Posts

Mfanyabiashara Afia Hotelini na Kete 30 za Heroin

Image
Mfanyabiashara wa dawa za kulevya, Kervin Mafita (40),mkazi wa Kinondoni, Dar es Salaam, amekutwa amekufa kwenye Hoteli  iliyopo jijini Arusha akiwa na shehena ya dawa hizo aina ya heroin tumboni mwake.   Meneja wa hoteli hiyo, Bw. Douglas Minja, alisema marehemu alifika hotelini hapo Aprili 12, mwaka huu, akiwa ameongozana na mama yake mzazi, mdogo wake na mtoto wake mwenye umri wa miaka 11 na kukodi vyumba viwili.   Alisema Aprili 15, mwaka huu, saa nne asubuhi, mhudumu wa hoteli alienda kugonga chumbani kwa marehemu ili aweze kufanya usafi na baada ya kufunguliwa mlango, ndani kulikuwa na marehemu, mama yake na mgodo wake marehemu.   Aliongeza kuwa, ndugu hao walidai muda huo walikuwa na mazungumzo hivyo hawakutaka usumbufu ambapo kutokana na majibu hayo, muhudumu huyo alilazimika kuwapisha ili waendelee na mazungumzo yao.   "Baada ya saa moja, ndugu wawili (mama na mdogo wa marehemu), walitoka na kutokomea kusikojulikana ila mtoto wak

CHAMA CHA TLP KIMEMPENDEKEZA MREMA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA VUNJO

Image
Mh. Augustine Mrema Kamati Kuu ya Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), imempendekeza Augustine Mrema ambae pia ni mwenyekiti wa chama hicho kutetea kiti chake cha ubunge katika jimbo la Vunjo. Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho Nancy Mrikaria, akiongea jana na gazeti la mwananchi alisema kuwa kamati hiyo pia imemthibitisha Mrema kuendelea na nafasi yake ya uenyekiti wa chama hicho kwa mara nyingine. Alisema kamati imeridhia Mrema kuendelea kugombea ubunge katika jimbo la Vunjo ikiwa na imani kuwa ana nafasi kubwa ya kushinda, ikilinganishwa na wengine waliotangaza nia ya kupambana nao. “Kamati imefikia hatua hiyo kwa kutambua uwezo alionao mwenyekiti katika kukiendeleza chama, pia hadi sasa hakuna mwanachama mwingine aliyejitokeza kugombea nafasi hiyo na tulianza kutoa fomu tangu Aprili 9 hadi 17, wakati kwenye nafasi ya makamu mwenyekiti Bara ndiyo kuna ushindani wa watu wawili wanaoigombea,” aliliambia gazet

MAYUNGA MSHINDI WA AIRTEL TRACE MUSIC STAR AFRIKA

Image
Nalimi Mayunga (katikati) akiwa amefurahi hadi akitaka kuanguka baada ya kutangazwa mshindi kwenye Shindano la Airtel Trace Music Star. Mayunga (kushoto) akiwa haamini kama jina lake ndio limetajwa ndiye mshindi wa shindano hilo.… Nalimi Mayunga (katikati) akiwa amefurahi hadi akitaka kuanguka baada ya kutangazwa mshindi kwenye Shindano la Airtel Trace Music Star. Mayunga (kushoto) akiwa haamini kama jina lake ndio limetajwa ndiye mshindi wa shindano hilo. Mayunga (katikati) akiwa na wadau mbalimbali akiwa ameshikilia tuzo yake. Mayunga akiimba. Watanzania wakishangilia baada ya Mayunga kuibuka mshindi. MTANZANIA Nalimi Mayunga ameshinda mkataba wa kurekodi muziki na Label ya Universal Music wenye thamani ya dola 500,000 ambayo ni shilingi milioni 900 kwenye Shindano la Africa Airtel Trace Star lililofanyika nchini Nairobi, Kenya Jumamosi iliyopita. Mayunga aliwashinda wasanii wengi kutoka nchi mbali

MAJAMBAZI WAUWA WAWILI NA KUPORA PESA ZA KAMPUNI YA BONITE MOSHI

Image
Mlinzi wa Kampuni ya Bonite, aliyetambulika kwa jina la Shamba baada ya kupigwa risasi na majambazi mjini Moshi. Dereva wa Kampuni ya Bonite aliyetambulika kwa jina moja la Mselemu mara baada ya kushambuliwa kwa risasi na majambazi. ...wakiwa kwenye gari baada ya kushambuliwa kwa risasi na… Mlinzi wa Kampuni ya Bonite, aliyetambulika kwa jina la Shamba baada ya kupigwa risasi na majambazi mjini Moshi. Dereva wa Kampuni ya Bonite aliyetambulika kwa jina moja la Mselemu mara baada ya kushambuliwa kwa risasi na majambazi. ...wakiwa kwenye gari baada ya kushambuliwa kwa risasi na majambazi. Mlinzi baada ya kuuawa na majambazi. MAJAMBAZI yaliyokuwa na silaha yamevamia gari mali ya Kampuni ya Bonite na kuwamiminia risasi dereva wa gari hilo aliyetambulika kwa jina moja la Mselemu na mlinzi wa Kampuni hiyo aliyetambulika kwa jina la Shamba kisha kupora fedha na kutokomea kusikojulikana. Tukio hilo limetokea jana mjini Moshi ambapo majambazi wanne waliokuwa kwenye pikipi
Image
Mohammed Mosri. Aliyekuwa Rais wa Misri, Mohammed Mosri amehukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani kwa kuwachochoea wafuasi wa kundi la Muslim Brotherhood kuwaua waandamanaji wa upinzani alipokuwa madarakani mwaka 2012.

TAARIFA ZAIDI TUKUO LA KUKAMATWA KWA MAGAIDI MOROGORO

Image
Polisi wakimjulia hali mwenzao aliyekatwa na sime shingoni. HII ndiyo A-Z ya wale watu tisa wanaoshikiliwa na polisi jijini Dar baada ya kukamatwa msikitini wakiwa na milipuko 30, sare za jeshi na bendera nyeusi inayodaiwa kutumiwa na kundi la wapiganaji wa Al Shabaab. Mmoja kati ya watu hao (wa kumi), Hamad Makweka aliuawa. Watu hao walikamatwa Aprili 14, mwaka huu saa 3:30 usiku katika Kitongoji cha Nyandero Tarafa ya Kidatu wilayani Kilombero, Morogoro wakiwa na silaha hizo ambapo ilidaiwa kuwa, walikuwa wakijiandaa kwenda kufanya uhalifu wa ‘kigaidi’ mahali. Ilidaiwa watu hao walilala kwenye Msikiti wa Answar Sunna uliopo Kidatu ambao unamilikiwa na Islamic Foundation. Baada ya kukamatwa, awali walishikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi, Morogoro na baadaye kupelekwa jijini Dar kwa siri ambako mahojiano makali yanaendelea. Habari kutoka ndani ya jeshi hilo zinasema kuwa, watu hao wanahojiwa ili kujua ukubwa wa mtandao wao, walikuwa wakafanye tukio wapi

UNYAMA WA KUTISHA DAR: WATOTO WACHOMWA MOTO HADI KUFA, KISA HAWARA WA BABA!

Image
Marehemu Jumanne Omar enzi za uhai wake. Tukio hilo la kinyama lilitokea wiki iliyopita Gongo la Mboto, Dar ambapo kijana aliyefahamika kwa jina la Hassan ambaye ndiye mkazi wa huko alidaiwa kuwafuata marehemu hao Mtoni Madafu na kuwaambia ametumwa na mama yake mzazi aende akafanye vurugu kwa hawara ‘mchepuko’ wa baba yake. INASIKITISHA sana! Vijana wawili, Jumanne Omar (17) na Mgeni Rashidi Rajabu (16) (aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Keko), Dar, wakazi wa Mtoni Madafu, Temeke wameuawa kwa kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali baada ya kudhaniwa kuwa ni wezi. Inadaiwa kuwa, Hassan akiwa na vijana wengine wawili, aliongozana na vijana hao kwenda Gongo la Mboto kwa mwanamke huyo ambaye ni mama lishe.Ndugu mmoja wa Jumanne anasimulia: “Walipofika kwa mama lishe huyo ambaye Hassan alidai ndiye mchepuko wa baba yake, waliagiza chakula. Walipomaliza kula yule mama aliwadai pesa, Hassan akasema hawana na hawatoi. “Tunasikia yule mama

HAKIMU AFIA MAHAKAMANI KIUTATA JIJINI DAR

Image
Marehemu Hakimu Rogart Venance Alphonce enzi za uhai wake.  Tukio hilo la kusikitisha na lililoibua vilio kwa watumishi wa mahakama hiyo na wale waliokuwa na kesi, lilijiri Aprili 13, mwaka huu mahakamani hapo wakati makarani wakiandaa mafaili ya kesi mbalimbali. HAYA ndiyo majanga! Hali ya hewa ilibadilika ghafla katika Mahakama ya Mwanzo Ukonga, Dar kufuatia Mheshimiwa Hakimu Rogart Venance Alphonce (54) kuugua ghafla, kudondoka na kutokwa povu mdomoni na puani, hatimaye kufariki dunia! Inauma sana! KUMBE ALIKUWA ANARIPOTI KITUO KIPYA CHA KAZI Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari mahakamani hapo, Mheshimiwa Alphonce siku hiyo ndiyo alikuwa akiripoti mahakamani hapo kikazi akitokea Mahakama ya Mwanzo Lugoba, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani ndipo akapatwa na matatizo hayo ambapo wengi walidai kifo chake kilitokana na ushirikina. “Huyu hakimu si mgeni kwangu, namjua kwa utendaji wake wa kazi na ni mtenda haki katika hukumu anazozitoa, amekuwa akifuata sheria

RAY C NAYE ATESWA NA UGUMBA

Image
Nyota wa muziki Rehema Chalamila, Ray C.   WAKATI staa wa Bongo Movie, Wema Sepetu akiweka wazi kuwa hawezi kupata ujauzito huku Judith Wambura ‘Jide’ naye akisumbuliwa na tatizo hilo, nyota wa muziki Rehema Chalamila, Ray C amefunguka na kusema kuwa hali ya kukosa mtoto ambayo ni sawa na ugumba, inamtesa, kwani katika umri wake wa miaka 33, hajabahatika kuwa naye. Akizungumza juzikati, Ray C alisema kuwa pamoja na hamu yake ya muda mrefu ya kupata mtoto, lakini ameshindwa ingawa anaamini siku yoyote Mungu atamuwezesha jambo hilo.“Hao kina Jide, Wema mi naona kama ni cha mtoto. Katika uhusiano wangu wa kimapenzi tangu nivunje ungo, nimewahi kushika mimba mara moja tu, wakati huo nikiwa na Mwisho Mwampamba, lakini bahati mbaya ilitoka, tokea hapo sijapata tena,” alisema staa huyo ambaye yupo katika mapambano ya kuacha matumizi ya madawa ya kulevya. Alisema katika umri wake huo anatamani sana kuwa na mtoto, kwani wasichana aliozaliwa nao wakati mmoja hivi sasa wanao w

Online Dating: Is it just for losers?

Image
Online dating used to be this scary and shameful thing when it just started.You know, back in the day, when people thought that internet is for porn and creepy perverts only. People used to have this weird idea that only creeps and losers would stoop so low as to try and find love on the internet. Thank god it’s all in the past and everyone knows that internet is awesome and serves many purposes. The truth is, nowadays you spend most of your day on the internet. We’re all constantly on Twitter, Facebook, Instagram, Pinterest, Youtube. That’s how we make friends. That’s how we work, shop, watch movies. So why not find love the same way? And yet, the last few, lets call them “oldfashioned” people who still don’t believe in online dating and think it’s a horrid idea. Well, let’s see how it really is and shun those ideas once and for all. First and foremost it’s important to state that 1 in 5 relationships starts online these days. Be it specific online dating services, or

WOLEPR ALEWA AZIMA, WEMA SEPETU NA MWANAUME SHOGA PATASHIKA! A-Z IPO HAPA MDAU...!

Image
Masistaduu wawili kunako gemu la Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu na Jacqueline Wolper Massawe wakipiga mtungi usiku mnene. ENEO LA TUKIO Hatari! Masistaduu wawili kunako gemu la Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu na Jacqueline Wolper Massawe, wamejikuta wakipiga ulabu hadi kulewa chakari, kisa kikielezwa kwamba wana msongo wa mawazo, Risasi Jumamosi linafunguka. Tukio hilo lililoshuhudiwa na gazeti hili lilijiri hivi karibuni, usiku mnene kwenye pati ya kuzaliwa (birthday) ya meneja wa kampuni ya Wema ya Endless Fame almaarufu Petit Man iliyofanyika kwenye nyumba ya jamaa mmoja maeneo ya Kinondoni-Manyanya jijini Dar na kuhudhuriwa na mastaa kibao. Katika pati hiyo ambayo mbali na mastaa ilihudhuriwa na watoto wa mjini, watu waligonga msosi wa kufa mtu kisha vikafuata vinywaji. Tofauti na ‘maraia’ wengine, Wema na Wolper walikuwa wakigonga vinywaji vikali hadi wakawa tilalila na kuanza kufanya vituko, jambo ambalo liliwashangaza wengi.Kadiri muda ulivyokuwa unasonga ndivy

MAMBO 10 ALIYOSEMA WEMA KATIKA MAISHA BAADA YA KUACHANA NA DIAMOND

Image
Ijumaa hii Wema Sepetu alikuwa mgeni kwenye kipindi cha Ubaoni cha EFM. Miongoni mwa mambo aliyoulizwa ni pamoja maisha baada ya kuachana na Diamond Platnumz.   Haya ni mambo 10 aliyosema: 1. Maisha yake bila Diamond yako poa tu japo mazoea yaliyokuwa yamezidi kati yao yanamfanya wakati mwingine kummiss! 2. Ameshakubali ukweli kwamba yuko mbali na Diamond 3. Anaamini kuwa Diamond anammiss pia kutokana mazoea waliyokuwa nayo 4. Wema na Diamond sio marafiki 5. Hana  kinyongo na Diamond ila anaamini kuwa Diamond bado ana kinyongo naye 6. Ni shabiki na ataendelea kuwa shabiki wa nyimbo za Diamond 7. Hawajahi kukutana na Diamond tangu waachane 8. Hajawahi kumpigia simu 9. Aliwahi kumtumia meseji Diamond kumpa pole kwa kuuguliwa na mama yake 10. Bado hajapata mwanaume mwingine

HIZI NDIO TAARIFA ZENYE UHAKIKA KUHUSU ALIYEKUWA MPENZI WAKE LULU MICHAEL

Image
Mitandao ya kijamii kuanzia kwenye Whatsapp mpaka twitter, Facebook na Instagram siku hizi imekua na nguvu kubwa na ndio maana hata taarifa zinaenea kwa kiasi kikubwa sana siku hizi bila kungoja Magazeti, Radio au TV. Najua kama unafatilia habari zinazoendelea mjini utakua umekutana na voicenote au taarifa ya kifo cha huyu ndugu yetu inaweza kuwa imekufikia lakini sio kwa usahihi, au chanzo cha kifo kinaweza kuwa kimepotoshwa.   Sasa familia ya Marehemu Lusekelo Samson Mwandenga ( Secky ) imekanusha taarifa zinazoendelea kusambazwa kupitia voice note na kwenye mitandao kuhusu chanzo cha kifo chake na kwamba alikwenda kwenye birthday,  "ukweli ni kwamba aliumizwa na kiti cha kioo akiwa kambeba mtoto wake nyumbani kwake, akapelekwa hospitali na baadae akafariki akiwa Hospitali, hakuna kingine zaidi ya hapo". Secky alikua rafiki wa watu wote wakiwemo wasanii wengi wa bongofleva na hata bongomovie pia ndio maana msiba huu umewagusa kutokana

Majibu ya Amanda Kuhusu Madai ya Kutumia ARV

Image
Staa wa Bongo Movies, Tamrina Posh ‘Amanda’ hivi karibuni aligeuka mbogo kwa shabiki wake aliyefahamika kwa jina la Joel baada ya kuambiwa eti ni mmoja wa wasanii wanaotumia vidonge vya ARV vya kuongeza siku za kuishi kwa waathirika wa Ukimwi. Ishu ilianzia kwenye mtandao wa Facebook ambapo Joel aliona picha ya Amanda akipima ugonjwa ambao haukujulikana ndipo kijana huyo alipokomenti kwamba eti msanii huyo ana ngoma.Akizungumza na Ijumaa, Amanda alisema amechoshwa na watu wanaomkashifu mtandaoni wakidhani kila msanii ni mhuni. “Nimeona nimtolee uvivu kwani asifikirie Bongo Muvi wote tunatumia ARV, mimi nimepima mara ya mwisho juzi na najiamini najua ninachokifanya, alinikera sana yule kijana ndiyo maana nikampa makavu,” alisema Amanda.

AJALI MBAYA YATOKEA KIWIRA MKOANI MBEYA YAUWA WATU 18 ASUBUHI HI!!

Image
Habari zaidi zitawajia punde tutakapozipata

IRENE UWOYA ANA MIMBA YA PILI?! SOMA ALICHOKIANDIKA NA TAZAMA PICHAZ HAPA...

Image
Staa mrembo wa Bongo, Irene Uwoya amewaacha njia panda mashabiki wake baada ya kubandika picha mtandaoni akionekana yupo bafuni akiwa amejishika tumbo na kuiandikia maneno akiwatata mashabiki wamtajiae majina mazuri ya kike. “Ntajie majina mazuri yakike unayoyapenda.....”- Uwoya aliandika. Kauli hii ilizua maswali mengi kutoka kwa mashabiki wakioji kama mrembo ambae ni mama wa mtoto mmoja kama anaujamzito au la, wengine walienda mbali zaidi wakisema kuwa inawezekana akawa ni mjauzito na anatarajia kujifungua mtoto wa kike. Mbali komenti nyingi kumtaka atoe maelezo zaidi juu ya hili, Uwoya hakujitokeza kusema lolote hivyo hadi sasa mashabiki wake wapo njia panda wakijiuliza, …ana ujauzito au hana? Swaga kama hizi ya mtandaoni huwa mara nyingi zina maaanisha picha picha za tumbo zimekuwa nyingi sana kutoka kwa mrembo huyo. ngoja tuendelee kusubiri kwani hili ni jambo la kheri. Mzee wa Ubuyu

HALI ILIVYOKUWA NYUMBANI KWA GWAJIMA LEO

Image
Askari wakiwa nyumbani kwa Gwajima. Makamanda wa polisi wakiwa tayari kwa lolote. Gari lililombeba Gwajima likitoka ndani ya nyumba yake kuelekea kituo kikuu cha polisi kwa ajili ya mahojiano. Mawakili wa Gwajima wakisalimiana na mmoja wa maofisa wa polisi mara baada ya kufika eneo la tukio. Waandishi wa habari wakiwa eneo la tukio. Waumini wa Gwajima wakiwa wamezunguka nyumba wa askofu wao.  Kundi la wafuasi wa Gwajima wakifika nyumbani kwake mara baada ya polisi kuondoka eneo la tukio.  Baadhi ya watu waliokuwemo ndani ya nyumba ya Gwajima wakichungulia dirishani.  Baadhi ya waumini wa Gwajima wakifuatilia kwa makini hali iliyokuwapo.  Baadhi ya waumini wakiwa mbele ya nyumba ya Gwajima. Gari la polisi likiondoka eneo la tukio. Hapa wakishangilia ushindi baada ya polisi kuondoka eneo la tukio. WAKATI taarifa zikisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya jamii kuwa nyumba ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, imezingirwa na polisi, habari kamili n