WOLPER AKIVISHWA PETE TU KWISHA HABARI YAKE!
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper. KUMBE! Waliosema ujana maji ya moto hawakukosea kwani una changamoto nyingi hasa pale unapofikia wakati wa kumtafuta wa kuwa naye maishani yaani mke au mume. Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe anaweza kuthibitisha hilo baada ya uchunguzi kuonesha kuwa ana listi ya wanaume waliomvisha pete za uchumba kisha wakapata walichokitaka, wakaingia mitini. Uchunguzi huo ulibaini kwamba, wanaume wengi wamekuwa wakitumia gia hiyo kumrubuni na kumwachia maumivu makali ya moyo. Katika makala haya tunakuletea listi ya wanaume ambao waliwahi kuwa na Wolper na kumvisha pete za uchumba na wengine kujitambulisha au kumtambulisha kabisa kwa wazazi lakini baada ya kumfaidi wakammwaga na kujikuta akihamia kwa mwingine, jambo ambalo watu wengine ambao ni mashabiki wake wamekuwa wakihoji ana nini mpaka yamkute hayo? ABDALLAH MTORO ‘DALLAS’ Mfanyabiashara huyo aliyekuwa na fedha ‘chafu’ alianzisha uhusiano na Wolper ambapo alimvisha pete ya u