Mrembo afanyiwa kitu mbaya
Mrembo huyo akiongea na simu kuomba msaada. Na Chande Abdallah, AMANI Dar es Salaam: Hatari! Mrembo aliyetambulika kwa jina moja la Saida, amefanyiwa kitu mbaya kweupe baada ya kukombwa vitu vyote na mwanaume aliyedaiwa kutoka naye baa aliyemsukuma kutoka ndani ya Bajaj waliyopanda na kumsababishia majereha. Tukio hilo likiwa ni mfululizo wa mengi yanayotokea maeneo ya Sinza, Afrika Sana jijini Dar, hasa nyakati za alfajiri, hivi karibuni wapita njia wa eneo hilo walisema kuwa walimuona Saida akitokea kwenye baa moja maarufu eneo hilo akiwa na mwanaume huyo asiyejulikana. Ilidaiwa kwamba, wawili hao walionekana wakiyumba kutokana na kukesha wakipata kinywaji, walipanda Bajaj kisha ikaanza kuondoka lakini kabla hawajafika mbali ndipo wakamuona mrembo huyo akidondoka huku Bajaj ikitokomea kusikojulikana. “Alipoinuka, alikuwa amechafuka sana na ameumia begani, damu zilikuwa zikimtoka ndipo akarudi tena hapa baa lakini wahudumu waligoma kumpokea, wakamweka nje,” alisema...