WEMA SEPETU AELEZA ‘MAHABA’ YAKE KWA JANUARY MAKAMBA!

Brighton Masalu
MTOTO ‘laini’ kunako tasnia ya urembo na filamu Bongo, Wema Sepetu ameeleza kwa hisia kali jinsi anavyompenda Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Mhe. January Makamba katika utendaji kazi wake.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, mbele ya naibu waziri huyo, Wema alisema miongoni mwa viongozi ambao humyima usingizi katika kuliongoza taifa hili kwa weredi mkubwa ni pamoja na Makamba.“Yeah, kusema ukweli nampenda sana Makamba, hakika ananivutia kwa mengi, hususan utendaji kazi wake,” alisema Wema.

Comments

Popular posts from this blog