MCHUNGAJI GWAJIMA AONJA JOTO LA KUMTUKANA PENGO...SOMA HAPA

 
Kanisa lisilo rasmi la Mchungaji Josephat Gwajima lililokuwa likiendesha shughuli zake kinyume na taratibu katika viwanja vya Tanganyika Packers mtaa wa Kawe Ukwamani Wilaya ya Kinondoni,
jijini Dar es salaam limeamuriwa kuondoka mara moja na kuacha eneo hilo wazi kwa ajili ya maendeleo ya watu wa Kawe. Kanisa hilo ambalo kwa muda mrefu limekuwa likiendesha shughuli zake kinyume na taratibu na kusababisha usumbufu na kero kubwa za makelele kwa wakazi wa maeneo hayo.
Katika Barua ya pili iliosainiwa na Meneja wa Mkoa wa Kinondoni wa shirika la nyumba la Taifa mnamo tarehe 9/03/2015 baada ya ile ya kwanza iliyotolewa tarehe 19/02/2015 imesisitiza kwamba pamoja na kutambuliwa umuhimu wa kanisa hilo kuendesha shughuli zake lakini shirika hilo halitaweza kutoa ruhusa kwa kanisa hilo kuendelea kufanya mahubiri katika viwanja hivyo kwani shirika hilo limeshaanza kutumia Viwanja hivyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa makazi nk. Bwn Masika alitoa siku 30 tu ambazo leo 7/04/2015 Mchungaji Gwajima anatakiwa kufunga virago na kuacha viwanja hivyo wazi kwa ajili ya maendeleo

Comments

Popular posts from this blog