Mghwira wa ACT-Wazalendo Azindua ‘Tanzania Role Model’

1       Mwenyekiti wa Chama cha  ACT-Wazarendo, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo,  Anna Mghwira, akizindua mashindano hayo.
2…Akifafanua jambo mbele ya warembo wanaoshiriki shindano.
3Mratibu wa mashindano hayo, Samweli Charles (wa kwanza kushoto) akizungumza jambo kabla ya kumkaribisha  Mghwira.
4Viongozi wakifuatilia nyendo za warembo waliokuwa wakipita mbele yao.
5Baadhi ya washiriki wa Tanzania Role Model wakifanya vitu vyao mbele ya mgeni rasmi.
6Baadhi ya ‘manjonjo’ yaliyoonyeshwa na warembohao.
7Washiriki wakitambulishwa mbele ya mgeni rasmi.
8Mshereheshaji ‘MC’ wa hafla hiyo, Sufian Juma (wa kwanza kushoto) akizungumza jambo baada ya shindano kuzinduliwa.
MWENYEKITI wa  ACT-Wazalendo na aliyekuwa mgombea urais kupitia chama hicho, Mama Anna Mghwira,  jana alizindua shindano lijulikanalo kama ‘Tanzania Role Model’ lililoandaliwa na kampuni ya Mass Television  Company (MTV) chini ya mkurugenzi wake, Samweli Charles.
Uzinduzi huo ulifanyika katika hoteli ya  Oceanic Resort iliyopo Mbweni jijini Dar es Salaam ambapo jumla ya washiriki 17 waliwakilisha  hifadhi 17 za mbuga za wanyama hapa nchini.
Akizungumza katika uzinduzi huo, mratibu wa mashindano hayo, Samwel Charles, alisema kuwa washiriki watakaa kambini kwa muda wa miezi mitatu wakitembelea hifadhi za taifa kama mpango wa kuhamasisha na kukuza utalii wa ndani kupitia warembo hao.
Naye mgeni rasmi katika hafla hiyo,  Anna Mghwira,  alisema kuwa nchi hii ina utajiri mkubwa wa asili tatizo lipo katika kuutangaza, hivyo kwa kupitia mashindano hayo  nchi inaweza kuutangaza utajiri huo hususani kwa kupitia utalii.
Alisema kila mwananchi anayepewa fursa ya kwenda katika mbuga za hifadhi ahakikishe anakuja na takwimu nzima ya hifadhi husika juu ya mambo atakayoyaona nakuyawasilisha katika jamii ili kuyatangaza.
Aidha, washiriki hao wakiwa kambini wataweza kujifunza mambo mbalimbali kama vile masuala ya mazingira,  afya, vipaji, elimu  na mengineyo.
Mghwira aliwataka Watanzania kufuatilia shindano hilo kwani linahamasisha uhifadhi wa mbuga zetu na akawataka wafadhili wengine kujitokeza kwani ni moja ya fursa za wao kujitangaza shughuli zao kibiashara.
NA DENIS MTIMA/ GPL

Comments

Popular posts from this blog