TAIFA STARS YATUA DAR KUPEPETANA NA MALAWI, TFF YAWAOMBA MASHABIKI KUFURIKA UWANJANI

DSC_4615Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
TIMU ya Taifa ya Tanzania chini ya kocha mkuu, Mholanzi, Mart Nooij inatarajia kujipima ubavu katika mechi ya kimataifa ya kirafiki jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam  dhidi ya timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) kuanzia majira ya saa 11:00 jioni.

Taifa Stars iliyopiga kambi yake mjini Tukuyu jijini Mbeya inatarajia kuwasili asuhubi hii majira ya saa 4:00 katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ndege ya Air Tanzania.
Wapinzani wa Taifa stars tayari wapo jijini Dar es salaam kwa ajili ya mechi hiyo muhimu kwa makocha  kuangalia uimara wa timu zao kabla ya kwenda kucheza mechi za mashindano.

Comments

Popular posts from this blog