WAZIRI STEVEN WASIRA AWAFUKUZA WAKURUGENZI WATATU KWA KUISABABISHIA SERIKALI HASARA YA BILLION 2.5
WAZIRI wa kilimo, Chakula na Ushirika Steven Wasira amewafukuza kazi wakurugenzi watendaji watatu wa Mamlaka ya Kuendeleza Bonde la Mto Rufiji (Yaani Rufiji River Basin Development Authority – RUBADA) kutokana na matumizi mabaya ya ofisi ya Umma ambayo yameitia hasara ya Bilioni 2.5 Serikali . Akitoa agizo hilo leo mbele ya Waandishi wa Habari, Waziri Wasira amewataja Watendaji hao kuwa ni Bwana Aloyce L. Masanja – Kaimu Mkurugenzi Mkuu; Bibi Tabu Ndatulu – Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji; na Bwana Filozi John Mayayi – Mkurugenzi wa Fedha na Utawala. Wassira amesema baada ya Ofisi yake kupata malalamiko kutoka kwa wananchi wa vijiji vya Rufiji pamoja na wawekezaji juu ya Urasimu wa shirika hilo, aliunda timu ya Uchunguzi kutoka wizara ya Kilimo na Hazina kwenda kuchunguza malalamiko hayo. “Baada ya kuunda tume kutoka hapa Wizarani ikishirkiana na Hazina, walienda kwenye shirika hilo kufanya ukaguzi.Tume ilibaini kwamba mfumo wa pale ulikuwa ni