Mike Tyson auza mjengo wake wa Las Vegas

Mike-Tyson-news-2016
Mike Tyson.
-UNGEPENDA kuishi kistaa na una kiasi cha Dola za Marekani Usd milioni 1.5 sawa na shilingi bilioni 3.3?
Kama hivyo ndivyo, basi unaweza kununua mjengo wa kifahari wa mwanamasumbwi wa zamani wa Marekani, Mike
Tyson.
Staa huyo ameishi katika mjengo huo wenye futi za mraba 5,800 tangu mwaka 2008 ila sasa ameamua kuhamia
kwenye mjengo mpya wenye vyumba vitano vya kulala na mabafu sita.
mike
Mbali na kuhama, mjengo huo bado hauko vibaya maana una sehemu tatu za kupashia moto nyumba (fireplaces), chumba cha kukutana na wahabari, sehemu ya kunywea mvinyo, eneo la kuchezea pool na maporomoko yaliyo sehemu ya kuingilia jumba hilo.
Wakala wa Tyson, Ken Lowman, ameeleza kuwa eneo hilo lote limefanyiwa maboresho mapema mwaka huu na
lipo katika muonekano mzuri japo linakosa kitu kimoja ambacho ni sehemu ya kufugia chui.

Comments

Popular posts from this blog