Samatta hajakubali kuona rekodi ya Tanzania ikivunjwa na Chad mikononi mwake
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars March 23 imeshuka katika dimba la Idriss Mahamat kucheza na wenyeji wao timu ya taifa ya Chad katika muendelezo wa michezo ya makundi ya kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika (AFCON) itakayochezwa mwaka 2017. Huu ulikuwa ndio mchezo wa kwanza wa Mbwana Samatta akiichezea Taifa Stars kama nahodha wa timu hiyo, katika mchezo huo uliochezwa Chad , Taifa Stars imeibuka na ushindi wa goli 1-0, goli la Taifa Stars lilifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 30, baada ya kutumia vyema krosi ya Farid Musa . Samatta amefanikiwa kuitunzia Tanzania rekodi dhidi ya Chad , kwani mara ya mwisho Taifa Stars alikutana na Chad , ugenini na kufanikiwa kuibuka kwa ushindi wa goli 2-1. Magoli ya Taifa Stars wakati huo yalifungwa na Mrisho Ngassa dakika ya 11 na Nurdin Bakari dakika ya 88, huku goli la Chad la kufutia machozi lilifungwa na Mahamat Labbo dakika ya 12. Taifa Stars itarudiana na Chad Jumatatu ya March 28 uwa