Unamuwaza kila wakati, hakuwazi kabisa, wa nini?
NAMSHUKURU Mungu kwa kunikutanisha na wewe msomaji wangu katika safu hii, hakika yeye ni mwema na ametujalia uzima ili na wewe uweze kupata kusoma kile ambacho nimekuandalia siku ya leo. Mapenzi ni dawa. Mapenzi yanatupa furaha, yanatingisha dunia. Hakuna kitu kizuri kama kupendwa. Umpate mtu akupende na wewe umpende. Dunia yote mnaiona ni ya kwenu. Pamoja na kuwa matamu, wakati mwingine hugeuka shubiri. Yanakuwa machungu pale mmoja wenu anapokuwa hampendi mwenzake sawasawa na anavyopendwa. Mmoja anapokuwa anampenda mwenzake wakati anayependwa harudishi upendo, penzi haliwezi kuwa na uhai mrefu. Linaweza kulazimishwa kwa sababu fulani lakini mwisho wa siku ukweli unabaki palepale. Naam! Hapo ndipo kwenye kiini cha mada yangu ya leo. Ambaye anapendwa ataleta visa ili mradi tu muachane, atafanya hivyo kwa sababu hakupendi. Yupo ampendaye. Si wewe. Wewe anakufanya wa akiba au maslahi fulani. Unayempenda anaweza kukudanganya. Akajifanya anakupenda kumbe hakupendi....