Posts

Madhara Ya Kula Mayai Yasipoiva Vizuri Kwa Afya

Image
Mayai ni moja ya vyakula vyenye viini lishe muhimu kwa ajili ya afya ya mwili wa binadamu. Kwa kawaida mayai kabla ya kuliwa, huandaliwa kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuchemshwa, kukaangwa au kuchanganywa na vyakula vingine kama vipande vya viazi mviringo ambavyo ni maarufu kwa jina la chips. Pia, kuna baadhi ya watu wanaopendelea kula mayai mabichi kama dawa ya tiba mbadala, kwa ajili ya kulainisha sauti na wengine hupendelea kula mayai ya kukaanga ambayo hayakukaushwa vizuri. Ukitembelea migahawa mingi utabaini kuwa watu wanakuwa na mitazamo tofauti na wanavyopenda kula mayai. Mfano kuna wanaoagiza watengenezewe mayai kwa mtindo unaojulikana kama ‘macho ya ng’ombe.’ Ukiagiza namna hiyo, mpishi atataka kuuliza kama ni ‘macho ya ng’ombe’ ya kugeuza. Ina maana kuwa ‘macho ya ngombe’ ya kugeuzwa ni yale yanayoivishwa pande zote lakini yale ambayo siyo ya kugeuza, huwa linaifa nusu. Upande mmoja unabaki ukiwa mbichi, na ndiyo raha ya baadhi ya watu. Hata u

Kauli ya Louis van Gaal baada ya Ubingwa wa Kombe la FA kwa Man United

Image
Baada ya kufanikiwa kutwaa Kombe la FA akiwa na Man United, Louis van Gaal amezungumza kauli ya kujivunia, licha ya kuwa kibarua chake kipo mashakani kuchukuliwa na Jose Mourinho kwa siku za usoni, licha ya kuwa mchana wa May 21 2016 ulianza kwa headlines zisizo njema kwake. Van Gaal ameripotiwa na Metro na AS kuwa atafukuzwa na Man United nafasi yake kuchukuliwa na Jose Mourinho, hiyo ilikuwa ni saa kadhaa kabla ya BBC na Sky Sports kuziongezea nguvu taarifa hizo, kwa kuripoti habari kama hizo katika tovuti zao. Louis van Gaal amekuwa akiandamwa na tetesi zinazohusu hatma ya kibarua chake, aliongea kauli zya kujivunia kama hana hofu na habari zinazoendelea.‘Hii ni furaha kubwa kwa klabu na mashabiki na kwangu pia ambaye nimefanikiwa kushinda taji hili nikiwa katika nchi nne tofauti ni makocha wachache wanaoweza kujivunia hilo, hivyo nina furaha sana na jambo hili”

Kiba, Diamond Kimenuka Hatari!

Image
    Kimenuka! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mafahari wawili wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kudaiwa kutupiana vijembe vya kufa mtu baada ya kuwepo kwa madai ya Kiba kuhujumiwa.       Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. Kwa mujibu wa chanzo makini, ili kuweka hujuma ya kibiashara, hivi karibuni, pamoja na kukanusha mara kadhaa kutokuwa na tatizo na Kiba, Diamond alidaiwa ‘kutengeneza’ kwa makusudi penzi la mwigizaji Jacqueline Wolper Massawe na msanii wa Wasafi Classic Baby (WCB), Rajabu Abdulhan ‘Harmonize’ kisha kuvujisha video ya uhusiano huo mpya siku ambayo Kiba alikuwa akiuachia wimbo wake mpya wa Aje (Jumamosi iliyopita), lengo likiwa kuhamisha upepo mashabiki kutoka kwenye wimbo mpya na kujali mapenzi ya wawili hao. “Ni hujuma ya kibiashara, Diamond na uongozi wake wameamua kumfanyia Kiba ili wimbo wake ukose kiki kwa watu,” kilidai chanzo chetu. Harmonize VIJEMBE VYATAWALA Hata hivyo, kwa muji

TAARIFA KUTOKA KWA FAMILIA YA MAREHEMU WILSON KABWE KUFUATIA UPOTOSHWAJI WA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI

Image
Familia ya Marehemu Wilson Kabwe  imesikitishwa sana na taarifa zilizosambazwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu kauli na msimamo wa familia katika shughuli za maazishi ya mpendwa wao Wilson Kabwe. Familia inapenda kuchukua nafasi hii kutamka bayana kwamba, Dk. Zawadi Machuve si msemaji wa familia. Kauli yake iliyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba:- " Sisi hapa hatukaribishi viongozi, huu ni msimamo wa familia kama wao watafanya utaratibu wao sawa, lakini hatuko kwa ajili ya viongozi" Kauli hiyo ambayo ililenga kutoishirikisha Serikali katika msiba wa mtumishi wake tunaomba ipuuzwe na siyo kauli ya familia. Familia inatambua na inathamini sana mchango mkubwa wa Serikali katika kugharamia matibabu na  huduma  zote za mazishi. Familia inachukua fursa hii kuwakaribisha viongozi wote wa Serikali, ndugu, jamaa na marafiki wanaopenda kushiriki katika shughuli za mazishi ya mpendwa wetu. Imetolewa na: PHILIP MKENGA KABW

JEMBE FESTIVAL YAWAKUNA WAKAZI WA JIJI LA MWANZA

Image
Msanii kutoka nchini Marekani Neyo akishambulia jukwaa na kuwapagawisha wakazi wa jiji la Mwanza . Neyo akiwa pamoja na Diamond Platnumz jukwaani wakiambulisha wimbo wao mpya mbele ya mashabiki na wapenzi wa muziki wa kizazi kipya. Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Ruby akiimba kwenye tamasha la Jembe Festival kwenye uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza. Rapa Stamina akiupagawisha umma na mistari iliyo simama kwenye tamasha la Jembe mjini Mwanza. Mr. Blu akirap nyimbo zake zilizompa umaarufu kwenye tamasha la Jembe lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Diamond Platnumz na vijana wake wakishambulia jukwaa kwenye tamasha la Jembe lililofanyika kwenye viwanja vya CCM Kirumba mjini Mwanza. Mgeni rasmi wa tamasha la muziki la Jembe , Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM Dk. Sebastian Ndege kwenye chumba maalum nyuma ya jukwaa ,CCM Kirumba . BOFYA HAPA KWA PI

JE, UNA HERUFI M KATIKA KIGANJA CHAKO? HII NDIO MAANA YAKE

Image
Watu wengi wanasema, mistari katika viganja vya kila binadamu vimebeba mambo mengi na maana nyingi kuhusu tabia yako na hatima yako kwa ujumla. Pia inasemekana watu wenye herufi 'M' katika viganja vyao,ni watu wa aina muhimu sana.Inasemekana watu hawa wana sifa za ajabu.Wana ushirikiano mzuri na wafanyakazi katika aina yeyote ile ya biashara. Kama una mpenzi mwenye alama 'M' katika kiganja chake,basi yakupasa kujua yupo makini katika uhusiano wenu.Hakuna utani,hakuna uongo na hakuna udanganyifu. Watu wenye herufi 'M' katika viganja vyao, wana uwezo mkubwa wa kufanya mabadiliko katika maisha yao na daima utumia vizuri fursa wanazozipata katika maisha yao. Imekuwa ikijulikana kwa watu wa zamani, kwamba manabii wote walikuwa na alama hii katika mikono yao. Angalia mkoni wako na endapo ukijikuta una alama ya 'M' basi tambua kwamba wewe ni mtu maalamu

Kumbukumbu ya Kuzama kwa Meli ya MV Bukoba Mei 21, 1996

Image
Meli ya MV Bukoba ikwa Ziwa Victoria wakati ilipokuwa ikitoa huduma ya usafirishaji kabla ya kuzama. KIUKWELI tarehe kama ya leo miaka 20 iliyopita haitoweza kusahaulika kirahisi kwenye mioyo ya Watanzania na Ulimwenguni kote, kwani usiku wa kuamkia Mei 21, 1996, meli ya MV Victoria ikiwa na abiria kati ya 750 na 800 pamoja na wafanyakazi 37 ilizama majini kwenye Ziwa Victoria mwambao wa Bwiru Jijini Mwanza ambapo ilikuwa takribani kilomita 30 kufika nchi kavu. Meli ya Mv Bukoba ikiwa inazama. Ripoti ya Tume ya Jaji Robert Kisanga, iliyochunguza chanzo cha hiyo ilieleza kuwa, kati ya hao, 114 waliokolewa wakiwa hai; wakati 391 waliopolewa wakiwa wamefariki na kuzikwa katika makaburi ya Igoma barabara ya Musoma, nje kidogo ya Jiji la Mwanza. Miili mingine ilichukuliwa na jamaa kuzikwa kwao. Jumla ya miili 332 haikupatikana. Kila mwaka, ifikapo Mei 21, viongozi wa dini, wa serikali na wananchi huongozana kwenda eneo la ajali kufanya kumbukumbu. Mnara wa Kumb

WAZIRI MKUU AFAFANUA KUHUSU KUTENGULIWA KWA UTEUZI WA WAZIRI KITWANGA

Image
Mh. Charles Kitwanga aliekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Charles Kitwanga umefuata kanuni za utumishi wa umma ambao unakataza mtumishi kulewa akiwa kazini.  “Zipo sheria za utumishi ambazo mtumishi hatakiwi kunywa pombe na wala hapaswi kulewa akiwa kazini… mtumishi anapaswa kuwa na akili timamu inayokuwezesha kufanya kazi za Serikali,” alisema.  Ametoa ufafanuzi leo usiku (Ijumaa, Mei 20, 2016) wakati akijibu swali la mwandishi wa TBC1aliyetaka kujua kama taarifa zilizoenea kuhusu kutenguliwa kwa Waziri huyo ni za kweli.  “Ni kweli Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Charles Kitwanga kuanzia leo tarehe 20 Mei, 2016 baada ya kuonekana amelewa wakati wa kazi. Na hili lilibainika pale alipokuwa akijibu maswali ya wizara yake leo asubuhi,” alisema Waziri Mkuu.  Waziri

Tanzia: Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar, Wilson Kabwe Afariki Dunia

Image
  Marehemu Wilson Kabwe. ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe amefariki usiku wa kuamkia leo nchini India alikokuwa ameenda kutibiwa. Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amethibitisha kutokea kwa msiba huo. Rais John Pombe Magufuli, Aprili 19 alimsimamisha kazi Bw. Wilson Kabwe kutokana na ufisadi katika utekelezwaji wa mikataba mitatu, inayohusu maeneo ya ukusanyaji mapato ya Stendi Kuu ya Mabasi Yaendayo Mikoani ya Ubungo na kodi ya uegeshaji magari katikati ya jiji na  kuisababishia  serikali  hasara  ya  pesa zaidi ya bilioni 3. Rais Magufuli alichukukua uamuzi huo siku ya uzinduzi wa daraja la Kigamboni, ambapo kabla ya Rais kuhutubia, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda alitoa hotuba fupi ya maswala kadhaa ya Mkoa wa Dar es Salaam  ikiwemo  ripoti ya tume aliyounda  kuchunguza utekelezwaji wa mikataba hiyo. Kabla ya kuhamishiwa jijini Dar es Salaam, Kabwe alikuwa ni Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza ambaye alih

A-Z Shoo ya Jide Mlimani City

Image
Malkia wa Bongo Fleva, Lady Jay Dee usiku huu amefunika vilivyo katika shoo yake ya Nasimama Tena iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City. Staa huyo akiwa na vijana wake wamepiga shoo kali ya Live iliyochukua saa tatu na kuzikonga vilivyo nyoyo za mashabiki walioshindwa kujizuia kukaa kwenye viti vyao na kunyanyuka mara kwa mara kwenda stejini kucheza nyimbo mbalimbali za malkia huyo. Shoo hiyo imehudhuriwa na mastaa kibao wa Bongo Fleva na Bongo Movies wakiwemo Alikiba, Idrisa Sultan, Wema Sepetu, Elizabeth Michael na wengineo kibao. Usikose kuangalia Global TV Online kuona video za matukio yote yaliyojiri. Picha: Clarence Mulisa, Gabriel Ng’osha na Rishard Bukos / GPL

MATUKIO YA BUNGENI LEO.

Image
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akibadilishana mawazo na na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwa(kulia) jana mjini Dodoma wakati wa mapumziko ya mchana ya kikao cha Bunge.   Afisa Habari wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Patson Sobha(aliyenyosha mkono) akitoa maelezo kwa wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dodoma walitembelea Bunge kama sehemu ya mafunzo jana mjini Dodoma.  Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe. Dkt. Dalaly Kafumu(kushoto) akibadilishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la Simanjirio Mhe. James Ole Milya(wa pili kushoto), Mbunge wa Tarime Vijijini Mhe.John Heche(wa pili kulia) na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwa(kulia) jana mjini Dodoma wakati wa mapumziko ya mchana ya kikao cha Bunge.  Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akibadilishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la Kilolo Mhe Venance Mwamoto(kushoto) jana mjini Dodoma wakati wa mapumziko ya mchana ya kikao cha Bunge. Picha na Ti

Sakata la Mauaji Msikitini Mwanza: Kundi la Kigaidi la ISIS lahusishwa

Image
YADAIWA ni kisasi baada ya Polisi kuwakamata wanaharakati wa IS saa 24 kabla. "baada ya swala kumalizika, watu hao waliingia na kuwaamuru kulala chini huku wakitoa bendera nyeusi na maandishi ya meupe ya Kiarabu kisha kumtaka Imamu wa msikiti kujitokeza mbele, bendera hiyo ni kama ile inayotumiwa na kundi la kigaidi la IS" "Imamu alipojitokeza huku tukiwa tumelala chini, watu hao walisikika wakisema 'Kwa nini mnaswali wakati wenzetu wamekamatwa na polisi, wengine wanapigana 'jihad'...hali hiyo ilitushtua zaidi baada ya Imamu kuanza kuchinjwa kwa panga," "Ghafla wakatuamuru kulala kifudifudi na kudai wao ni IS wamekuja kufanya kazi yao, kisha wakaanza kutushambulia na kujeruhi. Mwenzangu niliyekuwa naye pembeni alikatwa panga na kuangukia juu yangu, hali hiyo ilinifanya nionekane kama nimekufa," Habari za uhakika ambazo Nipashe imezipata zinasema. Imam huyo na wafuasi wake, waliuwawa na kundi la watu wanane waliokuwa na bu

SAKATA LA ESCROW, IPTL LAIBUKA UPYA BUNGENI

Image
Kambi ya upinzani imeliibua upya bungeni sakata la Escrow, Richmond na umiliki wa kampuni ya IPTL, huku ikihoji sababu za Rais John Magufuli kutoheshimu maazimio ya Bunge ya kumwajibisha Sospeter Muhongo, badala yake kumteua tena kuwa Waziri wa Nishati na Madini. Hoja hizo ziliibuliwa na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika wakati akiwasilisha maoni ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2015/16 na makadirio ya matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2016/17. Muhongo alikuwa akiiongoza wizara hiyo wakati kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh300 bilioni kutoka kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa kuhifadhi fedha za malipo umeme kusubiri kumalizika kwa mzozo wa kimkataba baina ya kampuni ya IPTL, inayozalisha umeme na Shirika la Umeme (Tanesco). Bunge lilimuona Profesa Muhongo kuwa alishindwa kuwajibika na kusababisha Serikali kupoteza mapato. Profesa Muhongo alilazimika kujiuzulu wadhifa huo saa chache kabla ya Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwet