JPM Kubadili Noti Kuwakomoa Walioficha Mabilioni Majumbani
Rais John Magufuli amewataka watu walioficha fedha majumbani kuziachia ziingie kwenye mzunguko vinginevyo anaweza kuamua kuzibadili ili wakose mahali pa kuzipeleka. Amesema watu hao wamekuwa na utaratibu wa kutoa fedha zao katika benki na kuzificha kwa kuogopa kuwa atabaini kiasi walichonacho, hivyo akawataka kuachana na tabia hiyo kwa sababu fedha hizo ni mali yao. Akizungumza katika mkutano wa 14 wa mwaka wa wahandisi uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jana, Rais Magufuli aliyetumia dakika 73 kuzungumza na wahandisi hao na kueleza mikakati na changamoto zinazoikabili Serikali ukiwamo wizi na ufisadi, alisisitiza; “Huu ujumbe ni kwa wale wanaoficha fedha, waziachie na wajiandae, naweza kuamua baada ya siku mbili tatu nabadilisha fedha na hizo zilizofichwa katika magodoro ziozee huko. Ni nafuu mzitoe mziweke katika mzunguko zikafanye kazi,” alisema. Katika mkutano huo uliohudhuriwa na mawaziri, naibu mawaziri, makatibu wakuu na wahandisi kutoka ndani