Posts

UTATA MTUPU KESI YA AUNT EZEKIEL ...!SOMA ZAIDI HAPA..

Image
MSANII  wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel amesema hivi karibuni aligongana uso kwa uso na Ivon Bigilwa ambaye anadaiwa kumchana kwa chupa mkononi na kesi hiyo inaendelea katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.   Msanii  wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel akliwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar. Aunty alisema hayo juzi Jumatatu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam mbele ya hakimu Agustina Mbando, akikanusha taarifa ya wadhamini wa Ivon, Christopher Mwaseba na Anthon Mwaseba walioiambia mahakama kuwa mtuhumiwa alikuwa nyumbani akimuuguza mama yake.   Ivon Bigilwa aliyemchana Aunt kwa chupa. Msanii huyo alisema wadhamini hao wanaidanganya mahakama kwa kuwa hivi karibuni alikuwa nchini China na aligongana naye uso kwa uso. Kutokana na hilo, Hakimu Mbando aliwaonya wadhamini hao kwa kuidanganya mahakama na kuwataka wampeleke mtuhumiwa huyo mbele ya mahakama hiyo Juni 10, mwaka h

BOTI YAZAMA NA KUUA WATU WATANO ZIWA VICTORIA

Image
Watu watano wamekufa maji baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama   ndani ya Ziwa Victoria.Kamanda wa Polisi wa Mkoawa Kagera, George   Mayungaalisema ajali hiyo ilitokea Mei 23 mwaka huu saa 8 usiku. Boti   ya Mv Kitoko II waliyokuwa wakisafiria kutoka Bugombe kupitia Kasenye   kwenda Mganza wilayani Chato, ilizimika ghafla ikiwa katikati ya   ziwa.Alisema boti hiyo inayomilikiwa na Mama Chacha aishiye Muganza ,   ilikuwa na abiria hao watano,ambao wote walikufa maji. Maiti   aliyepatikana ni mfanyabiashara raia wa Rwanda, Jane Mlekatete (36)   ambaye mwili wake ulikutwa ukielea. Wengine waliozama ambao   hawajapatikana ni Chikola Filbert (22) mkazi wa Muganza, Mapinduzi   Daud ( 38 )mkazi wa Mwanza, Ashana Suzy waliotambuliwa kwa jina moja   moja, wote wakazi wa Kasenyi na Mavombe (23) ambaye ni mkazi wa   Muganza.Alisema chanzo cha ajali hiyo ni boti kubeba mzigo mkubwa. Kwa   mujibu wa Kamanda, ilikuwa imebeba magunia 210.Chanzo kingine cha   ajal

ANGALIA PICHA MWANAMKE ACHANWA NA VIWEMBE KWA WIVU

Image
Stella Mbinga akiwa na majeraha ya viwembe. INASIKITISHA sana! Stela Mbinga ambaye ni mke wa mtu, mkazi wa Tegeta - Kontena jijini Dar amepata balaa kubwa baada ya kuchanwachanwa uso wake kwa viwembe na jirani yake aliyefahamika kwa jina la Zakia Mohamed. Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa, Zakia na Stella kwa muda mrefu wamekuwa wakiishi maisha ya uhasama na kuringishiana hali iliyojenga chuki miongoni mwao.“Hawa huwa wanashindana kimaisha. Huyu akifanya hivi, mwingine anafanya vile. Cha kushangaza huwa wanatishiana hadi mambo ya vyakula, kwamba nani anakula vizuri zaidi ya mwenzake. “Sasa juzi Stella alikuwa amekaa kibarazani wanazungumza na shoga yake, Zakia alipita akawakuta wanacheka, hata alipokuwa chumbani wakaendelea na vicheko vyao, akahisi wanamsema na kumcheka yeye, alipotoka akamvaa Stella, kumbe alikuwa na kiwembe, akaanza kumchana bila huruma,” alisema mmoja wa majirani wa wanawake hao. Wasamaria wema walimpeleka Stella Kituo cha

MWANAMKE ALIYEHUKUMIWA KIFO AJIFUNGUA.

Image
Mwanamke aliyeasi dini nchini Sudan na kupata adhabu ya kifo amejifungua mtoto mvulana akiwa jela mjini Khartoum kwa mujibu wa wakili wake. Meriam Yehya Ibrahim Ishag, aliolewa na mwanamume mkristo jambo lililopelekea mwanamke huyo kuhukumiwa kifo mapema mwezi huu baada ya kukataa kusilimu tena. Ataruhusiwa kumnyonyesha mtoto wake kwa miaka miwili kabla ya hukumu kutekelezwa. Meriam aliyezaliwa na wazazi waisilamu, alihukumiwa na mahakama ya ya kiisilamu. Bi Ibrahim alihukumiwa kifo kwa kosa la zinaa kwa sababu ameolewa na mwanamume mkristo wa kutoka Sudan Kusini na kwamba ndoa yao haikubaliki chini ya sheria ya kiisilamu ambayo inasema kuwa mwanamke muisilamu hawezi kuolewa na mwanamume mkristo. Kwa kosa hilo, jaji alimuhukumu adhabu ya mijeledi miamoja, adhabub ambayo itatekelezwa pindi mama huyo atakapopata nafuu kutokana na kujifungua. Bi Ibrahim alilelewa kwa njia ya kikristo , dini ya mamake kwa sababu babake aliyekuwa muisilamu hakuwepo katika

HOFU YATANDA: BINTI ALIYEZIKWA AIBUKIA KWAO

Image
Witness Obed (21) aliyefariki dunia Aprili 12 mwaka huu na kuzikwa kwenye makaburi ya nyumbani kwao Kijiji cha Nanja, mkoani Arusha na kuibuka akiwa hai tena. HOFU  ya ushirikina imetikisa Mkoa wa Arusha kufuatia tukio la hivi karibuni ambapo mwanafunzi wa Chuo cha Kompyuta jiji hapa, Witness Obed (21) aliyefariki dunia Aprili 12, mwaka huu na kuzikwa kwenye makaburi ya nyumbani kwao Kijiji cha Nanja, Kata ya Moshono wilayani Arumeru, Arusha kuibuka akiwa hai. Binti huyo aliibuka kwao hivi karibuni akiwa mpole na kuwafanya baadhi ya watu, wakiwemo wazazi wake kutimua mbio kwa hofu. Watu kutoka maeneo mbalimbali jijini hapa  wamekuwa wakimiminika nyumbani kwa wazazi wa binti huyo kwa lengo la kumshuhudia kwa vile ndugu walishaamini kuwa, mpendwa wao huyo alishakufa na alizikwa. Umati wa watu ukiwa katika hali ya mshangao kutokana na tukio hilo. UWAZI LATIA TIMU NYUMBANI Baada ya kusikia taarifa hizo, Uwazi lilifunga safari mpaka eneo la tukio na

ANGALIA PICHA MAJAMBAZI WALIOUWAWA TEMEKE

Image
Mwili wa jambazi mwingine ukiwa umeharibika vibaya baada ya kipigo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira. Mwili wa mmoja wa majambazi ukiwa chumba cha kuhifadhia maiti 

HII NDO JEURI YA PESA YA H-BABA ...CHEKI GARI JIPYA LA KIFAHARI

Image
  Maisha ya mastar wetu wa Kitanzania yanazidi kukua zaidi na kuwapelekea kumiliki baadhi ya vitu vya gharama,baada ya baadhi ya wasanii kuonyesha magari yao,hili ndilo gari sasa analotembelea mume wa Frola Mvungi hit maker wa Mpenzi Bubu,Poteza na hit zingine H.baba. Mbali na muziki H.baba amesema kuwa vyanzo vingine vya mapato ni pamoja na bidhaa zake za pipi alizozizindua miezi michache iliyopita zinazopatikana Mwanza pekee pamoja na uigizaji wa filamu mbalimbali za Kitanzania. Hii gari aina yake ni Mr s ambalo buti yake iko kwa mbele sehemu ambayo ipo engine yake,hapo chini nimekuwekea bei kama uki google ingawa kwa pesa za Kitanzania ni zaidi ya Milioni 70 kwa bado kuisafirisha na ushuru.

ANGALIA PICHA MATESO ANAYOPATA HUYU.MSAADA WAKO UNAHITAJIKA

Image
MWANAFUNZI wa kidato cha nne nchini Burundi, Miburo Anne Mony (17), raia wa nchi  hiyo amesema anakwenda kufia kwao baada ya madaktari ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kumwambia ugonjwa wake wa kansa umecheleweshwa hivyo si rahisi kutibika. HAJUI ATARUDIJE NYUMBANI Akizungumza na mwandishi wetu huku akibubujikwa machozi ndani ya Wodi Na. 24, Sewa Haji, Muhimbili, mwanafunzi huyo wa kike ambaye hajui Kiswahili wala Kingereza vizuri alisema hajui atarudije kwao Burundi kwa kuwa hana fedha baada ya kuishiwa. Aliongeza kwamba alikuwa na matarajio kuwa angepata matibabu hapa Tanzania baada ya huko kwao kushindikana. UGONJWA ULIVYOANZA “Ugonjwa huu ulianza kama uvimbe nikiwa kidato cha kwanza, ulikuwa ikiwasha kupita kiasi, ulizidi kuvimba kwa kasi ya ajabu, nikakatisha masomo kwa vile nilianza kupata maumivu makali mno. “Mama alianza kuhangaika kwa kunipeleka katika hospitali mbalimbali kule kwetu Burundi bila mafanikio. “Mama yangu ni mkulima, hana uwe

TAIFA STARS YATUA DAR KUPEPETANA NA MALAWI, TFF YAWAOMBA MASHABIKI KUFURIKA UWANJANI

Image
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam TIMU ya Taifa ya Tanzania chini ya kocha mkuu, Mholanzi, Mart Nooij inatarajia kujipima ubavu katika mechi ya kimataifa ya kirafiki jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam  dhidi ya timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) kuanzia majira ya saa 11:00 jioni. Taifa Stars iliyopiga kambi yake mjini Tukuyu jijini Mbeya inatarajia kuwasili asuhubi hii majira ya saa 4:00 katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ndege ya Air Tanzania. Wapinzani wa Taifa stars tayari wapo jijini Dar es salaam kwa ajili ya mechi hiyo muhimu kwa makocha  kuangalia uimara wa timu zao kabla ya kwenda kucheza mechi za mashindano.

BREAKING NEWZZ MSANII MWINGINE TENA ''RECHO'' AFARIKI DUNIA ASUBUHI HII

Image
Msanii wa Bongo Movie, Rachel Haule 'Recho' (pichani), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es slaaam. Habari zilizotua Global na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere, zimesema kuwa Recho alikwenda Muhimbili jana kujifungua ambapo mara baada ya kujifungua mtoto alifariki na yeye hali yake kuwa mbaya, ilibidi ahamishiwe ICU ambako hali ilizidi kuwa mbaya na baadae kufariki dunia. Kifo cha Recho kimekuja ndani ya wiki moja baada ya kufariki kwa msanii mwingine wa Bongo Movi Adam Kuambiana Jumamosi iliyopita, kifo hiki kimeleta mstuko mkubwa kwenye tasnia ya ya filamu za kibongo. Habari na picha zaidi zitawajia baadae.  PICHA: Makatab za GPL

VIATU VYA KANUMBA VYAKOSA MVAAJI, BONGO MOVIE NA WATAYARISHAJI FILAMU WALALAMA

Image
Wasambazaji wa filamu wanasema hakuna mauzo tena ya filamu toka kifo cha marehemu Steven Kanumba, wanalalamika kuwa mauzo yameshuka sana hadi hata wengine kuachana na biashara hiyo na kuamua kufanya biashara nyingine zinazowalipa. Inawezekana maneno yao yakawa sahihi au si sahihi, kutokana na hali halisi ya mfumo wa tasnia ya filamu ulivyo hasa katika idara ya mauzo, sasa kila mtu anajaribu kutafuta sehemu gani ya kuangukia ndio tunasikia wakisema kuwa toka kifo cha Kanumba hakuna mauzo ya filamu. Hayati Steven Kanumba Mtayarishaji na mwigizaji Nyota Swahiliwood Kanumba akiwa katika pozi Umati wa watu siku ya mazishi ya Kanumba Hayati Kanumba akiwa na mwigizaji wa kimataifa Ramsey Noah kutoka Nigeria Enzi za uhai wake Kanumba the Great Ni kweli hakuna ubishi kuwa Kanumba alikuwa na mvuto wa kipekee katika tasnia ya filamu Bongo lakini hatuna mbadala wake? Ambaye anaweza kuvaa viatu vyake na kuifanya tasnia ya filamu ifanye vizuri kam

PICHA ZA VIJANA WA MBWA MWITU NA PANYA ROAD WALIOKAMATWA NA JESHI LA POLISI BAADA YA KUWA TISHIO KWA WANAINCHI KWA MDA MREFU

Image
Hawa ndio viongozi wa panya road na mbwa mwitu ambao tayari wameshakamatwa  Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanya msako wa nyumba kwa nyumba, mtaa na maeneo yaliyoathirika kwa hofu ya vijana ambao ni vibaka maarufu kama Mbwa mwitu au Panya Road.  Msako huu uliofanyika ndani ya masaa 24 hadi alfajiri ya tarehe 26/5/2014 kwa lengo la kuwaondolea hofu na uhalifu dhidi ya makundi ya vijana wadogo wasio na ajira ambao uliibuka hivi karibuni.         Maeneo yaliyoathirika ni Kigogo, Magomeni, Tabata, maeneo yote yanayozunguka mto Msimbazi, maeneo ya Mbagala nk.  Msako huu unaendelea kufanywa na askari wa vikosi maalum ambao wamepewa kazi ya kuhakikisha kuwa vikundi hivyo haviibuki tena na vinatokomezwaa kabisa kwa  kuwakamata wale wote wanaojihusisha na vitendo vya kuvamia kwa mkundi wananchi ambao hawana hatia Kamishna kova ambaye amezungumza na wanahabari muda mfupi uliopita  Kati ya watuhumiwa 149 waliokamatwa mmoja amegundulika kuwa ni kiongozi aitw