WANANCHI KATA YA NZIHI JIMBO LA KALENGA WAMPONGEZA MBUNGE MGIMWA , MWENYEWE AWATAKA KUMPA USHIRIKIANO ZAIDI
MBUNGE wa
jimbo la Kalenga Bw Godfrey Mgimwa amesema atahakikisha anafanya kazi na
vyama vyote vya siasa na kuwa kuwataka wananchi wa jimbo la
Kalenga kuachana na makundi ya vyama vya siasa na kuunagana pamoja
ili kufanikisha jimbo hilo kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo.
Mbali ya
kuwataka kuachana na makundi ya kisiasa pia amewataka waliokuwa
wagombea wa nafasi za ubunge katika uchaguzi mdogo kupitia CCM
kuacha kujipitisha kwa sasa kwa wananchi na badala yake kusubiri
uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Akizungumza
kwa nyakati tofauti katika mikutano yake ya hadhara kwa lengo la
kuwashukuru wananchi kwa kumchagua na leo katika kata ya Nzihi ,mbunge
huyo alisema kuwa amelazimika kuomba ruhusa bungeni kwa spika ili
kurudi kuwashukuru wananchi hao hasa kutokana na upendo mkubwa ambao
wananchi wa jimbo hilo walionyesha kwake.
“Ndugu
zangu nilianza kuzunguka katika baadhi ya maeneo na kutekeleza ahadi
mbali mbali hata kabla ya kuapishwa rasmi bungeni ……na nitajitahidi
kulingana na uwezo wangu ili kuona natimiza wajibu wangu kwenu na
kamwe sitawaangusha ndani ya bunge na nje ya bunge”
Hivyo
aliwataka wananchi kwa umoja wao kuendelea kumuombea afya njema
ili kufanikisha kutimiza ndoto yake ya kufikisha maendeleo katika
jimbo hilo ikiwa ni pamoja na kutimiza sehemu kubwa ya ahadi ambazo
zilitolewa na marehemu Dr Wiliam Mgimwa aliyekuwa mbunge wa jimbo
hilo.
Kuhusu
suala la kuyawezesha makundi mbali mbali Mbunge Mgimwa aliwataka
wananchi kujiunga na vikundi vya VICOBA ili kuviwezesha vikundi
hivyo kiuchumi zaidi badala ya kuwa mtu mmoja mmoja na kuwataka
wazee pia kuanzisha umoja wao na kupeleka mahitaji yao katika
ofisi yake.
“Kuna
vikundi vya VICOBA ambavyo tayari vimeanzishwa na moja kati ya
vikundi hivyo tayari nimechangia kiasi cha Tsh 500,000 na
nitaendelea kuchangia na kuna eneo ambalo marehemu mbunge wetu
aliyepita aliahidi kuchangia milioni 1 katika kikundi cha VICOBA
Magubike nasema fedha hizo nitazitoa mimi “
Alisema
kuwa tayari ameanza kupigania suala la umeme na maji katika vijiji
vya jimbo la Kalenga bungeni na kuwa mawaziri wa wizara hizo
wameahidi kulifanyia kazi na kuendelea kusaidia miradi hiyo mikubwa
ambazo ndizo ahadi kubwa zaidi.
Awali
wananchi wa kijiji cha Magubike walimpongeza mbunge huyo na kuwa
katika historia ya jimbo la Kalenga hawajapata kuwa na mbunge mkweli
na mchakakazi kama huyo na kurudi mapema zaidi kwa wananchi kuwashukuru
na hivyo kumhakikishia kuwa hawana mpango wa kumchagua mbunge mwingine
mwaka 2015 na kukiomba chama cha mapinduzi kumbariki kuendelea
kuongoza jimbo hilo .
Kwa
upande wake katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Iringa Denis Lupala
alisema kuwa utendaji kazi mzuri wa mbunge huo ndio ambao
unakishawishi chama kuendelea kumpa ushirikiano zaidi na kuwa wananchi
hawana sababu ya kubabaishwa na wapinzani ambao wameanza kujipitisha
katika jimbo hilo.
Comments
Post a Comment