MREMBO MAARUFU BONGO AFIA NCHINI CHINA!!
Imelda Mtema Mrembo Mtanzania aliyejulikana kwa jina la Rehema Mohamed (30), anadaiwa kufia katika Mji wa Shanghai nchini China wiki mbili zilizopita baada ya kuugua kwa muda mrefu hadi mauti yalipomfika huku ndugu zake wakichanganyikiwa kutokana na taarifa za kifo hicho. Mwanadada Rehema Mohamed anayedaiwa kufia China. Habari zaidi kutoka kwa aliyekuwa rafiki wa karibu wa Rehema nchini China, (jina lake linahifadhiwa) zinasema kuwa wamekuwa wakihangaika ili kupata fedha za kusafirisha mwili huo lakini imekuwa ngumu kupatikana. Chanzo hicho kilisema kuwa kimefanya mawasiliano na baadhi ya ndugu wa marehemu ambao nao wanajikusanya kwa ajili ya kupata fedha hizo ili kuurudisha mwili nyumbani Dar kwa mazishi. “Yaani huku tunapata tabu sana na tuna uchungu kwa kuwa fedha zilikuwa zikihitajika nyingi sana lakini tunashukuru taratibu zinaenda sawa karibu tutaleta mwili nyumbani,” alisema rafiki huyo. Mmoja wa ndugu wa marehemu ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini,