Acer Yazindua Laptop Yenye Kikoo Kilichopinda

accer
Kampuni ya Vifaa vya kielektroniki ya Acer imezindua laptop ya kwanza yenye kioo kilichojipinda.
Acer inasema kuwa uvumbuzi huo utaiwezesha kucheza michezo ya video.
Televisheni kadhaa pia zimetumia uvumbuzi huo,lakini umezua mgawanyiko kwa kuwa una umuhimu na ubaya wake.
accer 2
Kampuni hiyo ya Taiwan pia ilitangaza kwamba imefanikiwa kupata teknolojia ya pet katika mkutano na wanahabari mjini Berlin.
Kampuni kadhaa za kielektroniki ikiwemo Samsung, Lenovo, DJI, Sony na Huawei zinatarajiwa kuzindua sura mpya ya laptop zake katika maonyesho ya kiteknolojia ya Ifa katika Mji Mkuu wa Ujerumani wiki hii.
Laptop hiyo ina kioo kikubwa ikilinganishwa na laptop ya kawaida ya Acer,lakini ni umbo lake ambalo liliifanya kampuni hiyo kudai kuwa ya kwanza kuzinduliwa duniani.

Comments

Popular posts from this blog