hakuna malipo yoyote ambayo wao watalipwa na
hawana kawaida ya kulipwa kwa kazi ya kuchimba kaburi na kuwa wao
ni vijana wanaotoka ndani ya mashirika na jumuiya za kanisa na
hilo ni jukumu lao.
Akizungumza
kwaniaba ya chifu wa wahehe Adam Abdu Sapi ambae ni mwanafunzi
kuhusiana na uamuzi wa familia ,serikali na shirika la Maria
Consolata la kuwazika mapacha hao katika kata ya Kalenga ambayo ni
kata aliyozikwa chifu Mkwawa mwakilishi wa chifu huyo Gerald Malangalila
pamoja na kusikitishwa na kifo cha Mapacha hao ila alisema
serikali ilipaswa kuwashirikisha Machifu katika vikao hivyo .
“
Juu ya vifo vya Mapacha hao tumesikia na tumesikitishwa sana
kuondokewa na watoto hawa ambao ni yatima na baba yao alikuwa ni
mwenyeji wa Mbeya na mama Mwenyeji wa Bukoba na sisi sote ni
watanzania hatupaswi kutengana uamuzi wa kuwazika Kalenga ni mzuri
ila ningeshirikishwa kama Chifu katika vikao vya maandalizi
tungewazika kwa heshima ya chifu wetu Mkwawa tungepiga risasi
kaburini na hewani mimi na wenzangu tungepewa usafiri tungefika
shida usafiri “
Alisema
chifu huyo kuwa iwapo serikali ingewashirikisha katika vikao
wangeweza kushiriki kikamilifu maana msiba huo ni mkubwa na
mazishi yanafanyika katika ardhi ya chifu Mkwawa hivyo wangeweka
utaratibu wa kuwapa heshima za kichifu watoto hao ambao
wameondoka ila wameacha historia kubwa katika Taifa na Kalenga .
Akizungumza
kwa njia ya simu akiwa safarini juu ya madai ya chifu wa wahehe
mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema kuwa mkoa umekuwa na
ushirikiano mkubwa na machifu hao pamoja na makundi yote yakiwemo
yote zikiwemo taasisi za dini ila katika suala hilo la mazishi
ya mapacha hao yafanyike wapi ni suala la kifamilia na kanisa
kupitia shirika la Maria Consolata sio serikali ila serikali
imeshirikishwa tu.
”
Hili ni suala la Kanisa na familia serikali imeshirikishwa tu
hivyo namba kama ambavyo watu wengine watakavyoshiriki tunaomba
nao waweze kushiriki kama waombolezaji wengine hatuwezi kuingilia
maamuzi ya kanisa “
Katika mazishi hayo askofu wa jimbo la Iringa Tarcisius Ngalalekumtwa ambae
ni Rais wa baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) anataraji
kuongoza mazishi hayo huku upande wa serikali Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia imekanusha taarifa zilizoenea ya kuwa, Waziri wa Elimu Prof.Ndalichako
anakusudiwa kushiriki mazishi hayo na viongozi wengine wengi
wakiwemo wakuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah , mkuu wa wilaya ya
Iringa Richard Kasesela na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza .
Maria na Consolata
walizaliwa mwaka 1996 katika kijiji cha Ikonda wilaya ya Makete na
walelelewa na shirika la Maria Consolata ,walisoma shule ya msingi
Ikonda Makete na sekondari walisoma Kilolo mkoani Iringa katika
shule ya Maria Consolata na elimu yao ya kidato cha tano na sita
waliipata shule ya Udzungwa iliyopo wilaya ya Kilolo mita chache
kutoka shule ya sekondari ya Maria Consolata na kituo walichokuwa
wakiishi cha Nyota ya Asubuhi kifo chao kilitokea Juni 3 mwaka
huu majira ya saa 2 usika katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
ambako walikuwa wakipatiwa matibabu
Comments
Post a Comment