Gari la Wema mikononi mwa Rais Magufuli


WEMA37 (1)Hali ni tete! Chanzo kimoja kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kimenyetisha kwamba, kasi ya Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ kuhakikisha hakuna Mtanzania anayekwepa kodi imepamba moto na sasa, imetua kwa mastaa wa Bongo ambapo kuna madai lile gari la kifahari la Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu (pichani) aina ya Range Rover Evogue linachunguzuwa na TRA, Amani limenyetishiwa.
SI YEYE TU
Kwa mujibu wa chanzo hicho, mbali na Wema, mastaa wengine ambao nao magari yao yako kwenye orodha ya kuchunguzwa mwenendo wa kodi ni Jacqueline Wolper Massawe (Toyota Prado), Kajala Masanja (Toyota Hilux) na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ (BMW X6).
8MAELEZO YAKO HIVI
“Unajua serikali imedhamiria kukusanya kodi. Anachotaka Rais Magufuli ni kila mtu mwenye haki ya kulipa kodi ya kitu fulani, afanye hivyo bila kukwepa. Na hakuna kumuonea mtu.
“Sasa bwana…bwana! Huko makao makuu (TRA) hakukaliki, huyo Kaimu Kamishna Mkuu, Phillip Mpango ni mkali balaa, anadhani Magufuli atamzukia wakati wowote wakati cheo kapewa juzi tu. Lakini nasikia Magufuli anataka ripoti mezani kwake.
“Na ujue si magari ya hao mastaa tu ndiyo yako kwenye orodha, hata watu wasio na majina hapa mjini, utaratibu umewekwa kuhakikisha magari yote yanalipiwa kodi kama sheria inavyotaka. Kwa hiyo kama mtu ana malimbikizo, imekula kwake, lazima alipe yote,” kilisema chanzo hicho.
WASIWASI WA VIPATO
Hata hivyo, chanzo hicho kilipoulizwa kama kuwabana mastaa kunatokana na maisha yao ya kifahari huku vipato vyao vikiwa haviko wazi, alijibu: “Ni zoezi. Linazingatia mambo mengi. Pengine hilo limo. Lakini ni zoezi maalum.”
ymCTBkpAMANI LAWASAKA
Ili kuthibitisha madai hayo, Amani lilianza kuwasaka mastaa hao, mmoja baada ya mwingine ili kuona ukweli wa kuwepo kwa madai hayo.
WOLPER
Wolper alikuwa wa kwanza kutafutwa kwa simu ambapo alipopatikana alishtuka na kusema:
“Yesu! Sijafuatwa na mtu yeyote, lakini na mimi jana (Jumatatu) nimeisikia hii. Lakini mimi nipo oke, ushuru nimeshalipa mwenyewe. Kimbembe kipo kwa wale wenye mbwembwe ndiyo nasikia soo…Teh! Teh! Teh!”
KAJALA
Kajala alipotafutwa kwa njia ya simu ya mkononi juzi, hakupatikana hewani.
WEMA SASA
Amani likamsaka Wema ambaye kwa bahati njema alikuwa hewani na alipokea simu. Baada ya kusomewa madai hayo, alijibu:
wema3“Usumbufu ulianza wakati linaletwa (mwezi Oktoba) lakini haukuwa mkubwa. Ila hivi karibuni walikuja jamaa wa TRA kwa mambo ya miliki. Lakini kuna huyu jamaa yangu (hakumtaja jina) alimalizana nao, ongea naye.”
Jamaa: “Ni jambo dogo tu, wala siyo ishu kubwa. Kwani nani kasema?”
Amani: “Tumezinyaka kivyetuvyetu.”
DIAMOND
Kwa upande wake, Diamond ilionekana kuwa ishu zaidi kwani, licha ya yeye kutojibu meseji baada ya kutumiwa, BMW X6 lake linadaiwa bado lina deni kutoka kwa mtu aliyemuuzia. Na mbaya zaidi, mtu huyo alifariki dunia Aprili, mwaka huu.
MANUNUZI YAO
Wema alisema Range lake alilinunua kwa dola za Kimarekani 90,000 (si chini ya shilingi milioni 200). Diamond yeye awali alisema BMW hilo alipewa na mameneja wake (Said Fella na Hamis Taletale ‘Babu Tale’) ambao walilinunua kwa shilingi milioni 90.
Wolper yeye Prado lake aliliingiza ndani kwake kwa shilingi milioni 60 huku gharama ya gari la Kajala zikiwa hazijulikani.

Comments

Popular posts from this blog