Posts

BREAKING NEWZZ….MAPAMBANO MAKALI KATI YA POLISI NA MAJAMBAZI MUDA HUU HUKO VIKINDU.

Image
Picha na Maktaba Mapigano makali yanaendelea kati ya polisi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi eneo la Vikindu, wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani. Timu ya Mwananchi iliyo eneo la tukio imeshuhudia magari ya polisi (defenda) zaidi ya 16 yakifika eneo la tukio huku polisi wakiwa wameshika silaha zao kwa umakini mkubwa. Kadhalika, magari yanayokwenda maeneo ya Vianzi Mkurang, Malela, Pemba Mnazi, Mfuru zimefungwa kutokana na mapambano hayo. Mapigano makali yanaendelea kati ya polisi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi eneo la Vikindu, wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani. Timu ya Mwananchi iliyo eneo la tukio imeshuhudia magari ya polisi (defenda) zaidi ya 16 yakifika eneo la tukio huku polisi wakiwa wameshika silaha zao kwa umakini mkubwa.

Salama: Nilimdis MwanaFA, Akanimaindi Kinoma!

Image
Salama Jabir. U KIAMBIWA umtaje Muasisi wa Kipindi cha Planet Bongo cha EATV ambacho enzi ana-kifanya kilicha-ngia ubora wa video za Muziki wa Bongo Fleva nchini kukua kutokana na kasumba yake ya kuzikosoa bila woga, moja kwa moja utamtaja Salama Jabir ‘EceJay’. Pia ukikutana naye, Salama ni mcheshi, mtundu na ana ufahamu mkubwa katika masuala ya burudani. Kama ulishawahi kufuatilia Vipindi vya Mkasi, Ngazi kwa Ngazi na Shindano la Bongo Star Search (BSS) namna ya uulizaji wake wa maswali kimtego utaku-baliana nami. Mwi-shoni mwa wiki iliyo-pita, Salama alifa-nyiwa maho-jiano katika Kipindi cha The Playlist cha Omary Tambwe ‘Lil Ommy’ kinachorushwa kupitia Radio Times FM na katika makala haya yanaanika mahojiano hayo; Ommy: Ngoma yako unayoikubali zaidi ni ipi? Salama: Ahahaa! Jana (Ijumaa) ujue nilikuandikia meseji, sasa nilikuwa nimeshiba kichizi na nilikuwa nimekaa kwenye kikochi changu f’lan hivi cha tafakuru ambacho ukikaa lazima madini yashuke! ...

Mbatia: Rais Apeleke Muswada Bungeni Kufuta Vyama vya Siasa

Image
    Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi Taifa, James Francis Mbatia (wa pili kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani). Mbatia (wa pili kushoto) akionesha hisia zake mbele ya wanahabari. Mkutano ukiendelea. Wanahabari wakichukua tukio hilo leo Agosti 25, 2016. Baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wakisikiliza maswali kutoka kwa wanahabari. NA DENIS MTIMA MWENYEKITI wa Chama Cha NCCR Mageuzi Taifa, James Francis Mbatia amemtaka Rais Dk. John Pombe Magufuli kupeleka muswada bungeni katika kikao kijacho cha Bunge ili kuandaa sheria ya kuvifuta vyama vyote vya siasa na kuangalia kile ambacho yeye anaona kitafaaa kuiongoza serikali bila migogoro kama inayojitokeza sasa. Hayo ameyasema leo katika makao makuu ya chama hicho yaliyopo Ilala-Bungoni jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari. Mbatia alisema kuwa, Rais Magufuli hawezi kukinzana na upinzani uliopo kwa sasa kwa kuzuia mikutano na maandamano wanayotaka kufanya k...

Mfanyabiashara Ataka Kujirusha Daraja la Ubungo

Image
    Shayo akiwa juu ya daraja. Gari la Jeshi la Zima Moto likiwa eneo hilo. Baadhi ya wananchi wakimshangaa Shayo (hayupo pichani). Shayo akiwa anavutwa baada ya kumpa mkono ndugu yake. Akiwa anapelekwa Kituo cha Polisi cha Ubungo. Katibu wa Chama cha Wafanyabiasha za Mezani katika maeneo ya Stendi ya Mkoa, Ubungo jijini Dar, John Shayo amekusanya umati baada ya kupanda juu kabisa ya daraja jipya lililopo eneo hilo na kutaka kujirusha, akihitaji Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda afike hapo kwani hakutendewa haki. Tukio hilo lililovuta hisia za wengi lilijiri kwenye Daraja la Ubungo ambapo katibu huyo alitaka afe kwa kuwa anadai hajatendewa haki na alitaka Makonda afike amwelezee shida zake katika suala zima la ufanyaji biashara ndipo aweze kushuka la sivyo angejirusha. Kundi kubwa la watu lilikusanyika eneo hilo huku polisi na gari lao la zima moto wakitanda wakimshangaa akiwa anazungukazunguka akisema yeye ni Mtanzania anahitaji haki ndipo w...

Breaking News: UKAWA Wakubali Kurudi Bungeni Baada ya Mkutano na Viongozi wa Dini

Image
  Vyama vya CHADEMA, NCCR MAGEUZI, CUF na ACT Wazalendo ambavyo vilisusia vikao vya bunge vimekubali kurejea bungeni baada ya mkutano wao na viongozi wa dini hapo jana

Zitto Kabwe afunguka yake kuhusu Oparesheni UKUTA

Image
  Wakati viongozi wa dini wakiendelea na jitihanda za kusaka suluhu kati ya upande wa Serikali na Chadema kuhusu namna ya kuzuia kwa amani kufanyika kwa Operesheni ya chama hicho iliyopewa jina la UKUTA, Septemba 1, Kiongozi Mkuu wa Chama Cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ametoa maoni yake. Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini amesema kuwa haoni haja ya kufanyika kwa vikao hivyo vya kusaka maridhiano kwani Chadema wanachotaka kufanya kiko kikatiba. “Sioni ni kwanini tunahangaika na vikao vya maridhiano na tahariri nyingi kuhusu shughuli ya CHADEMA kufanya operesheni yao ya UKUTA. Kuandamana ni Haki ya KIKATIBA. Tuache watu watimize Haki yao Kwa amani. Kuzuia watu kufanya jambo lao la kikatiba ndio kuvunja amani. Wanaotaka kuandamana waandamane na wanaotaka kufanya Kazi zao nyingine tuendelee na Kazi zetu. Kwanini kutekeleza Haki ya kikatiba iwe ni kuvunja amani? Kwanini?,” Zitto ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook. Hata hivyo, vikao vya maridhiano vi...

MIILI YA ASKARI WALIOUAWA NA MAJAMBAZI YAAGWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akipita kutoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yaliyobeba miili ya askari waliouawa baada ya kuvamiwa na majambazi katika eneo la Mbande, Temeke ,bada hiyo ya kuaga miili ilifanyika katika viwanja vya polisi vilivyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam. Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akitoa mkono wa pole kwa mmoja wa ndugu wa askari waliouawa baada ya kuvamiwa na majambazi katika eneo la Mbande, Temeke ibada hiyo ya kuaga miili ilifanyika katika viwanja vya polisi vilivyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni , akitoa mkono wa pole kwa mmoja wa ndugu wa askari waliouawa baada ya kuvamiwa na majambazi katika eneo la Mbande, Temeke ,ibada hiyo ya kuaga miili ilifanyika katika Viwanja vya Kambi Kuu ya Polisi iliyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam. Waziri wa Wi...

GARI ALILO PEWA ZAWADI MSANII RAYMOND KATIKA BIRTHDAY YAKE,LINA THAMANI YA TSH. MILIONI 20 0

Image

Exclusive: Vijana Waiba Baraghashia ya Mzee Akilimali, Achimba Mkwara Mzito

Image
Mzee Ibrahim Akilimali maarufu kwa jina la Mzee Akilimali. Taarifa zilizotufikia ni kuwa Mzee Ibrahim Akilimali maarufu kwa jina la Mzee Akilimali ambaye ni katibu wa Baraza la Wazee wa Klabu ya Yanga, amelalamika kuwa kofia yake aina ya baraghashia imeibiwa na mtu ambaye hajajulikana. Baada ya kuibiwa Mzee Akilimali ametoa mkwara mzito kwa yeyote ambaye amehusika kuiiba kofia hiyo ambayo muda wote amekuwa akionekana hadharani ameivaa. Mtu wa karibu wa Mzee Akilimali amesema kuwa mzee huyo alikutwa na mkasa huo jana alipokuwa ameenda kumtembelea mzee mwenzake aliyemtambulisha kwa jina la Mzee Mwika. “Sasa alipofika pale wakawa wamekaa wanapiga soka za hapa na pale, baada ya muda wakatengewa chain a vitumbua lakini Mzee Akilimali yeye huwa anapendelea mihogo na siyo mlaji wa vitumbua, akiwa amevua kofa yake, akaenda jirani kununua mihogo,” alisema mtu huyo wa karibu na mzee huyo. Mtu huyo wa karibu akaendelea kusimulia kuwa: “Aliporejea hakuikuta kofia yake hata ...

Prof. Lipumba Akana Kuhusika na Vurugu Mkutano wa CUF

Image
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba amesema kuwa hausiki na vurugu zilizoibuka katika mkutano mkuu wa chama hicho uliovunjika juzi Jumapili, Agosti 21, wakati wa uchaguzi wa kujaza nafasi zilizo wazi. Akieleza hayo jana Jijini Dar es Salaam, Prof. Lipumba amekiri kuwa hakualikwa katika mkutano huo lakini aliombwa na baadhi ya wajumbe kwenda kutoa maelezo ya kwanini aliachia nafasi hiyo ya uenyekiti jambo ambalo viongozi waliokuwepo ukumbini hapo hawakulitaka. Prof. Lipumba amesema kuwa anaheshimu maamuzi ya pande zote mbili kwa wanaomtaka arejee nafasi ya uenyekiti lakini pia maamuzi ya chama endapo utaratibu utafuatwa kwa kufuata katiba ya chama na demokrasia ya kweli ndani ya chama hicho. Prof. Lipumba amekataa kuhusika na kukana kutumika na kisiasa na baadhi ya watu ili kukivuruga chama hicho na kusema kuwa viongozi wa chama hicho waepuke maneno ambayo yataweza kukigawanya chama hicho na badala yake wajikite katika kudumi...

Mghwira wa ACT-Wazalendo Azindua ‘Tanzania Role Model’

Image
       Mwenyekiti wa Chama cha  ACT-Wazarendo, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo,  Anna Mghwira, akizindua mashindano hayo. …Akifafanua jambo mbele ya warembo wanaoshiriki shindano. Mratibu wa mashindano hayo, Samweli Charles (wa kwanza kushoto) akizungumza jambo kabla ya kumkaribisha  Mghwira. Viongozi wakifuatilia nyendo za warembo waliokuwa wakipita mbele yao. Baadhi ya washiriki wa Tanzania Role Model wakifanya vitu vyao mbele ya mgeni rasmi. Baadhi ya ‘manjonjo’ yaliyoonyeshwa na warembohao. Washiriki wakitambulishwa mbele ya mgeni rasmi. Mshereheshaji ‘MC’ wa hafla hiyo, Sufian Juma (wa kwanza kushoto) akizungumza jambo baada ya shindano kuzinduliwa. MWENYEKITI wa  ACT-Wazalendo na aliyekuwa mgombea urais kupitia chama hicho, Mama Anna Mghwira,  jana alizindua shindano lijulikanalo kama ‘Tanzania Role Model’ lililoandaliwa na kampuni ya Mass Television  Company (MTV) chini ya mkuruge...

PICHA LOWASSA BAADA YA KUTUA MBEYA

Image
 

Beki Simba aanguka bafuni, apasuka kichwani

Image
Mchezaji wa Coastal Union,Hamad Juma akiwa ameanguka chini huku mchezaji wa Simba, Hassan Kessy (kulia) akichanja mbuga kuelekea golini kwao mechi ya Ligi Kuu msimu uliopita. Wilbert Molandi, Dar es Salaam BEKI mpya wa kulia wa Simba, Hamad Juma, jana asubuhi alianguka bafuni akiwa nyumbani kwake na kusababisha achanike kisogoni kwake. Juma alijiunga na Simba msimu huu wa Ligi Kuu Bara akisaini mkataba wa mwaka mmoja akitokea Coastal Union baada ya mkataba wake kumalizika. Kwa mujibu wa taarifa ambazo Championi Jumatatu limezipata jana jioni na kuthibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, tukio hilo lilitokea nyumbani kwake kabla ya kukimbizwa Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam alipokwenda kulazwa. Manara alisema, beki huyo mara baada ya kufikishwa hospitalini hapo, madaktari walishauri alazwe kutokana na damu nyingi zilizokuwa zinamtoka. “Hamad ameanguka na amepoteza damu nyingi sana, alipata matatizo hayo akiw...

Askari wa Upelelezi Mwanza Auawa Club Akidai Laptop

Image
  Tarehe 21.08.2016 majira ya 10:00 usiku katika eneo la Club ya Villa Park Resort Kata ya Kirumba Wilaya ya Ilemela Mkoa wa Mwanza, askari namba g.5092 PC John Nyange wa Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi na Makosa ya Jinai Mkoa wa Mwanza (RCP), aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali eneo la shingoni na mtu aliyekuwa anaugomvi nae. Inadaiwa kuwa marehemu alikua na ugomvi wa muda mrefu na mtu aliyejulikana kwa jina Magina Hussein miaka [27] fundi computer Msukuma na mkazi wa Mtaa wa Kigoto, ambapo marehemu alikuwa akimdai Bwana Magina Hussein computer aina ya laptop.  Ndipo usiku wa leo majira tajwa hapo juu walikutana eneo la club ya Villa Park huku mtuhumiwa wa mauaji hayo ikisemekana kuwa alikuwa na wenzake watano ndipo walimvamia na kumchoma na kitu chenye ncha kali shingoni na kufariki dunia njiani wakati akipelekwa hospitali. Marehemu kwa sasa alikuwa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Stefano Moshi Memorial University College cha Mjini Moshi, ali...

Jeshi la Polisi Likifanya Mazoezi ya Utayari wa Kukabiliana na Uhalifu

Image
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wa wakiwa moja ya maozezi yao ya kupasha viungo kabla ya kuanza mazoezi ya kutuliza ghasia. Askari Polisi wa kikosi maalum cha polisi (CRT) wa mkoa wa Iringa wakiwa katika mazoezi ya utayari wa kukabiliana na matukio yoyote yatakayojitokeza katika maeneo mbalimbali. Askari wa vikosi vya kutuliza ghasia wa mikoa mbalimbali wakiwa na magari yao wakati wa mazoezi ya utayari wa kupambana na matukio mbalimbali ya uhalifu na wahalifu katika maeneo mbalimbali. Askari wa vikosi vya kutuliza ghasia wa wakiwa na magari yao wakati wa mazoezi ya utayari wa kutuliza ghasia na kukabiliana na matukio yoyote ya uhalifu na wahalifu. Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoa wa Lindi wakifanya mazoezi magumu ya kijiweka tayari kukabiliana na matukio yoyote yatakayojitokeza ikiwemo watu wasiotii amri za Jeshi la Polisi ikiwa ni pamoja na kutofuata sheria za nchi. Askari Polisi wa vikosi vya kutuliza ghasia  wa mikoa ya Li...