Posts

FAHAMU HUU UMUHIMU WA MASSAGE KWA MWILI WAKO

Image
Je, kuna siku umewahi kuamka asubuhi na kujikuta ukiwa mchovu sana kupita kiasi? hivi ulihisi nini baada ya kuamka hivyo? Je, ulihisi una kahoma kidogo? au uliwaza huenda ni uchovu wa kazi za jana yake? naamini kuna mengi ulijiuliza na huenda hukupata jibu la uhakika. Kwa kawaida huwa kuna sababu nyingi za mtu kuamka akiwa mchovu wa mwili, miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na uchovu wa kazi, michezo n.k. Lakini unaweza kuepukana na hili suala la kuamka na uchovu endapo tu utajenga utaratibu wa kupata huduma ya kukandwa ( massage ) mwili kila baada ya muda fulani. Huduma hii ni vyema ukafanyiwa na mwezi (mke au mume) wako nyumbani ikiwa unahitaji kufanya kwa lengo la kuweka mwili wako sawa  sawa tu. Mtaalam wa masuala ya 'massage' kutoka Mandai Herbalist Clinic Mathayo Masinema Bahebe anasema kuwa massage husaidia kupunguza na kuondoa maumivu yote ya mwili pamoja na kurekebisha mzunguko wa damu mwilini na kuweka sawa sehemu zote za maungio ya mifupa ...

TONTO DIKEH AOLEWA, ABADILI JINA INSTAGRAM

Image
Muigizaji kiwango kutoka Nigeria, Tonto Dikeh. Lagos ,NIgeria MUIGIZAJI kiwango kutoka Nigeria, Tonto Dikeh ameolewa rasmi na aliyekuwa mpenzi wake, Churchill Olakunle Oladunni wiki iliyopita.Tarifa za kuolewa zilianza kuzagaa mapema wiki iliyopita baada ya staa huyo kubadili jina lake kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram na kujiita, Mrs Tonto Wigo Dikeh-Churchill. Lakini wikiendi iliyopita zilizagaa picha mitandaoni zikimuonyesha staa huyo akiwa na mumewe huyo mpya lakini kubwa zaidi ni ile ambayo amepiga na bibi yake wakiwa wanapongezwa kwenye sherehe hiyo. Tayari inadaiwa kuwa Tonto ni mjamzito na bibi yake huyo ameonekana kuumia zaidi baada ya kudai kuwa anamuacha peke yake kwani alizoea kuishi naye lakini amemtakia maisha mema na mumewe huyo.

BREAKING NEWZZ..BAADA YA KAMATI KUU CCM KUFUTA MATOKEO MAJIMBO MATANO,HII NDIYO KAULI NZITO YA MEYA JERRY SILAA WA UKONGA

Image
Mungu hamtupi mtu mwenye dhamira ya kweli, hawezi shindwa hawezi kata tamaa... Wana CCM jimbo la Ukonga tukutane kwenye matawi ya CCM kesho kutwa tarehe 13 tuchague Mbunge wa CCM tunayemtaka NINI MAONI YAKO NDUGU

KAMATI KUU YA CCM LEO MJINI DODOMA

Image
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua kikao cha Kamati Kuu ya CCM, leo Agosti, 11, 2015 katika ukumbi wa Jengo la White House Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.     Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, leo Agosti, 11, 2015 katika ukumbi wa Jengo la White House Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.    Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Steven Wasira na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Adam Kimbisa wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo mjini Dodoma.   Wajumbe wa Kamati Kuu, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Adam Kimbisa na Dk. Emmanuel Nchimbi, wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo mjini Dodoma.   Wajumbe wa Kamati Kuu, Dk. Maua Daftari na Samia Suluhu Hassan, ...

Wema Aibu mpya! Anaswa na mwanaume hotelini

Image
Wem Sepetu ‘Madam’ akidendeka na mwanaume  mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakiwa kwenye Mgahawa wa hoteli  iliyopo Msasani jijini Dar. Mwandishi wetu Licha ya kudai kwamba skendo za ngono sasa basi, staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amekwaa aibu mpya baada ya picha zake kunaswa akiwa na mwanaume mwingine kwa mara nyingine, mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakiwa kwenye Mgahawa wa hoteli iliyotajwa kwa jina la Cape-town Fish Market iliyopo Msasani jijini Dar. Wakiendelea kufanya yao. MADAI MAZITO Chanzo chetu ambacho ni makini kilipenyeza kuwa, katika tukio hilo la hivi karibuni, staa huyo alikuwa hafahamiani na mwanaume huyo, lakini kuna kijana mmoja ambaye mara nyingi anawakuwadia mastaa wa Bongo kwa matajiri, alidaiwa kumtonya Wema kuwa kuna ‘mchati’ anataka kutoka naye. Kilifunguka kwamba, baada ya Wema kung’atwa sikio juu ya Mkongomani ambaye ana ‘hela chafu’, alidaiwa kuo...

MWENYEKITI WA CHADEMA AONGEA NA WAANDISHI WA HABARI KUELEZEA AFYA YAKE

Image
  Mbowe akiongea na Waandishi wa habari leo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mwenyekiti mwenza wa UKAWA Freeman Mbowe, ameongea na vyombo vya habari na Kuelezea maendeleo yake kiafya baada ya jana kuugua gafla na kukimbizwa Hospitali.  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Unamuwaza kila wakati, hakuwazi kabisa, wa nini?

Image
NAMSHUKURU Mungu kwa kunikutanisha na wewe msomaji wangu katika safu hii, hakika yeye ni mwema na ametujalia uzima ili na wewe uweze kupata kusoma kile ambacho nimekuandalia siku ya leo. Mapenzi ni dawa. Mapenzi yanatupa furaha, yanatingisha dunia. Hakuna kitu kizuri kama kupendwa. Umpate mtu akupende na wewe umpende. Dunia yote mnaiona ni ya kwenu. Pamoja na kuwa matamu, wakati mwingine hugeuka shubiri. Yanakuwa machungu pale mmoja wenu anapokuwa hampendi mwenzake sawasawa na anavyopendwa. Mmoja anapokuwa anampenda mwenzake wakati anayependwa harudishi upendo, penzi haliwezi kuwa na uhai mrefu. Linaweza kulazimishwa kwa sababu fulani lakini mwisho wa siku ukweli unabaki palepale. Naam! Hapo ndipo kwenye kiini cha mada yangu ya leo. Ambaye anapendwa ataleta visa ili mradi tu muachane, atafanya hivyo kwa sababu hakupendi. Yupo ampendaye. Si wewe. Wewe anakufanya wa akiba au maslahi fulani. Unayempenda anaweza kukudanganya. Akajifanya anakupenda kumbe hakupendi....

WEMA SEPETU AELEZA ‘MAHABA’ YAKE KWA JANUARY MAKAMBA!

Image
Brighton Masalu MTOTO ‘laini’ kunako tasnia ya urembo na filamu Bongo, Wema Sepetu ameeleza kwa hisia kali jinsi anavyompenda Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Mhe. January Makamba katika utendaji kazi wake. Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, mbele ya naibu waziri huyo, Wema alisema miongoni mwa viongozi ambao humyima usingizi katika kuliongoza taifa hili kwa weredi mkubwa ni pamoja na Makamba. “Yeah, kusema ukweli nampenda sana Makamba, hakika ananivutia kwa mengi, hususan utendaji kazi wake,” alisema Wema.

BREAKING NEWS : MWENYEKITI WA CCM MKOA WA DODOMA ADAM KIMBISA ABWAGA MANYANGA.

Image
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Ndg. Adam Kimbisa, aachia ngazi. Amedai kuwa anataka kumpumzika siasa ila wadadisi wa mambo wanasema ni maandalizi ya kuja UKAWA.  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

BREAKING NEWZZ, JESHI LA POLISI LAKANUSHA TAARIFA ZA KUPIGA MARUFUKU MSAFARA WA LOWASSA, SOMA HAPA WALICHOSEMA

Image
  Kamanda Kova asubuhi ya leo akiongea na ITV amekanusha taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo whatssap kuwa watu wasiokuwa na shughuli mjini wasiingie kwa sababu mgombea wa CHADEMA atakuwa anachukua fomu na foleni itakuwa kubwa pia itahusisha magari, pikipiki, guta, baiskeli na helikopta na wameweka jina langu, pili amesema maandamano yataanzia makao makuu ya CUF Ilala saa tatu asubuhi, njia waliyoandaa jeshi la polisi ya kiusalama itaanzia UFIPA, Kinondoni kupitia Salender Bridge kuelekea ofisi za NEC. Amewaambia wananchi waje mjini kama kawaida kwa sababu wengine rizki yao inategemea kuamka kwake na kujishughulisha asubuhi mpaka jioni na ukiwaachia tu watu kwa ajili ya kuchukua fomu itakuwa tatizo. Tunachukua fursa hii kukanusha haya maelezo sio ya kwetu hata jinsi jinsi tangazo sio namna yetu ya kuandika taarifa na watu waache kupotesha watu kupitia mitandao kwa sababu masuala ya kiusalama ni nyeti sana. Maandamano ni kitu sisi Polisi tunara...

Batuli aeleza sababu za kutoolewa.

Image
Yobnes Yusuph ‘Batuli’. Brighton Masalu STAA wa filamu Bongo, Yobnes Yusuph ‘Batuli’, ameeleza sababu zinazochangia yeye kutoolewa kuwa ni umaarufu wake. Akizungumza na mwandishi wetu pande za Mlimani City jijini, alisema kuwa wanaume wamekuwa wakiwahofia kwa sababu wao ni mastaa kama wengi wanavyoamini ukimuoa staa umeumia.“Natamani sana kuolewa ila wanaume ndiyo tatizo, wanatuhofia sisi mastaa, nawaambia wasiwe na hofu na mimi kwani nimetokea kwenye familia bora ambayo imenilea vyema,” alisema Batuli.

MAELFU YA WANACHAMA WA CUF WAJITOKEZA KUMLAKI LOWASSA BUGURUNI LEO, ANGALIA PICHA HAPA

Image
 

Mtoto wa zari amliza Diamond.

Image
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, akiwa na mtoto wake P rincess Tiffah . Musa mateja na imelda mtema HII ni kali! Muda mchache baada ya mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kujifungua salama, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, amejifungia chemba kisha kuangua kilio akisema Mungu ni mwema huku akiwataja waliowahi kuwa wapenzi wake, Penniel Mungilwa ‘Penny’ na Jokate Mwegelo kwa maneno yao ya shombo. Mama yake Diamond Platnumz, Sanura Kassim ‘Sandra’ akiwa na mjukuu wake wakiwa na Zari baada ya kujifungua. TUJIUNGE AGA KHAN Tukio la kujifungua mchumba wa Diamond, Zari lilijiri Agosti 6, mwaka huu mishale ya saa 10:40 alfajiri katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar  ambapo alipelekwa usiku huo baada ya kujisikia uchungu ambapo alijifungua mtoto huyo wa kike. Chanzo cha habari kilieleza kwamba, siku hiyo, wakiwa hospitalini hapo, muda mfupi tu baada ya Diamond kuambiwa kuwa tayari Zari amejifungua, ...

SKAINA: WAOMBA RUSHWA YA NGONO WAMENIKATISHA TAMAA!

Image
BRIGHTON MASALU SKYNER Ally ‘Skaina’ amekiri kukutana na changamoto ya kuombwa rushwa ya ngono na baadhi ya wazalishaji wa filamu (producers), ili aweze kuonekana kwenye filamu mbalimbali, jambo ambalo anakiri kumkatisha tamaa katika safari yake ya kufika mbali kisanii. ....Soma zaidi====> http://bit.ly/1KWNriy

MAGUFULI ASEMA YEYE NI MUUMINI WA MISINGI IMARA YA CCM

Image
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ally Mtopa akisalimiana na Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli nje ya ofisi ya CCM mkoa wa Lindi  Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kutoka Wilaya ya Lindi ,Mama Salma Kikwete mara baada ya kuwasli  kwenye ofisi za CCM mkoa wa Lindi.  Mgombea wa Urais kwa kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi Ally Mchumo mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za CCM mkoa wa Lindi. Mgombea wa Urais kupitia CCM ,Dk.John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana mkoa wa Lindi Ndugu Amiri Mkalipa wakati wa mapokezi nje ya ofisi za CCM mkoa wa Lindi.    Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mchumi wa CCM mkoa wa Lindi Ndugu Kassim Abdallah.  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Magufuli akisalimiana na...