Updates: Uchaguzi wa Meya Jiji la Dar

1
Mh. Edward Lowassa na Godbless Lema wakiwasili Ukumbi wa Karimjee kunakofanyika uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es salaam leo. x
Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt Vincent Mashinji (aliyesimama katikati) na Makamu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalim (wa kwanza kutosho) na baadhi ya wajumbe wakiwa nje ya Ukumbi wa Karimjee ambapo wamefika kufuatilia uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es salaam
xx
Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt Vincent Mashinji wa kwanza kushoto akijadiliana jambo na baadhi ya wajumbe.
xxx
Maofisa wanaosimamia uchaguzi huo wakikagua taarifa za wajumbe wanaositahili kuingia ukumbini kwa ajili ya kumchagua Meya wa Jiji la Dar.wajumbe
Hali ilivyo ndani ya Ukumbi wa Karimjee ambapo uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam unafanyika.
Baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuamuru uchaguzi wa Meya na Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, kufanyika leo kama ilivyopangwa. Baadhi ya wajumbe wanaoshiriki uchaguzi huo wamefika ukumbini Karimjee ambapo uchaguzi huo unafanyika.
Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sarah Yohana alitangaza na kutoa barua kwa wajumbe husika juu ya wito wa kikao cha Baraza la Madiwani kitakachokuwa na ajenda ya uchaguzi akisema wajumbe 163 watashiriki kupiga kura, kati yao 87 ni kutoka Ukawa na 76 CCM.
Wagombea  wanaowania kiti cha  Umeya wa Dar ni, Yenga Yusufu Omary (CCM )  na Isaya Mwita Charles (Chadema).

Comments

Popular posts from this blog