VYAKULA MUHIMU SANA MWILINI MWAKO



 
NDUGU msomaji. Katika makala zilizopita tuliwahi kuzungumzia jinsi dawa za ‘antibiotic’ zinavyoendelea kukosa umaarufu. Tuliongelea sababu zake na tukaweka wazi suluhisho kwa kipindi hiki cha mpito ni kuupa mwili mlo sahihi ili kujijengea wenyewe kinga na tiba ya maradhi takribani yote duniani.
Wasomaji wengi walipiga simu wakitaka kujua mlo sahihi ni upi hasa. Kula vyakula vyenye asili ya mimea na hasa vile ambavyo havipitii jikoni na kuchomwa na moto kabla ya kuliwa ndiyo sahihi na muhimili mkuu wa tiba na kinga ya maradhi anayougua binadamu, yakiwemo yale sugu kama kifua kikuu, saratani za aina tofauti, shinikizo la damu, kupooza, ganzi na hata kisukari.
Kitaalamu, ukikaa mezani kula mlo wa asubuhi, mchana, na hata jioni, hakikisha asilimia 75 ya mlo wako ni vyakula ambavyo havijapikwa kama vile kachumbari, matunda, mboga za majani zilizochemshwa tu, mbegu kama korosho, karanga n.k.
Tafiti nyingi duniani zimethibitisha kuwa kadiri mtu anavyoongeza vyakula visivyopikwa na kupunguza vile vilivyopikwa ndivyo kinga ya mwili inavyozidi kuimarika na kuifanya ngozi ya mwili kunawiri pia.

Vyakula visivyopikwa au vyakula hai hupitisha vizuri virutubisho mwilini pamoja na tindikali muhimu kwa binadamu toka ardhini wakati vile vinavyopikwa huwa vimekufa na pengine huwa sumu mwilini kwa kuwa havina uwezo wa kuyeyuka na kujifyonza virutubisho mwilini haraka kwa kukosa ‘enzeymes’ muhimu ambazo huungua jikoni.
Kila aina ya chakula chenye asili ya mimea kimeumbwa kwa mchanganyiko wa kipekee na ladha tofauti, ila karibu vyote vina ‘enzeymes’ ambao huharakisha ufyonzaji wa virutubisho na husaidia kutoa taka na sumu mwilini haraka zaidi. Ukila vyakula ambavyo maandalizi yake hayahusishi moto basi ndani ya miezi mitatu utaweza kubaini mabadiliko.
Utafurahia mng’aro wa ngozi, utaboresha mfumo wa uyeyushaji chakula mwilini, maradhi ya gesi tumboni pamoja na sumu nyingi mwilini huondoka, utaudhibiti uzito kama ulikuwa unaongezeka na utapunguza uzito kwa kiwango kikubwa kama tayari uzito ulikuwa ni tatizo kwako.
Aina nyingi za mboga za majani hupikwa ili tupate ladha na kuua wadudu waliyomo, hivyo tunashauriwa tusizipike kwa moto unaozidi nyuzi joto 47 kwa kuwa joto zaidi ya hapo litaua virutubisho vyote. Maziwa pia yanatakiwa yachemshwe vema ili kuua vijidudu.
Ni vizuri kujenga mazoea ya kula chakula pamoja na kachumbari kila mara, ambayo mara nyingi huwa ni mchanganyiko rahisi tu wa vitunguu, nyanya, ndimu na pilipili. Vinaweza kuonekana siyo muhimu kiafya, lakini ukweli ni muhimu sana kwa mwili.
Kutokana na mazingira na sababu mbalimbali, mtu unaweza kukosa fursa ya kula matunda, lakini wanasayansi wameturahisishia kwa kuweka virutubisho vipatikanavyo kwenye matunda na mboga.

Tatizo kubwa lililopo nchini Tanzania ni kukosekana kwa uelewa wa kutosha kuhusu vidonge lishe (Food Supplements), kutopatikana kirahisi na kwa bei anayoweza kuimudu mtu wa kipato cha chini.
Wenye maduka ya dawa baridi na zahanati nchini wanashauriwa kuweka vidonge lishe pia sehemu zao za tiba ili kuwarahisishia watu upatinaje wake, sisi pia kama chombo cha habari tuko tayari kusaidiana na wadau hao kuelekezana upatikanaji wake, halikadhalika msomaji usisite kuwasiliana nasi kwa lolote.

               

Comments

Popular posts from this blog