AIRTEL YAPIGA TAFU TIMU YA TAIFA YA VIJANA CHINI YA MIAKA 17
KAMPUNI ya Airtel Tanzania imeahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuendeleza michezo nchini ili kuleta ufanisi katika sekta ya michezo. Akizungumza kabla ya kukabidhi mipira 100 kwa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Airtel Tanzania Bwana Sunil Colaso alisema uwekezaji katika michezo ni mhimu hasa katika kipindi hiki amabacho Tanzania inajipanga kushiriki katika mashindano ya kikanda na kimataifa. “Airtel Tanzania tunakabidhi mipira 100 kwa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 kama sehemu ya juhudi zetu kusaidia maendeleo ya michezo. “Tutaendelea kushirikiana na Serikali pamoja na wadau wengine kuhakikisha nchi inapata mabalozi wa kutuwakilisha vizuri katika mashindano ya kimataifa” alisema Colaso alisema mwaka 2011 kampuni yake kwa makusudi ilianzisha Airtel Rising Stars ikiwa ni mpango wa kuvumubua na kuendeleza vipaji kwa vijana wadogo kutoka ngazi ya chini ili ku