MTITU, STEVE NYERERE BIFU KALI WAAPA KUTOZIKANA!

Msanii wa filamu Steven Mengere ‘Steve Nyerere’. Wakizungumza na Amani kwa nyakati tofauti juzi, wawili hao wameapa wasijuane kwa hali yoyote iwe kwa matatizo kama mmoja wao kufiwa au yeye kufariki dunia, basi mwingine asihudhurie msiba na mazishi. WASANII William Mtitu na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ wamejiapiza kuwa wasizikane ikitokea mmoja kati yao akafariki dunia huku chanzo ni kila mmoja kumtuhumu mwenzake kwa unafiki.
Steve Nyerere, ndiye alikuwa wa kwanza ‘kuachama’ mbele ya gazeti hili ndani ya Viwanja vya Leaders, Dar kulikokuwa na kikao cha maandalizi ya sherehe ya harusi ya msanii mwenzao, Hadji Adam ‘Baba Haji’.

“Hakuna mtu mnafiki kama Mtitu, sitaki kabisa hata kumsikia na kila nikimtazama najisikia vibaya mno, mkiwa pamoja anaonekana mwema lakini baada ya hapo anakuwa msaliti, kwanza hata nikifiwa sitaki kumuona msibani, nikifa mimi hakika asihudhurie mazishi yangu, naapa,” alisema Nyerere huku akimtazama mwandishi kwa jicho la ‘sitanii kaka’.

Naye kwa upande wake, Mtitu aliposikia hayo alionekana kumpuuza Nyerere huku akimtolea maneno ya kejeli na dharau tele.

Msanii wa filamu William Mtitu. “Steve ni mtoto mdogo sana halafu hana elimu kichwani, ameingia kwenye sanaa tunamuona, hana jipya zaidi ya kujipendekeza kwa viongozi wa serikalini kwa kuwaomba hela. Atafute mtu wa kushindana naye. Hata mimi nikifa asikanyage msibani na kaburini kwangu, nitazikwa hata na mawe au wanyama,” alisema Mtitu kwa sauti iliyojaa jazba

Comments

Popular posts from this blog