MSANII MWINGINE ALAZWA, NI SIKU CHACHE BAADA YA KUTOA WOSIA WA KIFO

Siku chache baada ya kutoa wosia kuwa akifa asizikwe kwa mbwembwe, mwigizaji Devotha Mbaga amezimia ghafla wakati wa kuaga mwili wa mwongozaji wa filamu na vipindi mbalimbali Bongo, marehemu George Otieno ‘Tyson’.

Kwa mujibu wa chanzo kilichoomba kusitiriwa jina (msanii), baada ya mwili wa Tyson kuagwa katika Viwanja vya Leaders Club, Juni 5, mwaka huu, ghafla Devotha alikutwa amezimia kwenye gari lake.
 Hatukujua sababu lakini kiukweli hali yake ilikuwa mbaya sana, tulimchukua na kumkimbiza Hospitali ya Mico, Kinondoni ambapo alilazwa na madaktari waligundua kwamba alikuwa na tatizo la presha
alisema msanii huyo.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mapaparazi wetu walifika katika Zahanati ya Mico alipokuwa amelazwa na kumkuta msanii huyo akiwa amewekewa dripu huku akizungumza kwa shida akidai hakujua kilichoendelea mpaka aliposhtuka akiwa kitandani hospitalini hapo.
Nilikuwa nimejiandaa kuusindikiza mwili wa Tyson mpaka airpot, nilikuwa ndani ya gari langu tayari lakini cha kushangaza sikujua kinachoendelea tena zaidi ya kujikuta hapa hospitalini nikiwa nimewekewa dripu, wasanii wenzangu wamenizunguka.
Madaktari wamesema ni presha imepanda sana na nimechomwa sindano ndiyo angalau sasa najisikia ahueni kidogo
alisema Devotha.
Kwa upande wake msanii Fatuma Makongoro ‘Bi Mwenda’ ambaye alikuwa hospitalini hapo alisema, inawezekana sababu ya Devotha kupandwa na presha kiasi hicho ni kutokana na vifo vya wasanii vilivyotokea mfululizo.
Unajua wasanii hatujapumzika kabisa kama mwezi mzima kwani wasanii watatu wamefariki dunia kwa kufuatana na Devotha alikuwa ni mmoja wa wanakamati, kwa hiyo ile mikikimikiki ndiyo iliyomfanya awe na hali hii ila tunamuombea Mungu apone
alisema Bi Mwenda.
Katika moja ya machapisho yetu mwanzoni mwa wiki Devotha alikaririwa kuwa endapo atafariki, hahitaji mbwembwe za kununuliwa vitu vingi vya gharama kama jeneza katika maziko yake, badala yake akashauri fedha hizo bora wapewe wanawe atakaowaacha duniani.

Comments

Popular posts from this blog