Posts

URAIS CCM KAZI IPO

Image

LOWASSA AZIDI KUVUNJA REKODI YA WADHAMINI, APATA 9516 MKOANI TABORA LEO

Image
Waziri Mkuu wa Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wana CCM waliofika kumdhamini pamoja na wananchi wengine, kwenye viwanja vya ofisi za CCM Tabora Mjini, leo Juni 12, 2015. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wana CCM 9516 kwa mkoani Tabora, ikiwa ni muendelezo safari yake ya kutafuta wana CCM wa kumdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi kimteue kuwania nafasi ya urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI. Waziri Mkuu wa Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akipokea majina kutoka kwa Naibu Katibu wa CCM Wilaya ya Tabora Mjini, Bi. Hidaya Rashid yenye idadi wanachama wa CCM 9516 waliomdhamini ili aweze kuteuliwa na Chama kuwania Urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Waziri Mkuu wa Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akizungumza na WanaCCM waliofika kumdhani pamoja na wananchi wa Mj

WAZIRI BERNARD MEMBE ANUSURIKA AJALI YA NDEGE, ZANZIBAR

Image
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (pichani) , amenusurika kifo baada ya ndege aliyokuwa akisafiria kutoka Iringa kwenda Zanzibar kutaka kugongana uso kwa uso na ndege nyingine dakika moja kabla ya kutua. Waziri Membe akiwa na ujumbe wake wa watu wanane, walikuwa wakisafiria ndege ya kukodi kampuni ya 5H NEG Precition Aviation ikirushwa na rubani Mathew Mhahiki, ambaye ameonyesha kushangazwa na tukio hilo alilodai “ni kwa rehema za Mungu tumepona ajali hii.”  Akizungumza na mwandishi wetu aliyeko katika ziara yake, rubani Mhahiki alisema: “Lazima kuna tatizo katika control center hata hivyo tayari nimeongea nao na wameniomba samahani na kudai walipitiwa, maana kwa hali ilivyokuwa ni kwamba tungegongana wakati wa kutua maana nimeshangaa tu kuona ndege hii hapa ndiyo maana nikaamua kumkwepa mwenzangu nikapanda juu.” Waziri Membe alisema: “Nina uzoefu mkubwa wa kusafiri na ndege mahali pengi d

JINSI SITTI MTEMVU ALIVYOYABADILISHA MAUMIVU YA SIKU 30 KUWA BIASHARA

Image
Aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Uingereza kuanzia mwaka 1940 hadi 1945 na kisha kurejea tena mwaka 1951 hadi 1955, Winston Churchill aliwahi kusema, “a pessimist sees the difficulty in every opportunity; an optimist sees the opportunity in every difficulty.” Alimaanisha kuwa “mtu muoga huona ugumu kwenye kila fursa na mtu jasiri huona fursa kwenye kila ugumu.” 2014 ulikuwa ni mwaka wenye majaribu na mitihani mingi kwa Sitti Mtemvu. Mara tu baada ya kushinda taji la Miss Tanzania 2014, skendo moja baada ya nyingine zikaanza kuibuka. Kubwa lilikuwa ni kitendo chake cha kudaiwa kudanganya umri na kuwasilisha cheti cha kuzaliwa ‘feki.’ Pia watu wakazusha kuwa mrembo huyo ana mtoto, kitu ambacho ni kinyume cha vigezo vya shindano hilo lililofungiwa mwaka jana. Sitti alijikuta kwenye kitimoto. Jina lake likavuma mitaani, kwenye vyombo vya habari na zaidi kwenye mitandao ya kijamii. Habari yake ya kudanganya umri ikawa kubwa kuliko ushindi wenyewe wa taji hilo. Watu

WASHINDI TUZO ZA KILI KUANIKWA KESHO

Image
Meneja wa Kilimanjaro ,Pamela Kikuli akizungumza na wanahabari (hawapo)pichani. Wanahabari wakichukua tukio. WASHINDI wa Kilimanjaro Music Awards 2015 (KTMA) wanatarajiwa kuanikwa kesho ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar. Akizungumza na waandishi wa habari leo, Meneja wa Kilimanjaro, Pamela Kikuli amesema kuwa washindi waliopatikana katika Promosheni za Bia ya Kilimanjaro zilizofanyika nchini kote wameanza kuwasili jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo kushuhudia Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards. “Hafla ya kukabidhi tuzo hizi inategemewa kufanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam kesho Jumamosi na jumla ya washindi 22 wanatarajiwa kuwasili leo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania ambapo washindi hawa wataungana na washindi wengine wanne wa hapa Dar es Salaam,” alisema Kikuli. Bi. Pamela aliongeza kuwa washindi hao waliochaguliwa kwa njia ya kuponi baada wanywaji kununua bia ya Kilimanjaro kwenye Bar zilizokuwa na Promosheni watalipiwa

OFFICIAL : MAN UNITED YAKAMILISHA USAJILI WA MEMPHIS DEPAY NA KUMPA JEZI

Image
Klabu ya Manchester United imetangaza  rasmi kukamilisha usajili wa nyota wa kimataifa wa Uholanzi,  Memphis Depay na kumsainisha mkataba wa miaka minne. Mpango wa kumsajili kinda huyu mwenye miaka 21 ulikamilika mwezi uliopita, lakini sasa dili limekamilika rasmi ambapo United imelipa ada ya uhamisho ya  paundi milioni 25. Kiungo huyo anajiunga na Manchester United kutokea klabu ya PSV Einhoven ambapo alionesha kiwango cha juu kwenye ligi ya Uholanzi akifunga magoli 22 msimu uliopita. Kijana huyo pia ameonesha kiwango kizuri timu ya taifa na wiki iliyopita alicheza mpira mwingi mno Uholanzi ikifungwa 4-3 na Marekani. Memphis Depay anakuwa mchezaji wa kwanza  kusajiliwa rasmi na Man United majira haya ya kiangazi ambapo Louis van Gaal anatafuta wachezaji wa kuimarisha kikosi cha kushindania ubingwa msimu ujao.

DAKTARI: KAJALA HAWEZI KUZAA TENA!, KISA HIKI HAPA

Image
Imelda mtema MAJANGA juu ya majanga! Siku chache kufuatia kufanyiwa kipimo na kubainika kuna tatizo kwenye ubongo baada ya kupigwa chupa kichwani kwenye Klabu ya New Maisha, Masaki jijini Dar, mkali wa sinema za Bongo, Kajala Masanja ‘Kay’ amepata pigo lingine la daktari kumwambia hawezi kuzaa tena!   Mkali wa sinema za Bongo, Kajala Masanja ‘Kay’. Kwa mujibu wa chanzo makini, Kajala alipewa maelezo hayo mapema wiki hii baada ya kufanyiwa kipimo na daktari bingwa wa hospitali moja iliyopo maeneo ya Morocco jijini Dar. HISTORIA YA TATIZO Kwa mujibu wa chanzo hicho, awali staa huyo alikuwa akisumbuliwa na tatizo la maumivu makali ya tumbo kwa kipindi kirefu na mara kwa mara hali iliyomlazimu kwenda kwenye hospitali mbalimbali za jijini Dar na kutibiwa lakini bila mafanikio. “Unajua awali, aliamini amepata vidonda vya vitumbo (Ulcers). “Pamoja na kupewa dawa mbalimbali kama ‘antibiotic’ kama Amoxicillin, Tetracycline, Clarithromycin na Metronidazole, daw

UZINDUZI WA BONGO STAR SEARCH 2015 “JUKWAA LAKO- KUWA ORIGINAL”

Image
…akizindua awamu nyingine ya shindano la BSS kwa mwaka 2015. Kushoto ni Madam Rita, kabla ya uzinduzi akiwa na mmoja wa wadau, kulia ni mbunifu wa mitindo nchini Ally Remtullah. Mmoja wa washindi wa BSS mwaka 2013, Emmanuel Msuya akizungumza jambo na wanahabari (hawapo pichani). Baadhi wa waandishi wa habari wakifuatilia kipindi maalumu cha wasanii na washindi waliopita katika shindano la BSS, miaka ya nyuma. Sehemu ya waraka kwa Watanzania.

SOMA BAJETI YA MWAKA 2015/16 ILIYOWASILISHWA NA WAZIRI WA FEDHA BUNGENI LEO

Image
Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Salum Mkuya (MB) akiwasilisha bungeni Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2015/16, Mjini Dodoma leo. Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Salum Mkuya (Mb) akionyesha Begi la Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2015/16 wakati anawasili katika Viwanja vya Bunge, Mjini Dodoma leo. SOMA BAJETI YA MWAKA 2015/16 HAPA===>>> BAJETI

MAKAMBA AVUNJA REKODI YA MAPOKEZI NA UDHAMINI IRINGA

Image
Wanafunzi wa Iringa University wakimpokea Mhe. Makamba kwa shangwe na furaha huku wakiwa wameshika mabango Mbunge wa Bumbuli na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia anayeendelea kusaka udhamini wa wananchama wenzake  ili kuingia katika kinyang’anyiro cha Urais mapema Oktoba mwaka huu, Mheshimiwa January Makamba, leo amepokelewa kwa kishindo na wanachama wa CCM Mjini Iringa na kuvunja rekodi ya udhamini ukilinganisha na wagombea waliopita. Akiongea kabla ya kumkaribisha mtangaza nia huyo anayeonekana kuwa na mvuto wa aina yake kwa vijana, Katibu wa CCM wilaya ya Iringa Zongo Lobe Zongo amemtaja Mheshimiwa Makamba kuwa ni mgombea aliyevunja rekodi mkoani hapo baada ya kupata wadhamini 680 ukiachilia mbali mapokezi yenye msisimko mkubwa tofauti na wagombea waliotangulia. Akiwashukuru Mheshimiwa January Makamba, ambaye anaomba kupendekezwa na chama chake kugombea nafasi ya urais, alisema kwamba ameamua kugombea si kwa kubip bali anagombea kushinda, pia kwamba

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YATOA RATIBA KAMILI YA UANDIKISHAJI KWA MIKOA 15

Image

MTITU, STEVE NYERERE BIFU KALI WAAPA KUTOZIKANA!

Image
Msanii wa filamu Steven Mengere ‘Steve Nyerere’. Wakizungumza na Amani kwa nyakati tofauti juzi, wawili hao wameapa wasijuane kwa hali yoyote iwe kwa matatizo kama mmoja wao kufiwa au yeye kufariki dunia, basi mwingine asihudhurie msiba na mazishi. WASANII William Mtitu na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ wamejiapiza kuwa wasizikane ikitokea mmoja kati yao akafariki dunia huku chanzo ni kila mmoja kumtuhumu mwenzake kwa unafiki. Steve Nyerere, ndiye alikuwa wa kwanza ‘kuachama’ mbele ya gazeti hili ndani ya Viwanja vya Leaders, Dar kulikokuwa na kikao cha maandalizi ya sherehe ya harusi ya msanii mwenzao, Hadji Adam ‘Baba Haji’. “Hakuna mtu mnafiki kama Mtitu, sitaki kabisa hata kumsikia na kila nikimtazama najisikia vibaya mno, mkiwa pamoja anaonekana mwema lakini baada ya hapo anakuwa msaliti, kwanza hata nikifiwa sitaki kumuona msibani, nikifa mimi hakika asihudhurie mazishi yangu, naapa,” alisema Nyerere huku akimtazama mwandishi kwa jicho la ‘sitanii kaka’. Naye kwa u

TWO INMATES MADE A DARING AND CINEMATIC ESCAPE OVER THE WEEKEND FROM CLINTON CORRECTIONAL FACILITY

Image
Two inmates made a daring and cinematic escape over the weekend from Clinton Correctional Facility, the upstate prison known as “Little Siberia,” somehow obtaining the power tools necessary to carve their way out of their steel cells and into a large pipe leading to a street outside. The account below is based on statements from the New York State governor’s office and police officials. First, the inmates cut neat rectangular holes in the steel at the backs of their cells. They fashioned dummies from sweatshirts and stuffed their beds to thwart discovery during regular cell checks by guards. The inmates, both serving long terms for vicious murders, had adjoining cells. The rectangular holes can be seen in both walls from the catwalk behind the cells. Once inside the mechanical corridors of the prison, the men broke through a brick wall, made their way to a 24-inch drain pipe and cut a hole in it. They left a taunting note for the authorities that included a racist ca

MANGULA ATAJA VIGEZO 13 VYA MGOMBEA URAIS WA CCM..NI HIVI HAPA

Image
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Philip Mangula amesema vigezo 13, vitatumika kuwachuja wanachama wa chama hicho ambao wameomba kugombea urais CCM. Alisema hayo jana mjini hapa wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya CCM mjini Dodoma. Aliwakumbusha watangaza nia kuwa hawaruhusiwi kutoa rushwa, kushawishi au kushawishika kuwapa rushwa wale wanaowadhamini. Vigezo vyenyewe Alitaja vigezo 13 vitakavyotumika kuwachuja wagombea kuwa ni uwezo mkubwa na uzoefu katika uongozi, uadilifu, unyenyekevu na busara. Pia, kuwa na elimu ya chuo kikuu au inayolingana na hiyo, mtu mwenye upeo mkubwa wa kuimarisha na kuendeleza Muungano, umoja na amani. “Anatakiwa kuwa na upeo mkubwa usiotiliwa mashaka kuhusu masuala ya kimataifa, asiye na hulka ya kidikteta au mfashisti, awe tayari kulinda kanuni, sheria na utawala bora,” alisema Mangula. Alitaja vigezo vingine ni kuwa mtetezi wa wanyonge na haki za bin

TAZAMA HAMISA MOBETO AKIWA KWENYE UBORA WAKE BAADA YA KUJIFUNGUA HIVI KARIBUNI.. HUWEZI KUAMINI ALIVYOKUWA MCHARO

Image
WEKA MAONI YAKO HAPA

JOHARI: RAY NI KILA KITU KWANGU!

Image
Diva wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’. PATAMU hapo! Diva wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amesema msanii mwenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’ ndiye kila kitu maishani mwake kutokana na msaada aliompa wa kumtoa kisanii na kumsapoti kwa mambo mengi kikazi. ‘Akianika mwanya’ katika mazungumzo na Amani juzikati, Johari alisema haoni sababu ya kuficha ukweli kuwa bila Ray isingekuwa rahisi yeye kufika alipo kisanii hivyo lazima akumbuke kurudisha shukrani. Vincent Kigosi ‘Ray’. “Lazima niwe mkweli kuwa, Ray ni kila kitu kwangu, nipo hapa nilipo leo kwa sababu ya jitihada zake. Alikuwa mwalimu wangu wa sanaa tangu Kaole (kundi la sanaa), siyo mimi tu hata marehemu Kanumba (Steven) na wengine, hivyo siwezi kuacha kumrudishia shukrani zangu,” aliweka nukta Johari.

MR NICE AMWANDIKIA BARUA YA WAZI RAIS WA BURUNDI, PIERRE NKURUNZIZA..ISOME TU UMPE NA WEWE USHAURI

Image
Mr Nice amechukizwa na hatua za rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza ya kutangaza nia ya kuombea urais kwa awamu ya tatu kinyume na katiba hali ambayo imesababisha machafuko. Kupitia ukurasa wa Facebook, Mr Nice ameandika: NI MAONI BINAFSI TU WALA SIJASHAURIWA NA YOYOTE…Pierre wewe ni kaka yangu ki -umri,,,,,ki -elimu huenda na kii -,,,,tejilinsia pia …. ukiwa kama mzaliwa na damu ya mburundi toka ktk kabila lolote lile ama dini ama jinsia yoyote pale burundi nakuomba sana hebu jaribu kuona uchungu na masononeko ya watu wako walioamini kuwa wewe ndiye mkombozi wao toka ktk lindi la machafuko na umwagaji damu uliotukuka duniani…usiwakumbushie tena kule ulikowatoa na sasa unataka kuwarejesha tena huko ..kama nchi yako umeiweka vizuri hadi hapo ilipo kaka kwanini usipewe sifa za uliyoyafanya baada ya machafuko ya damu za watu muda mrefu na nchi yako kuwa na amani..ningeoenda nikuone ukiishi kwa amani na heshma iliyotukuka kama waliotangulia……nchi c y

ISIS WAMWUA MFUNGWA BAADA YA KUJICHIMBIA KABURI LAKE

Image
Mfungwa akichimba kaburi lake. ...Akiwa amepewa fursa ya kuongea na watu awatakao. Mfungwa (mguu wake ukionekana kushoto chini) akiwa ameanguka kaburini baada ya kuuawa. Muuaji akifukia mwili wa mfungwa aliyeuawa. MFUNGWA ambaye wapiganaji wa kundi la ISIS lilimtuhumu kuwa jasusi wa Israel (Mossad) hivi majuzi aliuawa kwa kupigwa risasi kichwani katika jangwa la Sinai, Misri. Kwa mujibu wa video zilizopatikana, mfungwa huyo anaonekana akiwa amesimama katika shimo akichimba kaburi lake, akapigwa risasi nyuma ya kichwa na kusukumiziwa katika kaburi hilo. ISIS wamesema mtu huyo alikuwa anafanya ujasusi na kuripoti kwa serikali ya Israel kuhusu shughuli za ISIS eneo hilo la Misri.