Posts

HURUMAA...MZEE GURUMO ASTAAFU MUZIKI..AMWAGA CHOZI ASEMA HANA HATA BAISKELI

Image
Mzee Muhidin Gurumo (katikati) akizungumza na wanahabari wakati akitangaza kustaafu rasmi kazi ya muziki katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni mdau wa muziki Juma Mbizo na Meneja wa Msondo Ngoma, Said Kibiriti (kushoto). (Picha na Magreth Kinabo). Mwanamuziki mkongwe wa bendi ya Msondo Ngoma Mzee Muhidin Gurumo leo amestaafu rasmi kazi ya muzika alioifanya kwa muda wa miaka 53. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mzee  Gurumo mwenye umri wa miaka 73 amesema ameamua kustaafu kazi hiyo kwa hiari yake mwenyewe kutokana na umri wake kuwa mkubwa. Mzee Gurumo amesema “Muziki kwangu umekuwa kama asili yangu na kazi yangu lakini nimeamua kustaafu kutokana na umri wangu na nitabaki kuwa mshauri tu kwa mwanamuziki yeyote atakayetaka ushauri wangu”. Pamoja na kufanya kazi ya muziki Gurumo amesema kuwa hakupata mafanikio makubwa zaidi ya kujenga nyumba anayoishi na familia yake. Amesema ameimba kwa muda m...

WAZIRI MKUU PINDA AFUNGUA KONGAMANO LA UWEKEZAJI MANYARA

Image
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama asali wakti alipotembela Banda la Halmashauri ya Wilaya Mbulu  kabla ya kufungua kongomano la  Kwanza la  Uwekezaji katika mkoa wa Manyara  mjini Babati  Agosti 22, 2013.  Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dr, Mary Nagu na Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, Erasto Mbwilo.(Picha na Ofisi  ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama asali wakti alipotembela Banda la Halmashauri ya Wilaya Mbulu  kabla ya kufungua kongomano la  Kwanza la  Uwekezaji katika mkoa wa Manyara  mjini Babati  Agosti 22, 2013. (Picha na Ofisi  ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akitazama  mbolea  wakati alipotembelea  banda la kiwanda cha Mbolea cha Minjingu  kabla ya kufungua Kongamano  la Kwanza  la Uwekezaji  katika  Mkoa wa  Manyara mjini Babati Agosti 22, 2013. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Man...

Rais Museveni afunguka asema masomo ya ‘Arts’ yanachangia ongezeko la wahitimu wasio na ajira.

Image
  Rais Museveni wa Uganda amewakosoa wataalam wa elimu nchini humo kwa kuhamasisha masomo ya ‘Arts’ ambaye amedai yanachangia kuwepo kwa kiwango kikubwa cha wahitimu wa Vyuo Vikuu wasio na ajira. Akizungumza katika Sherehe za Shule ya Msingi ya Mchanganyiko ya Ibanda katika mji wa Ibanda, rais Museveni amesema katika miaka iliyopita aliwaambia wataalam wa elimu na wasomi kutoa muongozo wa fani na pia kuhamasisha masomo ambayo yanauzika, lakini hawakumsikiliza. Badala ya kuhamasisha masomo ya sayansi, rais Museveni amesema mameneja wa vyuo na taasisi za elimu waliwaacha wanafunzi kuendelea kusoma kozi zisizo na soko kama ‘Jinsi ya Kutatua Migogoro’ na ‘Saikolojia’. Aidha amewaasa wanafunza kuwa na nidhamu na kuepuka ngono katika umri mdogo, na kuongeza kuwa wanahitaji kuchanganya euelewa wa elimu ya asili nay a kisasa ili waweze kufanikiwa kimaisha. PATA MATUKIO YOTE HAPA:NAKUOMBA LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK ...

LIYUMBA MAJI SHINGONI TENA,MKE WAKE AMPANDISHA KIZIMBANI

Image
Amatus Liyumba. Mke wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu (BoT), Amatus Liyumba, Aurelia Ngowi amefungua kesi ya madai akipinga mumewe kuuza mali za familia na kumfukuza kwenye nyumba wanayoishi. Aidha,  anaiomba Mahakama iamuru yeye na watoto wake waendelee kuishi kwenye nyumba hiyo, hadi shauri hilo litakapokwisha. Mama huyo anadai Liyumba aliwafukuza na kuweka walinzi ili wasiingie kwenye nyumba hiyo. Kesi hiyo imefunguliwa mbele ya Hakimu Mkazi Jackline Rugemalila katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam. Katika hati ya madai, Aurelia anaiomba Mahakama iweke zuio la muda ili Liyumba asiuze mali za familia, pia asiuze nyumba iliyopo Africana Mbezi Beach, katika kiwanja namba 2232/2233 ambayo walikuwa wanaitumia kama makazi ya familia. Aurelia ameiomba Mahakama iamuru waendelee kuishi katika nyumba hiyo wakati shauri hilo likiendelea pia mshitakiwa alipe gharama za uendeshaji wa kesi....

WATU SABA WANUSURIKA KWA AJALI YA NDEGE ILIYOTUA ZIWA MANYARA

Image
Ndege ndogo ya shirika la Tanzanair iliyokuwa ikitokea mjini Bukoba mkoani Kagera kwenda Dar ss Salaam imelazimika kutua kwa dharura katika ziwa Manyara baada ya injini yake moja kuzimika ghafla ikiwa angani.  Ndege hiyo ilikuwa na abiria sita na rubani mmoja ambapo wote wamejeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Seliani mjini Arusha kwa matibabu. Chanzo: ITV

MKUU WA FFU - ARUSHA NA POLISI WENGINE WATATU WAFUKUZWA KAZI

Image
Imeandikwa na Lydia Churi — Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewavua madaraka Maafisa wanne wa Jeshi la Polisi nchini na kumsimamisha kazi mmoja ambaye atafunguliwa mashtaka ya kijeshi kutokana na kukiuka maadili na taratibu za jeshi hilo. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Waziri Nchimbi amesema hatua hiyo ni katika kuendeleza vita ya kuhakikisha kuwa jeshi la polisi linakuwa na nidhamu, linatekeleza wajibu wake wa kutenda haki na kuwalinda raia na mali zao. Alisema amewachukulia hatua Maafisa hao baada ya kuridhia maoni ya kamati aliyoiunda kufanya uchunguzi wa matukio yaliyolalamikiwa dhidi ya askari polisi katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro na Kigoma kati ya Desemba 2012 na Mei, 2013. Waziri Nchimbi aliwataja waliovuliwa madaraka kuwa ni Mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoani Arusha Mrakibu wa Polisi Ramadhan Giro, Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro Inspekta Jamal Ramadhan, ...

MANAIKI SANGA ATIWA MBARONI.....PICHA ZA UCHI ZIMEMPONZA....HIZI NI PICHA ZINGINE 400 AKIWA MTUPU

Image
    Jeshi la polisi kanda ya Dar es Salaam linadaiwa kumtia mbaroni msanii anaetuhumiwa kupiga picha chafu na wanawake mchanganyiko wakiwema mamiss maarufu na baadae kusambaza kwenye mitandao yote ya kijamii pamoja na kuripotiwa kwenye magazeti mbalimbali   Mwandishi wetu amefanikwa  kuzinasa  picha  za  Manaiki  akiwa chini ya ulinzi wa  polisi huku akiwa amevishwa pingu na kurukishwa kichurachura.   Habari za uhakika zilizonaswa  zinasema kuwa msanii huyo alikamatwa siku chache baada kuvuja kwa picha zake za aibu zikimuonesha akiwa na wanawake tofauti tofauti.   HIZI  NI  PICHA  ZAKE  NYINGINE  400  AKIWA  MTUPU  NA  MADEMU  ZAKE..... << PICHA, BOFYA  HAPA>>

POLISI FEKI 7 WANASWA TENA....

Image
SIKU chache baada ya kukamatwa kwa askari feki wa usalama barabarani, Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imewakamata watuhumiwa saba wa ujambazi, wakiwa na sare za Polisi, huku mwingine akijifanya ofisa Usalama wa Taifa.   Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaa, Suleiman Kova alisema watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na sare za Polisi jozi mbili. Watuhumiwa hao ni Khamis Mkalikwa (40), Magila Werema (31), Nurdin Bakari (46), Materu Marko (32), Louis Magoda (34), Amos Enock (23) na Amiri Mohammed (45), wote wakazi wa jijini Dar es Salaam.   Sare hizo, kwa mujibu wa Kamanda Kova, ni zenye cheo cha Sajenti wa Kituo, huku jozi moja ikiwa na jina linalosomeka SSGT A.M Mduvike.   Watuhumiwa hao walikamatwa jana katika eneo la Kiluvya, baada ya askari kuweka mtego, ambao ulifanikiwa kuwanasa.  Alisema watu hao walikuwa wakitumia silaha, sare za jeshi la Polisi na redio ya m...

RWANDA NA UGANDA WAJITOA BANDARI YA DAR ES SALAAM

Image
Chama cha Wasafirishaji wa Mafuta Tanzania (Tatoa), kimesema Rwanda na Uganda zitajitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam kuanzia Septemba Mosi, mwaka huu. Katibu Mtendaji wa Tatoa, Zacharia Hanspope aliwaambia waandishi wa habari jana baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuwa nchi hizo zinajitoa kutokana na matatizo mbalimbali ambayo kwa muda mrefu zimekuwa zikiyalalamikia lakini Serikali haikuchukua hatua. Hanspope alisema ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ni baadhi ya vikwazo ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa kwa muda mrefu na wafanyabiashara mbalimbali wa nchi hizo. “Serikali ipunguze gharama za ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ili kuwa na ushindani sawa na bandari nyingine na hivyo kuzivutia kutumia Bandari ya Dar es Salaam,” alisema Hanspope. Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo alikataa kuzungumzia lolote kuhusu suala hilo akisema halina mantiki yoyote kwake.... “Hivi hilo jambo unaloniuliza lina sense (mant...

MFANYABIASHARA ALIYEJIREKODI AKIMLAWITI MFANYAKAZI WA DUKANI AKAMATWA

Image
JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro limemkamata mfanyabiashara mashuhuri wa mjini Moshi, Totolii Kimath anayedaiwa kurekodi mkanda wa video ukimwonyesha akimlawiti mfanyakazi wake wa dukani.   Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, aliliambia Tanzania Daima kuwa kijana huyo ambaye anamiliki maduka ya kuuza na kutengeneza CD katika kituo kikuu cha mabasi cha mjini Moshi, alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), akitokea Dubai.   Alisema Jeshi la Polisi lilikuwa likifanya uchunguzi kwa muda mrefu wa picha zilizosambaa katika mitandao ya kijamii na simu ambazo zinaonyesha mwanaume na mwanamke wakifanya mapenzi kinyume cha maumbile.   “Tulikuwa tunafanya uchunguzi wa picha zilizosambaa kwenye mitandao pamoja na simu kwenye Whatsapp ambazo zinaonyesha watu wakifanya mapenzi kinyume cha maumbile, kimsingi ni kosa la jinai mwanamke kumruhusu mwanaume amuingilie kinyume cha maumbile ama mwanau...

KWELI NAWEZA SEMA SAFARI SIO KIFO ILA.......................

Image
  Tazama maisha ya Mtanzania yanavyozidi kuwa hatiani kila kukicha, hapa nia abira wakionekana kugombania usafiri na wengineo wakiwa wako juu ya keria ili mradi tu wafike waendako. JE NAULI INALIPWA KWA WOTE? Uko nchi ya jirani Kenya nako hali ya usafiri imekuwa ngumu kila kukicha, hawa nia abiria waliokutwa na kamera zetu wakiwa wamejazana kwenye matatuu nao hitaji lao ikiwa nikufika waendako bila kujali uasalama wa maisha yao

RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AFANYA MABADILIKO MAKATIBU WAKUU

Image
NA MAGRETH   KINABO NA ELEUTERI MANGI – MAELEZO RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya uongozi katika ngazi za juu za utendaji wa Serikalini kwenye nafasi za makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu katika wizara mbalimbali, ambapo  wapo waliohamishwa, wataopangiwa kazi nyingine na yumo anayestaafu.  Kauli hiyo ilitolewa leo jioni na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. “Rais amefanya mbadiliko haya kwa lengo kuu la kuimarisha utendaji wa kazi za Serikali  katika ngazi hizo za juu,”alisema Balozi Sefue.  Mabadiliko yaliyofanywa kwa upande wa makatibu wa wakuu ni kama ifuatavyo; Dk. Florens Turuka amekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, awali alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Joyce Mapunjo Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika...

ANGALIA PICHA ZA MAZISHI YA PHILIP MANGULA

Image
Mwakilishi wa Mheshimiwa Rais katika mazishi ya Nemela Mangula Mh. Anne Makinda akiwa ameongozana na Mh. Wassira na viongozi wengine wakipitia wosifu wa marehemu pamoja na ratiba za mazishi. Wana familia na waombolezaji wakiwa katika hali ya huzuni. Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia wakiwa wamebeba mwili wa Marehemu Nemela Mangula,mkoani Njombe.  Jeneza la Neema Philip Mangula  Watumishi wa CCM Makao Makuu wakibadilishana mawazo na Viongozi wa Dini wakati wa mazishi ya Neema Mangula. Mahala ulipopumzishwa mwili wa Neema Mangula.

MUUMINI NA WAZIRI SONYO WACHAPANA MAKONDE NA KUTAKA KUPIGANA VISU LIVE WAKIWA MAZOEZINI KWENYE BENDI

Image
WANAMUZIKI wawili wenye majina ya kutisha, Waziri Sonyo na Rais wa zamani wa bendi ya Victoria Sound, wamepigana katika mazoezi ya bendi yao yaliyofanyika Mbagala, jijini Dar es Salaam.    Waziri Sonyo kushoto. Katika kichapo hicho, inadaiwa kuwa Sonyo nusura amchome Muumini kisu, hivyo kuzua hofu katika patashika ya aina yake inayoendelea kuonyesha mgogoro mkubwa kati ya wanamuziki hao ndani ya Victoria Sound. Akizungumza muda mchache baada ya kadhia hiyo, Muumini alisema alishangaa kujikuta yupo chini na Sonyo akiwa ameshatoa kisu kutaka kumjeruhi. Muda mchache baadaye Muumini aliandika kwenye mtandao wa kijamii akielezea tukio hilo alilodai ni la aina yake huku akitumia lugha kali za kuudhi dhidi ya Sonyo. “Leo ndio nimedhihirisha huyu ( hapa kuna tusi ila limefichwa kwa sababu za kiungwana) ni kweli yy amenikuta nimekaa tena pembeni na tahadhali zote ila alivyokuja kwangu kunivamia sik...

ANGALIA PICHA ZA MAPOKEZI YA FEZZA KESSY NCHINI BOSTWANA

Image
Akiwa Katika Gari la wazi mara baada ya kupokelewa uwanja wa Ndege wa Bostwana..

AJALI YA LORI NA GARI NDOGO MOROGORO

Image
Gari Aina ya Prado tz ikiwa imepata ajali kwa kugongwa la lori la mizigo jana usiku Maeneo ya Nane Mkoani Morogoro.Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo ni kwamba Chanzo Cha Ajali hiyo ni Uzembe wa Dereva wa Gari ndogo aina ya Prado iliingia barabara kuu bila kuangalia pande zote kama kuna gari nyingine na ndipo alipoingia na kukutana la Lori La Mizigo likiwa kwenye Mwendo kasi na ndipo lilipoligonga gari hilo.Kwenye Gari Dogo alikuwa dereva Mwenyewe Hakuna Mtu Aliyepoteza maisha. Mashuhuda wa ajali hiyo wakiwa eneo la tukio wakiliangalia gari hilo lililopata ajali Eneo la Nane nane Mkoa wa Morogoro jana usiku.Picha na   MATUKIO NAMICHAPO BLOG Picha ya gari hilo mara baada ya kuondolewa eneo la tukio na hivi ndiyo lilivyoharibika baada ya Ajali Hiyo Askari Polisi wakiwa Eneo la tukio muda Mfupi Mara baada ya ajali hiyo kutokea Askari wa usalama barabarani akiwa e...

ANGALIA PICHA YA BINADAMU MWENYE KILO 610 APELEKWA RIYADH, SAUDI ARABIA KWA UPASUAJI

Image
Khalid Mohsen akishushwa toka ghorofa ya pili kwa folklift nyumbani kwake mjini wa Jazan nchini Saud Arabia kwa ajili ya kupelekwa Kwenye Hspitali ya Riyadh mji mkuu wa Saudi Arabia kwa upasuaji Khalid Mohsen akiwa kwenye Folklift kupelekwa uwanja wa ndege tayari kusafirishwa Riyadh, mji mkuu wa nchi hiyo kwa ajili ya upasuaji.   Khalid Mohsen akiingizwa kwenye ndege kutumia Folklift.  Khalid Mohsen akitolewa kwenye tolitoli mara baada ya kuwasili Hospitali ya Riyadh