ANGALIA PICHA MATESO ANAYOPATA HUYU.MSAADA WAKO UNAHITAJIKA

MWANAFUNZI wa kidato cha nne nchini Burundi, Miburo Anne Mony (17), raia wa nchi  hiyo amesema anakwenda kufia kwao baada ya madaktari ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kumwambia ugonjwa wake wa kansa umecheleweshwa hivyo si rahisi kutibika.
HAJUI ATARUDIJE NYUMBANI
Akizungumza na mwandishi wetu huku akibubujikwa machozi ndani ya Wodi Na. 24, Sewa Haji, Muhimbili, mwanafunzi huyo wa kike ambaye hajui Kiswahili wala Kingereza vizuri alisema hajui atarudije kwao Burundi kwa kuwa hana fedha baada ya kuishiwa.
Aliongeza kwamba alikuwa na matarajio kuwa angepata matibabu hapa Tanzania baada ya huko kwao kushindikana.
UGONJWA ULIVYOANZA
“Ugonjwa huu ulianza kama uvimbe nikiwa kidato cha kwanza, ulikuwa ikiwasha kupita kiasi, ulizidi kuvimba kwa kasi ya ajabu, nikakatisha masomo kwa vile nilianza kupata maumivu makali mno.
“Mama alianza kuhangaika kwa kunipeleka katika hospitali mbalimbali kule kwetu Burundi bila mafanikio.
“Mama yangu ni mkulima, hana uwezo, alikuwa akitafuta pesa kwa shida kwa vile baba alishafariki dunia, kwa hiyo majukumu yamekuwa ya kwake. Mama hakuchoka, alinipeleka Hospitali Kuu ya Roi Khared ambako pia matibabu yakashindikana, nikarudishwa nyumbani.”
UWEZO WA MAMA UMEKWISHA
“Nilikuwa natokwa machozi pale nilipowaona wanafunzi wenzangu tuliofaulu nao wakienda shule huku mimi nikiwa nyumbani na sijui hatima yangu.
Mama naye alivunjika moyo akawa hana pa kunipeleka kwani uwezo wake wa kuzunguka na mimi kifedha ulikwisha. Nilisubiri kifo tu.
“Siku moja mama aliambiwa na watu kwamba ugonjwa wangu unatibika katika Hospitali ya Muhimbili hapa Tanzania. Alijiuliza namna ya kunileta huku kwani nauli na fedha za matumizi alikuwa hana.”
MICHANGO ILICHANGWA
“Nilichangiwa michango lengo likiwa niletwe Muhimbili, fedha kidogo ilipatikana likaibuka swali la nani atanileta? Maana mama hajui Kiswahili wala Kingereza.
Akamuomba kaka yangu anaitwa Albert ambaye ni mtoto wa baba mkubwa, yeye anafanya kazi ya kufagia barabara na aliomba ruhusa ya wiki mbili ambayo inaelekea kwisha sasa.
“Tulipofika hapa Muhimbili nashukuru tulipokelewa vizuri, nikapata matumaini ya kipona. Madaktari walinikata nyama ya midomo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.”
UGONJWA HAUTIBIKI
“Baadaye madaktari walinishtua sana, waliniambia eti nina kansa na haiwezi kutibika maana imekaa kwa muda mrefu. Kwa hiyo sasa natakiwa nirudi nyumbani hadi hapo Mungu atakapochukua roho yangu.
“Niliposikia hivyo nilipoteza fahamu, nikazinduka baadaye. Kilichonifanya nizimie ni kule kuambiwa tegemeo la kupata matibabu hakuna.
“Sina mahalI pa kwenda tena bali ni kurudi Burundi  nikafie kule. Yote namwachia Mungu, hamna jinsi, nakufa nikijiona,” alimaliza kusema mwanafunzi huyo huku akibubujikwa machozi.
Kwa upande wake kaka yake Albert alisema wamezunguka kila hospitali kutafuta matibabu bila mafanikio.
“Kwa sasa nimeishiwa nauli, hatujui tutaendaje nyumbani, nilikwenda kwenye ubalozi wetu kuomba msaada wakaniambia si rahisi kusaidiwa kwa vile hatukuletwa na serikali. Sijui nitarudi vipi na huyu mgonjwa,” alisema Albert.
Anayetaka kusaidia nauli ya kurudi kwao Burundi anaweza kumchangia kwa kuwasiliana na Idara ya Ustawi wa Jamii Muhimbili kwa simu namba 0766 534498.

Comments

Popular posts from this blog