CHAMA CHA TLP KIMEMPENDEKEZA MREMA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA VUNJO

Mh. Augustine Mrema
Kamati Kuu ya Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), imempendekeza Augustine Mrema ambae pia ni mwenyekiti wa chama hicho kutetea kiti chake cha ubunge katika jimbo la Vunjo.
Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho Nancy Mrikaria, akiongea jana na gazeti la mwananchi alisema kuwa kamati hiyo pia imemthibitisha Mrema kuendelea na nafasi yake ya uenyekiti wa chama hicho kwa mara nyingine.
Alisema kamati imeridhia Mrema kuendelea kugombea ubunge katika jimbo la Vunjo ikiwa na imani kuwa ana nafasi kubwa ya kushinda, ikilinganishwa na wengine waliotangaza nia ya kupambana nao.
“Kamati imefikia hatua hiyo kwa kutambua uwezo alionao mwenyekiti katika kukiendeleza chama, pia hadi sasa hakuna mwanachama mwingine aliyejitokeza kugombea nafasi hiyo na tulianza kutoa fomu tangu Aprili 9 hadi 17, wakati kwenye nafasi ya makamu mwenyekiti Bara ndiyo kuna ushindani wa watu wawili wanaoigombea,” aliliambia gazeti la mwananchi.
CHANZO: MWANANCHI

Comments

Popular posts from this blog