Posts

MSEMAJI WA SIMBA HAJI MANARA AFUTIWA ADHABU YA TFF

Image
Haji Manara. KAMATI ya Nidhamu ya  Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) , chini ya mwenyekiti wake, Tarimba Abass, leo Jumatatu imefikia uamuzi wa kumfutia adhabu  Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba ,  Haji Manara. Kamati hiyo imefikia uamuzi huo baada ya  Manara  kuomba kupitiwa upya adhabu aliyopewa hapo awali ya kufungiwa kutojihusisha na soka kwa kipindi cha miezi 12 na kulipa faini ya Sh milioni 9. Kutokana na kufutwa kwa adhabu hiyo, Manara kuanzia leo atakuwa huru kuendelea kufanya majukumu yake ya soka ndani ya Simba. Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Tarimba Abbas akizungumza na wanahabari leo mchana ikiwa ni maamuzi waliyoyafikia ya kamati ya nidhamu na kuwafungulia baadhi ya wanafamilia wa mpira waliokuwa wamefungiwa kujihusisha na mpira ndani na nje ya nchi. Mbali na Manara, kamati hiyo pia imewafutia adhabu Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Rukwa, Blassy Kiondo, Mwenyekiti wa Kamati ...

Rais Magufuli kuzindua miradi tisa ya barabara na uwanja wa ndege.

Image

DAR: Watuhumiwa 250 Mbaroni, Wamo wa Madawa ya Kulevya

Image
Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum DCP, Lucas Mkondya akiwaonyesha wanahabari bangi zilizokamatwa na jeshi hilo. JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limesema kuwa limefanikiwa kuwatia nguvuni watuhumiwa 250 kwa makosa mbalimbali ya kihalifu yakiwemo ya kukutwa na madawa ya kulevya. Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, DCP Lucas Mkondya ameeleza kuwa watuhumiwa hao walikamatwa kupitia msako mkali kuanzia Julai 16, hadi leo Julai 17 ambapo watuhumiwa hao walikamatwa. Mkondya amesema, miongoni mwa makosa waliyokamatwa nayo watuhumiwa hao ni pamoja na kupatikana na madaya ya kulevya, unyang’anyi wa kutumia silaha, utapeli na kucheza kamari. Aliongeza kuwa upelelezi wa makosa hayo ukikamilika, watuhumiwa watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria. NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

JK amfuta Machozi Mwakyembe

Image
RAIS Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete amefika Nyumbani kwa Dk Harrison Mwakyembe kumfuta Machozi kutokana na Msiba wa Mke wake Linah Mwakyembe. Kikwete alifika Msibani hapo saa sita  mchana  "Mwakyembe ni rafiki yangu wa siku nyingi, hata wakati mama anaumwa aliniambia na nilienda kumjulia hali alipokuwa Muhimbili, nimtake awe mvumilivu tunajua ana majonzi msiba huu ni wetu sote," amesema. Wengine waliofika kumfariji Dk Mwakyembe ni Jaji Mstaafu Damian Lubuva, ambaye pia alimjulia hali Linah wakati akiwa hospitali. "Mwezi uliopita nilienda Aga Khan kumuona mgonjwa mwingine lakini nikakutana na Mwakyembe, akaniambia mkewe amelazwa nikaona si vibaya kwenda kumjulia hali na alikuwa anaonyesha matumaini," amesema. Wengine waliofika kumfariji Dk Mwakyembe ni Spika wa Bunge mstaafu, Anne Makinda; Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji; Waziri wa Ulinzi, Dk Hussein Mwinyi; Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga na viongozi wengine ...

STAA DIAMOND PLATNUMZ,BABU TALE NA MKUBWA FELLA WAKIWA MSIBANI KWA WAZIRI MWAKYEMBE

Image
Mwimbaji wa Bongofleva  Diamond Platnumz,   Mameneja wake  Said Fella  na  Babu Tale ni miongoni mwa mastaa wa Bongo waliofika nyumbani kwa Waziri wa Habari  Dr.  Mwakyembe  kutoa pole kufuatia kifo cha Mke wake  Linah George.

PICHA: KELVIN YONDANI APATA JIKO RASMI

Image
TAARIFA njema ikufikie popote ulipo kuhusu beki kisiki wa  Yanga, Kelvin Patrick Yondani  ambaye ameamua kuachana na ukapera. Mkali huyo alianza kwa  Send Off  kisha akamalizia mambo na mzazi mwenzake ambaye ameishi naye miaka mingi. Yondani anaingia kwenye orodha moja na wanasoka kama Emmanuel Okwi, Ibrahim Ajib, Mwinyi Kazimoto ambao ni wanacheza Ligi Kuu Tanzania Bara. Hongera Yondani kwa kuamua kufanya kweli.

Wanafunzi 10 wafutiwa matokeo ( Kidato cha sita) kwa Udanganyifu

Image
Wanafunzi 10 wamefutiwa matokeo yao baada ya kufanya udanganyifu kwenye mtihani wa Kidato cha sita  Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Necta Dk Charles Msonde  amesema  kuwa kati ya watahiniwa hao kumi, saba ni wa shule na watatu ni wa kujitegemea.  Pamoja na hao kumi, matokeo ya watahiniwa wengine 15 yalizuiliwa kwa kuwa hawakufanya mitihani ya baadhi ya masomo.  Watahiniwa hao walishindwa kufanya mitihani kutokana na matatizo mbalimbali ikiwamo ya kiafya na hivyo kushindwa kufanya baadhi ya mitihani hiyo. ‘Watahiniwa hao wamepewa fursa ya kufanya mitihani ya kidato cha sita, Mei 2018 kama wa watahiniwa wa shule,” imesema taarifa ya Dk Msonde. Pia, wapo watahiniwa 69 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mitihani yote, wamepewa fursa ya kufanya mitihani hiyo, Mei 2018. Wanafunzi 10 wamefutiwa matokeo yao baada ya kufanya udanganyifu kwenye mtihani wa Kidato cha sita  Katibu Mt...

Simba Kuna Makinikia - Wazee Simba

Image
Wazee wa Klabu ya Simba wametuhumu uongozi wa Klabu hiyo kikihuumu Klabu hicho na kwamba wamemtaka rais John Magufuli kuingilia kati hujma hizo. Wakizungumza na Waandishi wa habari leo wazee hao wameeleza kuwa hujuma hizo zinatokana na Uchu wa madaraka na tamaa ya fedha kwa viongozi hao. Felex Makuwa Mratibu wa wazee hao ameeleza kuwa Serikali kupitia Mamlaka zake iwakamate wahusika na Iwachukulie hatua  

BREAKING NEWS : ANGALIA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA ACSEE 2017

Image
  Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokoe ya mtihani wa kuhitimu elimu ya sekondari kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita. Bonyeza HAPA kufatilia matokea ya shule zote Tanzania. BOFYA HAPA KUYAONA

Profesa Jay Afunguka Wema Kukacha Harusi Yake

Image
Mbunge wa Mikumi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Haule ‘Profesa Jay’akifanya yake na mke wake Grace Mgonjo baada ya kufunga ndoa. BAADA ya Jumamosi iliyopita Mbunge wa Mikumi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Haule ‘Profesa Jay’ kufunga ndoa na mchumba’ke wa kitambo, Grace Mgonjo katika Kanisa la Mtakatifu Joseph lililopo Posta jijini Dar na sherehe kufanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, ameibuka na kufunguka suala la Miss Tanzania 2006/07, Wema Sepetu kuikacha harusi yake. Staa wa Bongo, Wema Sepetu. Taarifa za awali kutoka kwa chanzo makini zilieleza kuwa, Profesa Jay na Wema ambaye alihamia Chadema miezi kadhaa iliyopita wana bifu kali japokuwa haijulikani chanzo ni nini, ndiyo maana mwanadada huyo hakuhudhuria kwenye harusi hiyo. “Unajua Wema na Jay hawana uhusiano mzuri tangu ahamie kwenye chama hicho yaani wana bifu ndiyo sababu hata Wema hakuhudhuria kwenye sherehe ya harusi ya Jay...

CHAI, KARANGA NA MTINDI KWA HESHIMA YA NDOA!

Image
WAPENDWA wasomaji wangu, bila shaka mko poa mnaendelea vyema na majukumu yenu kama kawaida. Leo kwenye safu hii nitazungumzia umuhimu wa chai kwa mwanamke ili kudumisha uhusiano wako na ndoa kwa ujumla. Nafanya hivi kwa kuwa, wengi wamejikuta wakipoteza ndoa zao kwa kupoteza mvuto na kupuuzia mambo madogomadogo. Sasa leo nakupa tipu juu ya namna chai ya rangi, maziwa ya mtindi, karanga na supu ya pweza vinavyoweza kuinogesha ndoa yako hasa katika eneo la faragha. Mwanamke fanya hivi; kunywa chai kutwa mara tatu. Kumbuka kazi ya chai ni kukupatia joto mwilini. Ukijua kuwa muda wa kukutana na mwenza wako faragha unakaribia, pata kikombe chako cha chai ya moto kisha jirushe uwanjani uone mechi itakavyokuwa bomba. Chai hiyo itakupa nguvu na hivyo kuweza kumudu mikikimikiki ya mwenza wako. Na nikuambie tu kwamba, ukiwa umepata chai yako hiyo, neno; ‘nimechoka mume wangu’ haliwezi kuwepo, labda achoke yeye. Unaachaje sasa kuitumia chai ambayo hata haina kazi kuiandaa ...

Diwani Chadema Mbaroni kwa Tuhuma za Rushwa

Image
Diwani Kata ya Msigani, Ubungo, Israel Mushi ( 48 ) na Mrasimu ramani wa Manispaa ya Ubungo, Francis Mwanjela Peter ( 28 ) wamekamatwa na Tasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),wilaya ya Kinondoni kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa  Sh.5,000,000/=. kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa  TAKUKURU wilaya ya  Kinondoni Teddy Mjangira, amesema kuwa Watuhumiwa walikamatwa Julai 12, 2017 baada ya kupokea kiasi hicho cha fedha toka kwa mwananchi ambaye jina lake limehifadhiwa na ambaye mbali na kutoa kiasi hicho cha pesa alitakiwa  na watuhumiwa kuwapa  rushwa ya Sh.10,000,000/= Inadawaiwa Watuhumiwa walishawishi na kupokea rushwa ili waweze kutoa ushawishi kwa wajumbe wa kamati ya mipango miji  inashughulikia maombi ya kubadilisha michoro, kubadilisha matumizi ya kiwanja na kupitisha kibali cha ujenzi katika Manispaa ya Ubungo. Uchunguzi wa tuhuma unaendelea na Watuhumiwa ambao wanatuhumiwa kutenda makosa k...

Majaliwa Amkalia kooni Mkurugenzi Lindi

Image
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Lindi, Samuel Warioba Gunzar leo alijikuta katika wakati mgumu mbele ya waziri mkuu wa Jamuhuri ya Tanzania, Kassim Majaliwa baada ya kukutana na maswali mzito mfululizo kutoka kwa kiongozi huyo wa juu wa nchi.  Hayo yamejiri katika mji mdogo wa Mtama kwenye mkutano wa hadhara uliokuwa umefurika mamia ya wananchi. Hali ilikuwa mbaya kwa Gunzar kutokana na taarifa iliyotolewa na mbuge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye aliyekueleza waziri mkuu kwamba katika mji huo mdogo in unaokadiriwa kuwa na wakazi takribani 4000 hauna kituo cha afya.  Maelezo ya Nape yalisababisha waziri mkuu amuite mkurugenzi huyo aeleze nikwanini eneo hilo lisiwe na kituo cha afya wakati linaidadi kubwa ya watu. Huku akihoji kwanini imekuwa hivyo wakati kuna madiwani na watendaji katika halmashauri hiyo.  Alisema sera ya afya ipo wazi nasifa za kuwa na zahanati, vituo vya afya na hospitali zinafahamika. "Mkurugenzi  njoo utuele...

Usher Raymond atembelea mbuga ya Serengeti

Image
Usher Raymond Msanii wa Marekani Usher Raymond yuko ziarani nchini Tanzania akitembelea eneo la uhifadhi wa wanyama pori la Serengti National Park. Bwana Raymond alichapisha baadhi ya picha akiwa na familia yake katika akaunti yake ya Twitter. Alielezea hali ilivyo katika eneo hilo kama ya kufurahisha . Ripoti za Usher Raymond kuzuru Tanzania zilisambaa kwa haraka nchini humo. Watu wengine maarufu akiwemo mchezaji wa zamani wa Manchester United na Real Madrid David Becham, aliyekuwa mchezaji wa Liverpool Mamadou Sakho, mchezaji wa Everton Morgan Schneiderlin ni miongoni mwa wale waliozuri katika sehemu mbali mbali za kitalii nchini humo mwaka huu. Vivutio vya kitalii nchini Tanzania kama vile mbunga ya uhifadhi wa wanyama pori ya Serengeti na mlima Kilimanjaro ni vivutio vinavyoongoza kwa utalii ambapo watu wengi maarufu wametembela.

ACACIA Yakubali Kulipa Mirabaha Iliyomo Kwenye Sheria Mpya Madini

Image
Balozi wa Canada nchini na Mwenyekti wa Barrick Gold Corporation (mmiliki mkubwa wa Acacia) Prof. Thornton wakiongea na waandishi wa habari Ikulu Dar. (Picha na Maktaba). Kampuni inayomiliki Makampuni ya Uchimbaji wa Madini ya ACACIA imesema italipa mirabaha iliowekwa katika sheria mpya za madini. Sheria mpya ya madini inawataka wawekezaji katka sekta hiyo kulipa asilimia 6 ya mirabaha ikiwa ni ongezeko la asilimia 2 zilizokuwepo awali, ambapo asilimia 1 ni kwaajili ya usafirishaji kwenda nje.

Umewaona mapacha wa Beyonce?

Image
Beyonce na mapacha wake. MWANAMUZIKI maarufu duniani, Beyonce Knowles kwa mara ya kwanza ameawaanika hadharani watoto wake mapacha ikiwa ni takribani mwezi mmoja baada ya kujifungua. Alichokiandika Beyonce Januari akiwa na mimba. Muimbaji huyo kupitia mtandao wa Instagram, ameonyesha kuwa watoto hao wana mwezi mmoja tangu wamezaliwa. “Sir Carter and Rumi 1 month today. 🙏🏽❤️👨🏽👩🏽👧🏽👶🏾👶🏾,” ameandika Queen Bey kwenye mtandao huo. Mapacha hao waliozaliwa ni mmoja wa kike na mwingine wa kiume na tayari walishapewa majina ya Sir na Rumi.

Taiwan: Wabunge Wavurugana Bungeni, Wachapana Live

Image
Wabunge wakizichapa kavukavu. WABUNGE wa Taiwan leo walichapana makonde, wakarushiana viti na mabaluni ya maji baada ya kutofautiana kuhusu mradi mmoja wa miundombinu. Tukio hilo ni mwendelezo wa matukio yaliyoanza jana ambapo katika kubishana, wabunge hao walikwidana mashati na kuchapana wakati wa kupitia bajeti ya mradi huo. Mpango huo ni moja ya miradi mikubwa iliyopendekezwa na Rais Tsai Ing-wen ambayo inajumuisha ujenzi wa reli za kutoa huduma ndogondogo, hatua za kuthibiti mafuriko na mazingira yanayosababishwa na viwanda. Hata hivyo, chama cha upinzani cha Kuomintang kinapinga mradi huo kikisema unapendelea miji na wilaya ambazo zinaunga mkono chama cha Democratic Progressive (DPP) ambako kina uhakika wa kuungwa mkono katika uchaguzi wa mikoa mwaka kesho. Isitoshe, wapinzani wanapinga kiasi kikubwa mno cha Dola bilioni 13.8 ambazo zitatumika katika mradi huo. Waziri Mkuu Lin Chuan alishindwa kutoa ripoti ya bajeti hiyo Alhamisi baada kutupiwa b...

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI YA MADAKTARI AFRIKA YA NCHINI MAREKANI WAFANYA MATIBABU YA MOYO KWA WAGONJWA KWA KUWEKA KIFAA MAALUM

Image
Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu kambi maalum ya matibabu ya Moyo inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Madaktari Afrika ya nchini Marekani kwa wagonjwa ambao mapigo yao ya moyo yako chini sana na hivyo kuwekewa kifaa maalum cha kurekebisha mapigo ili yawe sawa (kwa jina la kitaalamu Pacemaker) . Kushoto ni Daktari Bingwa na Magonjwa ya Moyo Mathew Sackett. Tangu kuanza kwa kambi hiyo mwanzoni wa juma hili jumla ya wagonjwa 20 wameshapatiwa matibabu kati ya hao nane wamewekewa Pacemaker na wengine wanne wanatarajia kuwekewa leo na kesho.  Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Madaktari Afrika ya Nchini Marekani Mathew Sackett akizungumza na waandishi wa habari na kuipongeza Serikali kwa uwekezaji mkubwa ulioufanya katika matibabu ya Moyo wakati wa kambi maalum ya matibabu ya Moyo inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana n...

Hakuna aliyekamilika, Cha Muhimu ni Kuvumiliana

Image
UHALI gani msomaji wangu! Ni matumaini yangu kuwa uko poa kabisa. Ni ijumaa nyingine nzuri ninayokualika kwenye uwanja huu, kwa wewe ambaye mambo yako hayaendi sawa, nakuombea kwa Mungu akufanyie wepesi. Mada yetu ya leo ni kama inavyojieleza, wapo baadhi ya watu ambao wao kamwe hawakosei, kila tatizo linapotokea basi wanawasukumia mizigo wenzi wao, wanaamini wao ni wakamilifu ila wenzi wao ndiyo wana matatizo. Ipo wazi kwamba uhusiano wa kimapenzi ni jambo ambalo linatakiwa kuwa la furaha, wewe na mwenzi wako muishi kwa upendo na amani, hata kama kunatokea misuguano, basi inakuwa ni ile ya kawaida ambayo mnaimaliza mapema, kwa amani na maisha yanaendelea. Kwa bahati mbaya, uhusiano wa kimapenzi wa watu wengi siku hizi, umejawa na migogoro, maudhi na karaha za mara kwa mara, hasa kwa wale wapenzi wanaoishi kwenye uhusiano wa kudumu, uwe ni uchumba au ndoa. Jambo ambalo watu wengi huwa hawalijui, ni kwamba amani, upendo na maelewano huwa haviji tu, ni lazima vij...

Malinzi ajiuzulu Urais TFF Akiwa Rumande

Image
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amejiuzulu wadhifa wake wa Ujumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA). Kupitia kwa wakili wake, kampuni ya Rwegoshora, Malinzi amewaandikia barua FIFA kuwataarifu kujitoa kwenye Kamati hiyo kutokana na kuwa mikononi mwa dola kwa sasa. Malinzi, pamoja na Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa na Mhasibu, Nsiande Isawafo Mwanga. wapo rumande hadi Julai 17, upepelezi wa kesi yao utakapokamilika baada ya kunyimwa dhamana Julai 3 katika kesi inayowakabili. Watatu hao walipandishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa mara ya kwanza Juni 29 na kusomewa mashitaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF iliyopo katika banki ya Stanbic, Dar es Salaam. Katika mashitaka hayo, 25 yanakwenda moja kwa moja kwa Rais wa shirikisho hilo, Malinzi akidaiwa kughushi michakato mbalimbali ya kifedha, huku matatu yakiwahusu wote na Katibu wake na Mhasibu wake Nsiande Isaw...