Kauli ya Louis van Gaal baada ya Ubingwa wa Kombe la FA kwa Man United


Baada ya kufanikiwa kutwaa Kombe la FA akiwa na Man United, Louis van Gaal amezungumza kauli ya kujivunia, licha ya kuwa kibarua chake kipo mashakani kuchukuliwa na Jose Mourinho kwa siku za usoni, licha ya kuwa mchana wa May 21 2016 ulianza kwa headlines zisizo njema kwake.
Van Gaal ameripotiwa na Metro na AS kuwa atafukuzwa na Man United nafasi yake kuchukuliwa na Jose Mourinho, hiyo ilikuwa ni saa kadhaa kabla ya BBC na Sky Sports kuziongezea nguvu taarifa hizo, kwa kuripoti habari kama hizo katika tovuti zao.
Louis van Gaal amekuwa akiandamwa na tetesi zinazohusu hatma ya kibarua chake, aliongea kauli zya kujivunia kama hana hofu na habari zinazoendelea.‘Hii ni furaha kubwa kwa klabu na mashabiki na kwangu pia ambaye nimefanikiwa kushinda taji hili nikiwa katika nchi nne tofauti ni makocha wachache wanaoweza kujivunia hilo, hivyo nina furaha sana na jambo hili”

Comments

Popular posts from this blog