Posts

MOTO WATEKETEZA MAROLI MAWILI YA MAFUTA MWANZA

Image
Malori mawili ya mafuta yameteketea kwa moto uliosababishwa na hitilafu ya Jenereta iliyokuwa inatumika kushusha mafuta kutoka ndani ya malori hayo kwa ajili ya kuyahifadhi kwenye kisima cha mafuta cha sasa kazi kilichopo eneo la Butimba kona jijini Mwanza na kusababisha hasara ya mamilioni ya shilingi,sambamba na kuteketea kwa pikipiki moja mali ya Ayoub Ismail. Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea majira ya saa 4.30 asubuhi wanasema malori hayo aina ya SCANIA – moja lenye namba za usajili T 509 AFD na Tela lake namba T 592 ACL lililokuwa limebeba lita 35 za mafuta ya Dizeli pamoja na lori jingine lenye namba za usajili T 674 AHH ambalo lilikuwa limeegeshwa kando kidogo ya kituo hicho cha mafuta cha sasa ni kazi yameteketea na kusababisha wingu kubwa la moshi mweusi,huku juhudi za wananchi kuzima moto huo uliokuwa ukiwaka kwa kasi ya ajabu zikigonga mwamba. Muda mfupi magari ya jeshi la zimamoto na uokoaji jijini Mwanza yakawasili katika eneo la tuki...

MASHA AACHIWA KWA DHAMANA

Image
Lawrence Masha akiwa na wanachama wa Ukawa baada ya kuachiwa. Baada ya jana kulala mahabusu ya segerea, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha leo ameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana. Masha, ambaye anashitakiwa kwa kosa la kuwazuia Polisi wasifanye kazi ikiwa ni pamoja na kuwatolea lugha ya matusi. Jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo alisomewa mashtaka ambayo aliyakana lakini ikalazimu apelekwe mahabusu ya Segerea baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

BREAKING NEWS UKAWA WAZUIWA KUZINDUA KAMPENI JANGWANI

Image
Cloudsfm Radio ‪#‎News‬ UKAWA Wazuiwa kuzindua kampeni Jangwani Jiji la Dar es Salaam wamemzuia Mgombea waUKAWA, Edward Lowassa kuzindua kampeni yake kwenye viwanja vya Jangwani Jumamosi ya 29 Agosti , 2015 .Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA , James Mbatia amesema jiji umewagomea kufanya uzinduzihuo Jangwani kwa madai kuwa tayari kuna mtu mwingine ambaye ameshalipia uwanja huo.Mbatia anasema pamoja na kufanya juhudi zakuomba kutajiwa aliyelipia uwanja huo iliwazungumze naye , Jiji walikataa.Mbatia anasema viongozi wengine wa UKAWA wanashughulikia suala hilo ikiwa pamoja nakumtaka Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Damian Lubuva kuingilia kati.

BREAKING NEWS : FEDHA ZA KAMPENI YA LOWASSA ,UKAWA NA CHADEMA MAKUBWA YAIBUKA

Image
Kwa mujibu wa habari nyeti nilizotonywa sasa hivi kuna kizazaa cha fedha za kampeni zinazowafanya Lowassa, Chadema na UKAWA kwa ujumla kuwa katika mtafuruku mkubwa na mpaka sasa uliopelekea kuchelewa kuanza uzinduzi wa kampeni ya Urais wa ukawa. Vyama vinayounda UKAWA vinasema Lowassa aliahidi kuwa atatowa fedha zote za kampeni kwa hiyo wao wasiulizwe. Lowassa anasema alizotowa zinatosha (hasemi katowa kampa nani na za nini), Chadema nao wanavunga kuwa mpaka sasa akaunti ya kutowa kiasi kikubwa cha fedha ni lazima saini ya Katibu Mkuu iwepo na Katibu Mkuu wa chadema alipofatwa kusaini yeye kagoma ( huu ni ungo wa chadomo) wanasema eti Katibu Mkuu wao anataka kwanza taratibu za kubadili saini yake zikamilike kama watatowa fedha watowe wenyewe akikamilisha zoezi la kubadili kuwa ndiyo anawakwamisha. Kizungumkuti kinaendelea wakati marafiki matajiri waliokuwa wanampa fedha azitakazo Lowassa wameona mambo yanakuwa magumu na badala ya fedha wameanza kumpa ahadi za ke...

RAIS KIKWETE ASHIRIKI MAZISHI YA MTOTO WA JAJI MKUU MJINI TANGA

Image
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Jaji Mkuu Mhe.Mohamed Chande Othman kufuatia kifo cha mwanaye Said Mohamed Chande wakati Rais alipokwenda Chumbageni Tanga kuhudhuria mazishi ya marehemu. Jaji Mkuu Mhe.Mohamed Chande Othman akiweka udongo katika kaburi la mwanaye Said Mohamed Chande wakati wa mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Chumbageni Tanga leo jioni. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Said Mohamed Chande wakati ya mazishi yaliyofanyika katika eneo la Chumbageni Tanga leo.Marehemu Said ni Mtoto wa Jaji Mkuu Mhe.Mohamed Chande Othman. Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal akiweka udongo katika kaburi la mrehemu Said Mohamed Chande wakati wa mazishi yaliyofanyika huko Chumbageni Tanga. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal,Jaji Mkuu Mhe.Mohamed Chande Othman wakiomba dua wakati wa mazishi ya marehemu Said Mohamed Chande ambaye ni mtoto wa jaji mkuu yaliyofa...

LOWASSA AFUNGUKA KUHUSU MAISHA YAKE KISISASA

Image
Edward Ngoyai Lowassa 1 hr   ·   Facebook Mentions   ·   Leo ninasherehekea siku yangu ya kuzaliwa na kwa namna ya pekee ninamshukuru Mungu kwa kuendelea kunibariki, kunishika mkono na kuniongoza. Maisha yangu ni mfano wa baraka za Mungu. Kuna nyakati nilianguka lakini  kwa upendo wake akaninyanyua na mpaka sasa ameendelea kunionyesha baraka zake. Kwa namna ya pekee ninapenda kuishukuru familia yangu na watanzania wenzangu kiujumla kwa upendo na imani yao juu yangu hata pale nilipopitia vipindi vigumu katika maisha yangu. Nina furaha zaidi leo kwa kuwa ninasherehekea siku yangu ya kuzaliwa nikiwa katika kilele cha mapambano ya kusaidia wananchi wenzangu

Rais Kikwete afungua Mkutano wa Chama Cha Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashariki

Image
Rais Kikwete akifungua Mkutano wa siku tatu wa Chama Cha Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashariki unaofanyika katika Hoteli ya Malaika Beach Resort Mwanza. .Baadhi ya washiriki wa Mkuano huo. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano wa Chama Cha Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashariki (picha na Freddy Maro)

CHADEMA WAMJIBU KAMANDA KOVA

Image
Baada ya Kamishna wa Polisi kanda maalum ya Dsm kupiga marufuku Wagombea wa vyama vya siasa kufanya vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa wananchi katika maeneo mbalimbali ya jiji kama alivyofanya mgombea wa uraisi wa Chadema kwa kutembelea Gongo la mboto na kupanda daladala jambo ambalo limeleta taharuki pamoja na kusababisha shughuli za watu kusimama. Afisa habari wa Chadema, Tumaini Makene amesema Jeshi la polisi haliwezi kuwapangia nini cha kufanya. Wataendelea kufanya mikakati yao watakayoipanga ili mradi hawavunji sheria za nchi na sheria za uchaguzi

LOWASSA AZIDI KUWATEMBELEA WANANCHI DAR, NI MTAA KWA MTAA, NYUMBA KWA NYUMBA

Image
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Wazee wa Tandale, wakati alipotembelea Soko la Tandale, jijini Dar es salaam leo, akiambatana na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni (kushoto). PICHA ZOTE NA MTAA KWA MTAA BLOG Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakipata maelezo kutoka kwa Bw.Omari Juma (kulia) ambaye ni mfanyabiashara ya kuuza Maharage katika Soko la Tandale, Manzese Jijini Dar es salaam leo Agosti 25, 2015, wakati walipotembelea Soko hilo kujionea hali ya biashara masokoni. Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakiwapungia wananchi wa Tandale, Manzese Jijini Dar es salaam leo Agosti 25, 2015. Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demo...

KAZI ZASIMAMA SUMBAWANGA NI BAADA YA MAGUFULI KUWASILI NA KUONGEA NA WANANCHI

Image
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa Nelson Mandela ,Sumbawanga mjini tayari kuwahutubia wakazi wa mji huo.  Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kada wa CCM Mzee Chrisant Mzindakaya wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa Nelson Mandela ,Sumbawanga mjini.  Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Sumbawanga mjini Ndugu Aeshi Hilaly .  Kada wa CCM Mzee Chrisant Mzindakaya akiwahutubia wakazi wa Sumbawanga mjini kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Nelson Mandela.  Umati wa wakazi wa Sumbawanga mjini wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM ambapo mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.  Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda akimtambulisha mgombea w...