HOFU YATANDA: BINTI ALIYEZIKWA AIBUKIA KWAO
Witness Obed (21) aliyefariki dunia Aprili 12 mwaka huu na kuzikwa kwenye makaburi ya nyumbani kwao Kijiji cha Nanja, mkoani Arusha na kuibuka akiwa hai tena. HOFU ya ushirikina imetikisa Mkoa wa Arusha kufuatia tukio la hivi karibuni ambapo mwanafunzi wa Chuo cha Kompyuta jiji hapa, Witness Obed (21) aliyefariki dunia Aprili 12, mwaka huu na kuzikwa kwenye makaburi ya nyumbani kwao Kijiji cha Nanja, Kata ya Moshono wilayani Arumeru, Arusha kuibuka akiwa hai. Binti huyo aliibuka kwao hivi karibuni akiwa mpole na kuwafanya baadhi ya watu, wakiwemo wazazi wake kutimua mbio kwa hofu. Watu kutoka maeneo mbalimbali jijini hapa wamekuwa wakimiminika nyumbani kwa wazazi wa binti huyo kwa lengo la kumshuhudia kwa vile ndugu walishaamini kuwa, mpendwa wao huyo alishakufa na alizikwa. Umati wa watu ukiwa katika hali ya mshangao kutokana na tukio hilo. UWAZI LATIA TIMU NYUMBANI Baada ya kusikia taarifa hizo, Uwazi lilifunga safari mpaka eneo la t...