ANGALIA PICHA NJIWA MWENYE HIRIZI ATIKISA MUHIMBILI
Njiwa aliyetua kwenye kitanda cha mgonjwa na baada ya muda mgonjwa akafariki. Hofu kubwa ilitanda katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jumatatu ya wiki iliyopita, baada ya Njiwa mweusi, mwenye miguu myekundu akiwa na hirizi iliyofungwa katika mojawapo ya mabawa yake, kutua katika miguu ya mgonjwa aliyekuwa amelazwa wodi namba tatu, jengo la Mwaisela.Taarifa zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya wauguzi wa wodi hiyo ambao hawakutaka majina yao yaandikwe gazetini, walisema tukio hilo lilitokea saa 3.55 asubuhi ambapo njiwa huyo aliingia kupitia dirishani na kwenda kutua mguuni mwa Mwanahawa Ngunda (61) aliyekuwa amelala kitanda namba 7, ambaye anadaiwa kuwa mkazi wa Kimara. Njiwa huyo aliingia dirishani muda mfupi baada ya mgonjwa aliyekuwa jirani na Mwanahawa, aitwaye Fatuma Musa (45) kurejea wodini hapo akitokea kupata vipimo ambapo alisaidiwa na ndugu zake kupanda kitandani kutokana na kuishiwa nguvu. Inadaiwa kuwa baada ya kuingia wodini, njiwa huyo alianza