WANANCHI KATA YA NZIHI JIMBO LA KALENGA WAMPONGEZA MBUNGE MGIMWA , MWENYEWE AWATAKA KUMPA USHIRIKIANO ZAIDI
Wazee kijiji cha Nyamihuu wakimpa baraka na kumpongeza mbunge Mgimwa kwa uchapa kazi wake MBUNGE wa jimbo la Kalenga Bw Godfrey Mgimwa amesema atahakikisha anafanya kazi na vyama vyote vya siasa na kuwa kuwataka wananchi wa jimbo la Kalenga kuachana na makundi ya vyama vya siasa na kuunagana pamoja ili kufanikisha jimbo hilo kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo. Mbali ya kuwataka kuachana na makundi ya kisiasa pia amewataka waliokuwa wagombea wa nafasi za ubunge katika uchaguzi mdogo kupitia CCM kuacha kujipitisha kwa sasa kwa wananchi na badala yake kusubiri uchaguzi mkuu mwaka 2015. Akizungumza kwa nyakati tofauti katika mikutano yake ya hadhara kwa lengo la kuwashukuru wananchi kwa kumchagua na leo katika kata ya Nzihi ,mbunge huyo alisema kuwa amelazimika kuomba ruhusa bungeni kwa spika ili kurudi kuwashukuru wananchi hao hasa kutokana na upendo mkubwa ambao wananchi wa jimbo hilo walionyesha kwake. “Ndugu