Mume amfunga mkewe mtini kisa kutopata mimba
Jeni Marwa akiwa amefungwa kamba mtini na mumewe. Stori: Gregory Nyankaira, UWAZI MARA: Nyango Hakimu mwenye umri wa miaka 37, anatafutwa na polisi akidaiwa kumfunga mkewe Jeni Marwa (23) kwenye mti na kumpa kichapo kilichomsababishia majeraha kwa madai ya kutoshika ujauzito kwenye ndoa yao. Tukio hilo lilitokea jioni ya Februari 6, mwaka huu katika Kijiji cha Singu, kilichopo Kata ya Kukirango wilayani Butiama mkoani Mara, ambako mwanamke huyo alipigwa kwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake, akidaiwa kutokuwa na faida nyumbani hapo. Mashuhuda wa tukio hilo wamesema, baada ya mumewe kumfunga mkewe kamba mikononi na miguuni kabla ya kumfunga kwenye mti na kuanza kumchapa, mwanamke huyo alipiga mayowe ya kuomba msaada ndipo watu walifika na kumkuta akitokwa damu nyingi baada ya kukatwa na kisu mguuni. Huku mumewe akiwa amekimbilia kusikojulikana, wasamaria wema walimchukua na kumpeleka Kituo cha Polisi cha Kiabakari ambako alipewa fomu ya matibabu (PF3) kabla ya...